Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

XABI ALONSO; Tajiri aliyezifuata pesa za Todd Boehly Chelsea

ATM Pict

Muktasari:

  • Alonso ambaye alifanya vizuri sana akiwa Bayer Leverkusen kabla ya kushindwa kuisaidia Real Madrid, inadaiwa atakuwa anapata mshahara mnono zaidi ya ule aliokuwa akiupata jijini Madrid.

LONDON, ENGLAND: Chini ya umiliki wa Todd Boehly na Clearlake Capital, Chelsea imeendelea kubadili sura yake kwa kuwekeza katika mradi wa muda mrefu wa kurudisha klabu hiyo kwenye kilele cha soka la Ulaya. Katika mabadiliko hayo, Xabi Alonso amepewa jukumu la kuwa mhimili wa ujenzi mpya wa kikosi hicho, akitarajiwa kuleta nidhamu, mbinu za kisasa na uthabiti wa ushindani.

Alonso si jina jipya katika soka la ushindani wa juu. Akiwa mchezaji na baadaye kocha, amepita katika klabu kubwa na zenye historia nzito kama Real Sociedad, Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich, kabla ya kujijenga zaidi kama kocha kupitia Bayer Leverkusen ambako alionekana kubadilisha kabisa taswira ya timu hiyo kwa mafanikio makubwa ya kihistoria.

Kama mchezaji, Alonso alikuwa kiungo wa kiwango cha dunia, akishinda mataji makubwa ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Liverpool mwaka 2005 katika fainali ya Istanbul, La Liga akiwa na Real Madrid, pamoja na Bundesliga akiwa Bayern Munich. Alijijengea sifa ya pasi sahihi, uongozi uwanjani na uwezo wa kuamua mechi kubwa.

Safari yake ya ukocha ilianza taratibu lakini kwa uthabiti na kilele chake kilijitokeza Bayer Leverkusen na aliigeuza timu hiyo kutoka kuwa ya kawaida hadi kuwa tishio kubwa Bundesliga na mashindano ya Ulaya, hatua iliyomfanya kuvutia klabu kubwa zaidi kama Chelsea.

Sasa akiwa Stamford Bridge, Alonso anaingia si tu kama kocha mpya, bali kama mtu mwenye historia ya mafanikio ya kiwango cha juu kama mchezaji na kocha, jambo linaloongeza matarajio makubwa kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo chini ya Boehly.

AT 05

ANAPIGAJE PESA

Safari ya kifedha ya Xabi Alonso imejengwa kwa mafanikio yake ya muda mrefu katika soka la kiwango cha juu. Kama mchezaji, alipata mishahara mikubwa katika klabu alizopita na akiwa Real Madrid na Bayern Munich alikuwa akipata hadi takribani Euro 150,000 kwa wiki katika kilele cha maisha yake ya uchezaji.

Baada ya kustaafu, alihamia kwenye ukocha na mapato yake yameendelea kuongezeka kwa kasi. Akiwa Bayer Leverkusen na katika nafasi zake za juu za ukocha, mshahara wake umekadiriwa kufikia Euro 9 milioni hadi 12 kwa mwaka, huku Chelsea ikitarajiwa kumpa mkataba wenye hadhi zaidi kutokana na ukubwa wa majukumu yake.

Zaidi ya mshahara, Alonso hupata bonasi za mafanikio zinazoweza kufikia mamilioni kulingana na matokeo ya timu. Hii inamfanya kuwa miongoni mwa makocha wanaolipwa vizuri zaidi Ulaya.

Pia ananufaika na mikataba ya udhamini na kampuni kubwa kama Adidas, Audi, Nivea Men na EA Sports na hupata mapato ya ziada ya mamilioni ya Euro kila mwaka. Kwa jumla, utajiri wake unakadiriwa kuvuka Dola 50 milioni hadi 55.

AT 03

NYUMBA

Alonso anamiliki nyumba ya kifahari Hispania katika eneo la San Sebastián, yenye thamani ya takribani Dola 3 milioni. Nyumba hiyo inaonyesha maisha ya utulivu na familia, ikiwa na gym binafsi, bwawa la kuogelea na bustani kubwa.

Zaidi ya hapo, amejikita kwenye uwekezaji wa nyumba za kupangisha Ulaya na hupata kipato cha kudumu kupitia kodi, hatua inayomjengea utajiri wa muda mrefu usiotegemea kazi ya ukocha pekee.

AT 02

NDINGA

Katika maisha yake ya kifahari, Alonso amehusishwa na magari ya hali ya juu yenye hadhi ya kiweledi badala ya anasa za kujionyesha. Miongoni mwa magari hayo ni Audi Q8, Porsche Cayenne, Mercedes-Benz S-Class na Range Rover Sport, yote yakionyesha mtindo wa maisha ya utulivu na nidhamu.

Audi Q8 – Euro 100,000

Porsche Cayenne – Euro 120,000

Mercedes-Benz S-Class – Euro 130,000

Range Rover Sport – Euro 110,000

AT 04

MSAADA KWA JAMII

Kupitia Aladina Foundation ya Hispania, Alonso amekuwa akijihusisha na miradi ya kusaidia watoto wagonjwa, hasa wanaopambana na saratani, pamoja na familia zisizojiweza. Pia alishiriki katika kampeni za misaada wakati wa janga la COVID-19, akitoa michango ya kifedha na vifaa vya afya.

Hii imeimarisha taswira yake kama mtu anayeelewa mafanikio ya kweli hayaishii uwanjani au kwenye benki, bali pia kwenye maisha ya watu wengine.

AT 01

FAMILIA NA MAISHA BINAFSI

Alonso ameoana na Nagore Aranburu na wana watoto watatu, Jontx, Ane na Emm. Licha ya maisha ya soka yenye presha kubwa, amekuwa akihusishwa na maisha ya utulivu, akiepuka starehe za kelele na maisha ya anasa za kupindukia.

Muda wake mwingi huutumia akiwa na familia yake, akijikita zaidi kwenye mazoezi, kazi na maisha ya kawaida ya nyumbani. Hali hii imefanya aonekane kama mmoja wa makocha wachache wenye usawa kati ya mafanikio, utajiri na maisha ya familia.