Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa kila klabu EPL

MATAJIRI Pict

Muktasari:

  • Winga huyo amekubali mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya jumla ya Pauni 78 milioni, sawa na Pauni 300,000 kwa wiki. Hii inazidi mshahara wa Kai Havertz anayelipwa Pauni 280,000 kwa wiki, ambaye awali ndiye aliyekuwa mchezaji mwenye mshahara mkubwa kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Mhispaniola, Mikel Arteta na yenye maskani yake Emirates.

LONDON, ENGLAND: MKATABA mpya wa Bukayo Saka kwenye kikosi cha Arsenal unamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika klabu hiyo.

Winga huyo amekubali mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya jumla ya Pauni 78 milioni, sawa na Pauni 300,000 kwa wiki. Hii inazidi mshahara wa Kai Havertz anayelipwa Pauni 280,000 kwa wiki, ambaye awali ndiye aliyekuwa mchezaji mwenye mshahara mkubwa kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Mhispaniola, Mikel Arteta na yenye maskani yake Emirates.

Lakini, Saka na Arsenal wako wapi ukilinganisha na nyota wanaolipwa zaidi katika klabu nyingine za Ligi Kuu England?

Bado Saka yuko mbali sana na mshahara wa Pauni 525,000 kwa wiki anaolipwa Erling Haaland. Mshahara huo mkubwa unamfanya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Norway kuwa miongoni mwa wanaolipwa zaidi duniani, huku akiwa namba moja Manchester City na Ligi Kuu England.

MATA 01

Mohamed Salah ndiye anayelipwa zaidi katika klabu ya Liverpool akiwa anapokea Pauni 400,000 kwa wiki, huku Bruno Fernandes akiwa kinara wa mishahara katika kikosi cha Manchester United, akilipwa Pauni 350,000 kwa wiki.

Saka anafuata katika orodha hiyo, akimtangulia Reece James wa Chelsea (Pauni 250,000), Jack Grealish aliyeko kwa mkopo Everton (Pauni 225,000) na Jadon Sancho aliyeko kwa mkopo Aston Villa analipwa Pauni 200,000 kwa wiki.

Tottenham Hotspur inashika nafasi ya nane huku Cristian Romero na Xavi Simons wakilipwa Pauni 190,000 kwa wiki kila mmoja. Wanafuatiwa na Bruno Guimaraes anayepokea Pauni 160,000 kwa wiki katika klabu ya Newcastle United, pamoja na Jarrod Bowen anayelipwa Pauni 150,000 katika kikosi cha West Ham United. Aliyekuwa kipa wa Arsenal, Bernd Leno, anapokea Pauni 130,000 kwa wiki, akiidakia Fulham.

Daichi Kamada alikuwa analipwa zaidi katika kikosi cha Crystal Palace, Pauni 105,000 kwa wiki, lakini alizidiwa mara mbili dirisha la usajili kwanza na Brennan Johnson (Pauni 110,000 kwa wiki) na kisha na usajili wa rekodi, Jorgen Strand Larsen, anayelipwa mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki.

MATA 02

Morgan Gibbs-White na Granit Xhaka wanalipwa Pauni 110,000 kwa wiki katika kikosi cha Nottingham Forest na Sunderland mtawalia, huku Joao Gomes wa Wolverhampton Wanderers akilipwa Pauni 105,000 kwa wiki.

Dominic Calvert-Lewin anahakikisha Leeds United inafanya vizuri huku akiwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa katika kikosi hicho, Pauni 100,000 kwa wiki, wakati Pascal Gross anaripotiwa kulipwa karibu Pauni 90,000 tangu aliporejea Brighton, ikiwa ni Pauni 5,000 zaidi ya anayolipwa Evanilson huko kwenye kikosi Bournemouth.

Na wanaokamilisha orodha ya wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi kwa kila timu ya Ligi Kuu England ni Kyle Walker wa Burnley, pamoja na wachezaji wawili wa Brentford, Jordan Henderson na Mikkel Damsgaard. Wachezaji hao watatu kila mmoja analipwa Pauni 75,000 kwa wiki.