Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usajili Bara, unajua yupi kapatia, yupi kazingua?

USAJILI Pict

DIRISHA la usajili Ligi Kuu Bara na mashindano mengine ya ndani lilifungwa Januari 30, 2026, baada ya kudumu kwa takriban mwezi mmoja tangu lilipofunguliwa Januari 1, 2026 kwa ajili ya klabu kuvuta silaha mpya.

Baada ya dirisha hilo kufungwa, Mwanaspoti linakuletea uchambuzi wa timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kwa kuangalia aina ya wachezaji ziliowasajili ikiwa zimezingatia upungufu wa vikosi tangu msimu wa 2025-2026 uanze.

USAJ 01

AZAM FC

Kikosi hiki cha matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC, kimefanya maboresho kadhaa kwa ajili ya kuongeza ushindani wa nafasi, kutokana na mashindano mbalimbali inayoshiriki timu hiyo ikiwemo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.

Miongoni mwa nyota wapya walioanza kuonyesha ushindani ni mshambuliaji, Jean-Jacques Ngita, aliyetokea Aris Limassol FC ya Cyprus, akishindana na nyota mwenzake pia raia wa DR Congo, Jephte Kitambala, aliyejiunga na kikosi hicho msimu huu.

USAJ 04

Ngita ameanza maisha yake vizuri Azam, baada ya kufunga bao moja la Ligi Kuu katika ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya TRA United, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam, Januari 29, 2026.

Ongezeko la Ngita ni kukifanya kikosi hicho cha Kocha, Florent Ibenge kuongeza ufanisi mkubwa katika eneo la umaliziaji, huku Ilese Kolonga Caleb, Aimar Hafidh Abubakar ‘Haaland’ na Mzee Hassan Mzee ‘Aziz KI’, wakiendelea kuonyesha kiwango bora.


YANGA

Miongoni mwa nyota wapya wa Yanga ambao hadi sasa wameanza kuonyesha matumaini makubwa, ni mshambuliaji Laurindo Dilson Maria Aurelio ‘Depu’ raia wa Angola, aliyejiunga na kikosi hicho dirisha hili dogo akitokea Radomiak Radom FC ya Poland.

Mshambuliaji huyo amechukua nafasi ya Andy Boyeli aliyerejea Sekhukhune United FC ya Afrika Kusini, baada ya kuichezea Yanga kwa nusu msimu kwa mkopo na Depu ameziba vyema pengo hilo kwa kuhusika katika mabao manne ya Ligi Kuu Bara.

USAJ 06

Depu amefunga mabao matatu na kuasisti moja ya ligi, akiingia kikosi cha kwanza moja kwa moja, sambamba na Mohamed Damaro anayecheza eneo la katikati ya uwanja na viungo washambuliaji, Emmanuel Mwanengo na Mganda Allan Okello ambaye kiwango chake kimewakosha mashabiki wa soka.

Kipa, Hussein Masalanga na winga Mgambia Buba Jammeh, bado hawajaanza kukichezea kikosi hicho hadi sasa, ingawa ni moja ya sajili zinazosubiriwa kuona kama zitaongeza ushindani wa nafasi, licha ya uwepo wa nyota bora wanaocheza pamoja.

USAJ 08

SIMBA

Timu hii inayonolewa na Kocha, Steve Barker, msimu huu sio mzuri hadi sasa kutokana na mabadiliko makubwa ya wachezaji iliyofanya hasa dirisha hili la Januari 2026, ikiingiza nyota wapya takriban wanane kuongeza nguvu.

Licha ya urejeo wa kiungo mshambuliaji, Clatous Chama aliyetokea Singida Black Stars, ila winga, Libasse Gueye aliyetoka Teungueth FC ya kwao Senegal, ndiye anayegonga nyoyo za mashabiki wa kikosi hicho kutokana na kiwango anachokionyesha.

