Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hongera Tanzania kwa rekodi CAF, tusilale

HONGERA Pict

Muktasari:

  • Simba SC na Yanga SC zimefuzu hatua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam FC na Singida Black Stars Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la Tanzania Bara, timu zote nne zilizoiwakilisha nchi katika mashindano ya klabu ya Afrika zimefuzu hatua ya makundi.

Simba SC na Yanga SC zimefuzu hatua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam FC na Singida Black Stars Kombe la Shirikisho Afrika.

Huu ni mwanzo mpya wa zama za mafanikio kwa soka nchini, hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa katika miaka yote ya ushiriki wa klabu za Tanzania kwenye mashindano ya CAF. Ni ishara soka la Tanzania linaendelea kukua kimfumo, kifedha na kimkakati.

CA 01
CA 01

Simba na Yanga zimeendelea kuwa nguzo kuu za mafanikio haya, zikitumia uzoefu na uwekezaji mkubwa hasa benchi la ufundi na wachezaji wenye ubora wa kimataifa.

Simba kwa upande wake imeweka historia ya kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya sita mfululizo, rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na klabu yoyote ya Tanzania, huku Yanga ni mara nne mfululizo, jambo linaloonyesha uthabiti na mwendelezo wa maendeleo ya klabu.

CA 03

Azam, ambayo kwa miaka 21 imekuwa ikijaribu kujenga klabu ya kisasa na yenye ushindani, hatimaye imevuna matunda kwa kufuzu makundi kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Hii ni hatua muhimu inayothibitisha uwekezaji wa muda mrefu katika klabu, bila kukata tamaa, unaweza kuleta matokeo makubwa.

Kwa upande mwingine, Singida Black Stars imeandika historia yake binafsi kwa kufuzu makundi katika msimu wake wa kwanza kabisa wa kushiriki michuano ya CAF, kitu ambacho hapo awali kiliwahi kufanywa na Namungo FC.

CA 05

Hata hivyo, pamoja na furaha hii, ni muhimu tukumbuke mafanikio haya siyo mwisho wa safari, bali ndiyo mwanzo wa jukumu kubwa zaidi.

Timu zetu zisiridhike kwa kufika tu hatua hii, bali zitazame mbali zaidi, katika ndoto ya kuona klabu za Tanzania zikifika robo fainali, nusu fainali au hata kutwaa ubingwa wa Afrika.

Wakati huu, wadau wote wa soka nchini, TFF, serikali, wadhamini, mashabiki na viongozi wa klabu wanapaswa kuungana kuhakikisha klabu hizi zinapata mazingira bora ya kuendelea kufanya vizuri. Ufadhili wa kutosha, usimamizi makini wa rasilimali na motisha kwa wachezaji ni mambo yanayopaswa kupewa kipaumbele. Timu zinapokuwa kwenye michuano ya kimataifa, zinabeba bendera ya taifa. Hivyo, kila mafanikio yao ni heshima ya Tanzania nzima.

CA 06

Viongozi wa klabu wanapaswa pia kujifunza kutokana na changamoto zilizopita. Msimu uliopita, baadhi ya timu ziliingia makundi lakini zikashindwa kushindana ipasavyo kutokana na upungufu wa maandalizi, uchovu wa msimu, au kukosa uzoefu wa kushindana kimataifa.

Safari hii, tunatarajia kuona timu zetu zikicheza kwa ujasiri, nidhamu na ubunifu. Zisibweteke kwa shangwe za kufuzu, bali zijiandae kwa vita kubwa zaidi iliyoko mbele yao.

Kwa kizazi hiki cha soka la Tanzania, huu ni wakati wa kuamini inawezekana. Miaka michache iliyopita, kufika hatua ya makundi kulihesabika kama ndoto, lakini leo ni jambo la kawaida kwa klabu zetu kubwa.