Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#WC2018: Makocha wa timu za Taifa wanaolipwa pesa ndefu.

Muktasari:

  • Mastaa kama Paul Pogba, Neymar, Messi na wengine kibao watakuwa wakionyeshana ubabe kila mmoja akisaka ushindi kwa timu yake, lakini huku nje makocha ndio mpango mzima katika kuwapa mbinu.

MOSCOW, RUSSIA

HUKO Russia ni lazima kitanuka mwanangu kwani, ukiachilia mbali vita ya mastaa kuonyeshana kazi ndani na nje ya uwanja, pia kuna makocha ambao wanatamba kinoma.

Mastaa kama Paul Pogba, Neymar, Messi na wengine kibao watakuwa wakionyeshana ubabe kila mmoja akisaka ushindi kwa timu yake, lakini huku nje makocha ndio mpango mzima katika kuwapa mbinu.

Kutokana na kazi kubwa ya makocha, ndio sababu baadhi wamekuwa wakilipwa pesa ndefu ili kuwafanya kuwa watulivu na kutoa mbinu bora za kuipa ubingwa timu yake.

Sasa makala haya yanaangazia makocha 10 ambao wanakwenda Russia huku kwenye akaunti zao kukiwa na mzigo maana. Hawa ndio


Joachim Low, Ujerumani (Euro 3.85 milioni)

Ujerumani huwaelezi kitu kwa Joachim Low kwani, amewapa mafanikio makubwa na kuiweka taifa hilo juu kwenye ulimwengu wa soka. Low ameshinda taji la Dunia na lile la Ulaya na kwa sasa anaongoza orodha ya makocha kule Russia wanaolipwa mshahara mkubwa. Anapokea mshahara wa Euro 3.8 milioni kwa mwaka.

 

Tite, Brazil (Euro 3.5 milioni)

Anaitwa Adenor Leonardo Bacchi wenyewe wanapenda kumuita Tite, huyu ni moja ya makocha wanaotajwa kuirudisha Brazil katika utawala wake wa soka la kimataifa. Kwa sasa anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya makocha wanaovuta pesa ndefu akitia kibindoni Euro 3.5 milioni kwa mwaka.

 

Didier Deschamps, Ufaransa (Euro 3.5 milioni)

Baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya mataifa ya Ulaya dhidi ya Ureno kwa bao 1-0 mwaka 2016 michuano iliyofanyika kwenye ardhi yao, hii itakuwa nafasi yake kuhakikisha kizazi hiki cha dhahabu cha Ufaransa kinatwaa taji la dunia. Deschamps analipwa Euro 3.5 milioni kwa mwaka.

 

Julen Lopetegui, Hispania (Euro 3 milioni)

Lopetegui alipata mafanikio makubwa na timu za vijana za taifa hilo kabla ya kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya wakubwa, akichukua nafasi ya Vicente del Bosque aliyejiuzulu mwaka 2016. Julen analipwa Euro 3 milioni kwa mwaka.

 

Stanislav Cherchesov, Russia (Euro 2.6 milioni)

Huyu jamaa anatarajiwa kuliongoza taifa mwenyeji wa mashindano hayo na kuhakikisha anawapa furaha mashabiki wake kwa kufika mbali kwenye fainali hizo. Cherchesov anapokea kitita cha Euro 2.6 milioni kwa mwaka.

 

Fernando Santos, Ureno (Euro 2.25 milioni)

Baada ya kuingoza Ureno kutwaa taji la mataifa ya Ulaya mwaka 2016, Santos alipanda thamani na kuongezewa mkataba wenye donge nono la Euro 2.25 milioni kwa mwaka.

 

Carlos Queiroz, Iran (Euro 2 milioni)

Unamkumbuka huyu? Alikuwa msaidizi wa karibu wa Sir Alex Ferguson pale Manchester United, lakini kwa sasa anasimama na miguu yake mwenyewe. Ameiongoza kwa mafanikio makubwa timu ya taifa ya Iran na kuiwezesha kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu. Queiroz anaweka kibindoni Euro 2 milioni kwa mwaka.

 

Gareth Southgate, England (Euro 2 milioni)

Southgate ana kibarua kizito cha kupeleka furaha kwa Waingereza baada ya kukosa mataji ya kimataifa kwa muda mrefu. Kocha huyu analipwa kitita cha Euro 2 milioni kwa mwaka.

 

Jorge Sampaoli, Argentina (Euro 1.8 milioni)

Kazi kubwa aliyonayo kocha huyu ni kuhakikisha Argentina ya Lionel Messi inatwaa Kombe la Dunia mwaka huu, kinyume na hapo sidhani kama atakuwa na msamaha kwa waajiri wake. Anavuna Euro 1.8 milionI kwa mwaka.

 

Oscar Tabarez, Uruguay (Euro 1.7 milioni)

Orodha hii inakamilishwa na moja ya makocha wakongwe kwenye fainali za mwaka huu, babu Oscar Tabarez. Kocha huyu anachukua mkwanja wa Euro 1.7 milioni kwa mwaka.


Kuhabarika zaidi, pakua HAPA jarida letu la #KombelaDunia2018 linaloletwa kwako na magazeti uyapendayo ya Mwananchi  na Mwanaspoti.