Gueye tayari amefunga bao moja la Ligi Kuu Bara hadi sasa katika ushindi wa kikosi hicho wa mabao 2-0, dhidi ya maafande wa Mashujaa FC, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni jijini Dar es Salaam, Januari 29, 2026.

Kuondoka kwa aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu wa 2024-2025, Jean Charles Ahoua aliyejiunga na CR Belouizdad ya Algeria, kukawafanya mabosi wa kikosi hicho kufanya maboresho makubwa ya kuingiza nyota wengine wa kuziba nafasi hiyo.

USAJ 09

Wengine ni Alain Anicet Oura, Nickson Kibabage ambaye anapata nafasi ya kucheza na kipa wao namba moja kwa sasa, Mahamadou Tanja Kassali aliyechukua nafasi ya Moussa Camara aliye majeruhi ambao tayari nyota wote hao wameanza kuonyesha matumaini ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha, Steve Barker.

Beki, Ismael Olivier Toure na mshambuliaji, Baraka Mwangosi wanasubiriwa pia kuongeza kitu eneo hilo sambamba na Inno Jospin Loemba, aliyechukua nafasi ya aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Mganda Steven Mukwala aliyetua Al-Nasr SC ya Libya.


SINGIDA BLACK STARS

Kikosi hiki kinachoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yake msimu huu, imefanya maboresho makubwa dirisha la Januari 2026, kutokana na wingi wa wachezaji kuondoka ili wakapate changamoto mpya.

USAJ 07

Mshambuliaji, Joseph Guede aliyerejea tena baada ya kwenda kuitumikia Al-Wehdat SC ya Jordan, ndiye anayetegemewa eneo la ushambuliaji akishirikiana na Mkenya Elvis Rupia, baada ya Mzambia Andrew Phiri kujiunga na Hard Rock FC ya Zimbabwe.

USAJ 02

Nyota wengine ni Abdallah Kheri ‘Sebo’, Abdallah Said Ali ‘Lanso’, Miraji Abdallah ‘Zambo’ na Abdulmalik Zakaria, ambao wameingia moja kwa moja katika kikosi hicho cha kwanza eneo la kujilinda, sawa na Ahmed Bakari Pipino, Mboni Stephen Kibamba, Linda Mtange, Mossi Nduwumwe na winga, Offen Chikola aliyetokea Yanga, ambaye bado hajaanza kuonyesha makali yake.    


PAMBA JIJI

Licha ya kuondoka kwa kipa, Arjif Ali Amour, beki wa kati, Abdallah Kheri ‘Sebo’, kiungo, Saleh Masoud Abdallah ‘Tumbo’ na mshambuliaji, Abdallah Idd ‘Pina’, ila kikosi hiki hakijafanya mabadiliko pia kutokana na wingi wa wachezaji waliopo.


COASTAL UNION

Kikosi hiki cha ‘Wagosi wa Kaya’, kimefanya usajili wa nyota wapya wanane, ingawa miongoni mwa wanaotazamwa zaidi ni aliyekuwa mshambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo, Al-Hilal Omdurman ya Sudan na JS Saoura ya Algeria, Thomas Ulimwengu.

Mshambuliaji huyo amejiunga na timu hiyo akiwa huru, ingawa usajili wake unalenga kuongeza uzoefu katika eneo hilo la ushambuliaji, akiungana na aliyekuwa winga wa Simba, Shiza Kichuya, aliyeachana na kikosi cha maafande wa JKT Tanzania.

Wachezaji wote tayari wamecheza mechi moja ya Ligi Kuu na kuonyesha matumaini ya kikosi hicho, ambapo tayari Kichuya ameifungia bao moja, huku akiwa ni miongoni mwa nyota wanaopewa nafasi zaidi ya kucheza na Kocha Mkuu, Mohamed Muya.

