Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unaijua ligi ya makocha wa Simba na Yanga?

MAKOCHA Pict


ACHANA na fujo za usajili zinazoendelea kwa kila timu kuboresha mapungufu yaliyoonekana kuanzia msimu huu wa 2025/26 ulipoanza.


Timu zote 16 zinapambana kuwania saini za mastaa kutoka klabu mataifa mbalimbali lakibi ukiondoa hilo kuna vita ya chini chini iliyopo baina ya mahasimu wa jadi Simba na Yanga.


Timu hizo kongwe ukiondoa ushindani wa uwanjani zikipokezana kutwaa mataji baada ya Simba kuanza ikitwaa mara nne mfululizo Yanga imelipa na sasa ni msimu wa nani kuamua ubingwa kati yao.

Wakati vita hiyo ikipamba moto kwa timu zote kucheza mechi sita huku kinara ikiwa ni Yanga baada ya kukusana pointi 19 ikiiacha Simba kwa pointi tatu baaya ya kukusanya pointi 16.

Mwanaspoti linakuletea rekodi ya makocha waliopita katika klabu hizo ndani ya miezi saba kuanzia Julai hadi Januari mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kusuka benchi bora la ufundi linaloweza kuzipa mataji klabu hizo kongwe.

MAKO 02

FADLU DAVIDS

Fadlu alijiunga na Simba akichukua nafasi ya Mualgeria, Abdelhak Benchikha aliyeondoka Aprili 28, 2024, akitokea, Raja Casablanca ya Morocco aliyojiunga nayo tena baada ya kuachana na kikosi cha Msimbazi alichokiongoza kwa mwaka mmoja tu.

Kwa msimu wa 2024-2025, Fadlu aliiongoza Simba kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara na pointi 78, baada ya kocha huyo kushinda mechi 25, sare tatu na kupoteza miwili tu, nyuma ya mabingwa Yanga, iliyomaliza kinara na pointi zake 82.

Licha ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ila Fadlu aliandika rekodi ya kipekee ya kuipeleka Simba hadi fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 32, tangu ilipofika fainali ya michuano ya CAF mwaka 1993.

Katika fainali hiyo msimu wa 2024-2025, Simba ilikosa ubingwa mbele ya RS Berkane ya Morocco, baada ya kuchapwa jumla ya mabao 3-1, ugenini 2-0, Mei 17, 2025, huku marudiano yaliyofanyika Zanzibar ikatoka sare ya 1-1, Mei 25, 2025.

Msimu wa 2025-2026, aliiongoza mechi mbili za kimashindano, akianza na ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na kuchapwa bao 1-0, Septemba 16, 2025, kisha akaifunga Gaborone United 1-0, hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Septemba 20, 2025.

Septemba  22, 2025, Klabu ya Simba ilitangaza kufikia makubaliano ya kuachana na Fadlu Davids raia wa Afrika ya Kusini, ikiwa ni siku 444, tangu atambulishwe kukitumikia kikosi hicho rasmi, Julai 5, 2024.

MAKO 06

HEMED MOROCCO

Baada ya kumalizana na Fadlu uongozi wa Simba ukamteua aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco', kwa ajili ya kukiongoza kikosi hicho kwa muda 'Caretaker', huku mchakato wa kumtafuta mrithi wa Fadlu Davids aliyeondoka ukiendelea.

Morocco aliiongoza timu hiyo mechi moja tu ya awali ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana na kuisha kwa sare ya bao 1-1, katika pambano lililopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 28, 2025.

Licha ya sare hiyo, ila Simba ilifuzu kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1, baada ya pambano la kwanza Botswana kushinda bao 1-0, hivyo, kutinga hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo ilikutana na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini.

Katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara za timu hizo, ziliongozwa na Kocha Msaidizi, Selemani Matola ambazo zote alishinda, akianza na ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya Fountain Gate, Septemba 25, 2025, kisha pia 3-0 na Namungo FC, Oktoba 1, 2025. 

MAKO 05

DIMITAR PANTEV

Oktoba 3, 2025, uongozi wa Simba ukamtangaza rasmi aliyekuwa Kocha wa Gaborone United ya Botswana, Dimitar Pantev, kwa lengo la kukiongoza kikosi hicho, akichukua nafasi ya Fadlu Davids.

Pantev aliyeteuliwa Oktoba 3, 2025, amedumu Simba kwa siku 60, huku akiwa amekiongoza kikosi hicho jumla ya mechi tano za msimu huu wa 2025-2026, nne ni za Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na moja ya Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo alianza kuiongoza Simba hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kushinda ugenini kwa mabao 3-0, dhidi ya Nsingizini Hotspurs kutoka Eswatini, Oktoba 19, 2025, huku marudiano Dar es Salaam akatoa suluhu (0-0), Oktoba 26, 2025.

Ushindi huo wa jumla ya mabao 3-0, ukaifanya Simba kufuzu rasmi hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa 2025-2026 na Pantev alianza vibaya kwa kuchapwa mechi mbili mfululizo, zilizosababisha kusitishiwa mkataba wake.

Simba iliyopangwa kundi D la michuano hiyo, ilianza kwa kuchapwa bao 1-0, dhidi ya Petro Atletico ya Angola, Novemba 23, 2025, kisha ikachapwa tena 2-1 na Stade Malien ya Mali, Novemba 30, 2025 na hapo ndipo ikawa mechi ya mwisho kwa Pantev.

Katika Ligi Kuu Bara, Pantev aliiongoza Simba kwenye mechi moja tu na kushinda mabao 2-1, dhidi ya JKT Tanzania, Novemba 8, 2025 na  kijumla alishinda miwili, sare moja na kuchapwa pia miwili, huku akifunga mabao sita na kuruhusu manne.

