Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hongera Twiga Stars, ipewe nguvu zaidi

KIKA 04

Muktasari:

  • Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, Stars ilishinda mabao 2-0, na kusafiri hadi Addis Ababa kumalizia kazi kwa bao la Diana Lucas na kufuzu fainali hizo zitakazofanyika Morocco mwaka 2026.

TIMU ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars imefuzu kwa mara ya tatu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) baada ya kuifunga Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-0, baada ya kushinda bao 1-0 ugenini.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, Stars ilishinda mabao 2-0, na kusafiri hadi Addis Ababa kumalizia kazi kwa bao la Diana Lucas na kufuzu fainali hizo zitakazofanyika Morocco mwaka 2026.

Tunaipongeza Stars kwa kupambana hadi kufikia hatua hiyo na imeonyesha ubora katika harakati zao tangu mwanzo chini ya Kocha Bakari Shime.

Tunaamini huu ni mwanzo wa mafanikio zaidi yanayowasubiri huko mbele na hasa katika fainali za Morocco na inatakiwa ifanye kweli.

KIKA 02

Fainali za WAFCON ambazo zimepangwa kufanyika kuanzia Machi 17 hadi Aprili 3, ndizo zitakazotoa mataifa manne yatakayoiwakilisha Afrika katika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwaka 2027.

Kabla ya kukutana na Ethiopia, Twiga Stars ilionyesha ubora wao kwa kuiondosha Equatorial Guinea, taifa ambalo limewahi kushinda WAFCON mara mbili.

Huo ulikuwa ujumbe mzito kwa wapinzani wa Afrika kuwa Tanzania haitaki tena kuwa wasindikizaji katika mashindano ya wanawake na kama ilivyokuwa miaka ya nyuma imepania kufanya makubwa ikiwa na kikosi chake bora.

Stars ilishindwa kuvuka hatua ya makundi katika fainali mbili zilizopita na safari hii ikionekana kuwa imara zaidi itatakiwa kupiga hatua zaidi kuvuka hatua ya makundi na kucheza robo fainali au zaidi, jambo ambalo linawezekana iwapo maandalizi yatafanywa mapema.

Tunatamani kuiona Stars ikiwa miongoni mwa mataifa manne bora ya Afrika yatakayoiwakilisha bara hili kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake mwaka 2027 nchini Brazil. Hii ni nafasi ya kuandika historia ambayo haijawahi kufikiwa na taifa letu.

Ili kufikia huko, tunakumbusha tena TFF na serikali kwa jumla zinapaswa kuhakikisha maandalizi yanaanza mara baada ya kufuzu.

KIKA 03

Stars ipangiwe mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu bora ili kuimarisha uzoefu na uthubutu wa kimashindano. Wapo wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa, tunaamini wakiwekwa pamoja mapema, watatengeneza kikosi imara zaidi kitakachofika mbali kwenye fainali za WAFCON.

Hatua iliyopiga Tanzania kisoka si ya kurudi tena nyuma. Watanzania wanaamini kwa kikosi cha Twiga Stars cha sasa kina uwezo wa kucheza fainali hizo za WAFCON na hata za Kombe la Dunia na kinachotakiwa ni kuweka mikakati ya kufanikisha ndoto hiyo.

Kocha Shime ana kazi ya kufanya kuanzia sasa baada ya kufuzu WAFCON kuandaa jeshi lake ili likafanye kweli Morocco.,

Tunaamini kwa ubora walioonyesha katika michezo ya kufuzu, ndivyo watakavyoonyesha katika WAFCON ambayo maandalizi yake yanatakiwa kuanza mapema.

Pia wadau na mashabiki wa soka waipe sapoti kubwa timu hii kwani imekuwa ikifanya vyema na kuzidi kuipaisha Tanzania. Ni vyema kuzipa timu zote za taifa sapoti kubwa kwani ndizo zinazotuwakilisha kimataifa.