USAJ 05

NAMUNGO FC

Baada ya kuondoka kwa kipa, Mrundi Jonathan Nahimana, kikosi hiki cha ‘Wauaji wa Kusini’, kimeziba pengo la nyota huyo kwa kumsajili, Ahmed Feruz aliyewahi kucheza Simba, kufuatia kuachana na Stand United inayoshiriki Ligi ya Championship.

Timu hii haijafanya maboresho makubwa kutokana na asilimia kubwa ya nyota wengi kubakia kikosini, ikiongeza mabeki, Ali Hassan Chamulungu na Julius Machela kutoka Azam kwa mkopo na kiungo mshambuliaji, Julius David aliyetokea Alliance FC.  


TRA UNITED

Miongoni mwa maeneo makubwa ambayo kikosi hiki cha TRA imekifanya ni eneo la kiungo ambalo ameongezwa aliyekuwa nyota wa Simba, Mzamiru Yassin na Muhsin Malima aliyetoka Azam, kwa ajili ya kutengeneza balansi nzuri ya kuzuia na ushambuliaji.

USAJ 10

Denis Nkane aliyetoka Yanga, ni mchezaji mwingine atakayeleta manufaa makubwa kwa kikosi hicho kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani, ambapo tayari ameifungia bao moja, akiungana na aliyekuwa beki wa kushoto wa Simba, Valentin Nouma, aliyerejea tena, ambaye bado hajaanza kuingia kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja msimu huu.


DODOMA JIJI

Urejeo wa mshambuliaji, Waziri Junior aliyetoka Al-Minaa SC ya Iraq na Elias Maguri, ni miongoni mwa sajili bora za timu hii eneo la ushambuliaji, akitazamiwa kuongeza makali eneo hilo kwa kushirikiana na Elias Maguri kutengeneza balansi.

Beki wa zamani wa Yanga, Simba, Gadiel Michael kutoka Singida Black Stars, amejiunga pia na kikosi hicho na tayari ameanza kuingia kikosi cha kwanza moja kwa moja, baada ya kupishana na Miraji Abdallah ‘Zambo’, aliyetua Singida Black Stars.

USAJ 11

MASHUJAA FC

Kikosi hiki cha maafande kimeendelea kuamini nyota walio kikosini, ambapo licha ya kuondoka kwa beki wa kati, Abdulmalik Zakaria aliyejiunga na Singida Black Stars, ila bado timu hiyo ina nyota wengi wanaoweza kucheza eneo hilo kwa ufasaha.

Uwepo wa beki, Mohamed Mussa aliyejiunga na kikosi hicho mwanzoni mwa msimu huu akitokea Kagera Sugar na Samson Madeleke aliyerejea tena akitokea Pamba Jiji, wameendelea kutengeneza balansi nzuri kwa timu hiyo chini ya Kocha, Salum Mayanga.

USAJ 12

JKT TANZANIA

Baada ya kuondoka kwa Shiza Kichuya na Hassan Dilunga aliyejiunga na Mbeya City, mabosi wa timu hiyo wakafanya maboresho machache kwa kuwaingiza Said Zanda aliyetokea Bigman FC na Tepsi Evance wa Azam ili kuziba nafasi za nyota hao kikosini.

JKT Tanzania haijafanya maboresho makubwa katika dirisha dogo la Januari 2026, kutokana na wachezaji wengi wa timu hiyo kuendelea kubaki, hali inayompa nafasi Kocha, Ahmad Ally, kutovuruga mfumo wake wa kiuchezaji wa kikosi hicho hadi sasa.

USAJ 13

KMC FC

Mojawapo ya changamoto kubwa ya KMC tangu msimu huu umeanza ni katika eneo la ushambuliaji na uzuiaji, ambapo timu hiyo inayoburuza mkiani katika mechi 12 ilizocheza hadi sasa imefunga mabao matatu, huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 19.

Katika kuboresha maeneo hayo hususani eneo la ushambuliaji, timu hiyo imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa maafande wa Transit Camp, Adam Uledi, ambaye msimu huu pekee tayari kwenye Ligi ya Championship amekifungia kikosi hicho mabao 11.

Uledi ni mshambuliaji mzoefu akiwahi kuzichezea Stand United, Namungo FC, Ruvu Shooting, African Sports, Coastal Union, TMA, KenGold na timu ya vijana ya Yanga, akiungana na Eliuter Mpepo aliyeachana na kikosi pia cha Singida Black Stars.

Nyota hao wameanza kuingia kikosi cha kwanza cha Kocha, Abdallah Mohamed ‘Baresi’, wakitazamiwa kuleta mageuzi makubwa katika safu ya ushambuliaji.

USAJ 14

MTIBWA SUGAR

Timu hii inayonolewa na Kocha Mkuu, Mkenya Yusuf Chippo akishirikiana na Awadh Juma ‘Maniche’, imeendelea kuamini vijana wadogo na wenye vipaji kikosini humo, wakiongozwa na Fredrick Magata na Haroun Evody, ambao wanaendelea kufanya vizuri.

Mtibwa ilikuwa ni timu ya kwanza msimu wa 2024-2025, kupanda Ligi Kuu Bara, huku ikiwa na mechi mbili mkononi kutokana kuonyesha soka safi tangu mwanzoni, ikirejea tena katika hekaheka za michuano hiyo, baada ya kushuka msimu wa 2023-2024.

USAJ 03

MBEYA CITY

Kikosi hiki kinachonolewa na Kocha Mecky Maxime, kimeongeza pia idadi kubwa ya wachezaji katika maeneo mbalimbali, huku katika eneo la ushambuliaji ikimuongeza aliyekuwa nyota wa Yanga, Yacouba Songne, aliyecheza TRA United msimu uliopita.

Uzoefu wa Yacouba, ni faida kwa timu hiyo akiungana na nyota wengine wapya ambao ni Kelvin Kijili, Abdallah Kulandana, Said Naushad, Hijjah Shamte, Kelvin Kijili, Abalkassim Suleiman, Omary Abdallah Omary, Mohamed Kassim na Hassan Dilunga.

Wachezaji wote wameanza kuingia taratibu kikosi cha kwanza, huku Kocha, Maxime akiendelea kutengeneza balansi nzuri ya kiuchezaji kati yao.


TANZANIA PRISONS

Miongoni mwa mapendekezo makubwa kwa Kocha wa Tanzania Prisons, Mkenya Zedekiah ‘Zico’ Otieno, ilikuwa kuongezewa nguvu katika eneo la ushambuliaji, ambapo mabosi wa timu hiyo wamefanya kweli kwa kuongeza nyota wawili wenye uzoefu mkubwa.

Nyota hao ni Samson Mbangula aliyerejea tena baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha na mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2021-2022, George Mpole, ambaye hakuwa na timu yoyote tangu alipoachana na kikosi cha Pamba Jiji.

Mpole ameingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza na ameifungia timu hiyo bao moja la Ligi Kuu, akitegemewa kuongeza ushindani eneo hilo.

USAJ 15

FOUNTAIN GATE

Baada ya kuondoka Joshua Ibrahim aliyerejea tena Tusker ya Kenya, mabosi wa timu hiyo wakaenda Mbeya Kwanza inayoshiriki Ligi ya Championship na kumsajili mshambuliaji, Boniface Mwanjonde, ambaye tangu msimu umeanza ameonyesha kiwango bora.

Katika mechi 14 za Mbeya Kwanza msimu huu, alihusika na mabao 13, baada ya kufunga tisa na kuasisti manne, akiungana na viungo washambuliaji, Saleh Masoud Abdallah ‘Tumbo’ aliyetoka Pamba Jiji na Tariq Mohamed Mkonga kutoka JKU ya Zanzibar.

Bado wachezaji hao hawajaanza kukitumikia kikosi hicho, ingawa wamebeba matumaini makubwa ya kutokana na viwango ambavyo wanao.