Desemba 2, 2025, Simba ilitangaza kusitisha mkataba na Kocha Pantev, baada ya kikosi hicho kupoteza mabao 2-1, dhidi ya Stade Malien ya Mali, katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi iliyopigwa, Novemba 30, 2025.

MAKO 03

STEVEN BARKER

Desemba 19, 2025, Simba ilimtangaza Kocha, Steven Robert Barker ili kurithi mikoba ya Pantev, akitoka Stellenbosch ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo mwaka 2017, baada ya kuachana na kikosi cha Mpumalanga Black Aces akitokea AmaZulu FC.

Kocha huyo aliyezaliwa Desemba 23, 1967, aliiongoza Chuo Kikuu cha Pretoria kuipandisha daraja Mei, 2012, japo licha ya mafanikio hayo makubwa ila aliondoka Novemba 2014, kisha kujiunga na AmaZulu, aliyoiongoza kuanzia mwaka 2014 hadi 2016.

Barker aliyecheza kiungo akiwa mchezaji, amechukua Carling Knockout Cup 2023 na Stellenbosch, huku akianzia soka la vijana la Ramblers, Potchefstroom Celtic na SANDF, wakati zile za wakubwa alicheza Wits University na SuperSport United.

Katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (Betway Premiership), Barker aliiongoza Stellenbosch katika mechi 14 na kati ya hizo alishinda tatu, sare tatu na kufungwa nane, ikifunga mabao 10 na kuruhusu 18, akiiacha nafasi ya 14 na pointi 12.

Kwa msimu huu wa 2025-2026, Barker aliyezaliwa Lesotho, ameiongoza Stellenbosch katika mechi 24 za mashindano tofauti, akiwa na kikosi hicho cha Afrika ya Kusini na kati ya hizo alishinda mara nane, akitoka sare sita na kupoteza 10.

Ndani ya kikosi cha Simba kocha huyo alianza na michuano ya Mapinduzi Cup aliiongoza timu hiyo kushinda mechi tatu akianza na Fufuni FC timu ilishinda mabao 2-1, mchezo wa pili dhidi ya Muembe Makubi ikishinda bao 1-0 na mchezo wa tatu ilicheza dhidi ya Azam FC na kukubali kichapo cha bao 1-0 na kuondoleea kwenye michuano hiyo.

Baada ya kurudi Ligi Kuu Bara Simba ikiwa chini ya Barker ameiongoza timu hiyo kwenyechezo mmoja ikiambulia sare dhidi ya Mtibwa Sugar.


WAKATI YANGA

OKTOBA 18, 2025, uongozi wa Yanga uliachana na Kocha, Mfaransa Romain Folz aliyejiunga na kikosi hicho, Julai 23, 2025, akichukua nafasi ya Miloud Hamdi aliyeipa ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2024-2025, kisha kujiunga na Ismaily SC ya Misri.

Kocha huyo mwenye leseni ya UEFA Pro na CONBEL Pro, alitua Yanga kuchukua nafasi ya Miloud Hamdi aliyetimkia Ismaily ya Misri, baada ya kudumu kwa miezi sita na kushinda ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Muungano na Kombe la Shirikisho (FA).

Hamdi mwenye uraia pacha wa Algeria na Ufaransa huku akiwa na leseni A ya UEFA, alitua nchini kujiunga na Singida Black Stars, Desemba 30, 2024, ingawa hakuiongoza hata mechi yoyote hadi Yanga ilipoinasa saini yake rasmi, Februari 4, 2025.

MAKO 01

Kocha huyo, alitambulishwa Yanga baada ya kuondoka kwa Mjerumani, Sead Ramovic aliyejiuzulu mwenyewe, Februari 4, 2025, kwa makubaliano ya pande mbili, tangu atambulishwe kikosini humo Novemba 15, 2024, akitokea TS Galaxy ya Afrika Kusini.

Msimu wa 2025-2026, Folz aliiongoza Yanga katika mechi sita za kimashindano na alishinda nne, akitoka sare mmoja na kupoteza pia mmoja, akianza na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Simba, kwenye Ngao ya Jamii, iliyopigwa Septemba 16, 2025.

Baada ya hapo akafungua pazia la Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali kwa kuifunga Wiliete De Benguela ya Angola mabao 3-0, Septemba 19, 2025, huku mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam akashinda pia 2-0, Septemba 27, 2025.

Katika Ligi Kuu Bara, Folz alianza kwa ushindi baada ya kikosi hicho kuifunga Pamba Jiji mabao 3-0, Septemba 24, 2025, ingawa upepo wa kuendelea kubakia ndani ya timu hiyo ulibadilika kufuatia suluhu (0-0) na Mbeya City, Septemba 30, 2025.

Folz akaiongoza Yanga katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na timu hiyo ikiwa ugenini ilichapwa bao 1-0, dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, Oktoba 18, 2025, na hapo ukawa ndio mwisho wake kikosini.

katika mechi hizo sita za kimashindano, Folz aliiongoza kushinda nne, sare moja na kupoteza moja na alifunga jumla ya mabao tisa na kuruhusu moja tu, huku mzaliwa huyo wa Bordeaux huko Ufaransa, alianza rasmi kazi ya ukocha mwaka 2018.

Mwaka 2018, aliteuliwa kocha mkuu wa klabu ya West Virginia United ya Marekani, huku mwaka 2019, akihudumu kama kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda, kisha baada ya hapo akateuliwa kocha msaidizi wa klabu ya Pyramids kutokea Misri.

MAKO 04

Mwaka 2020, Folz aliteuliwa kocha mkuu wa klabu ya Bechem United ya Ghana, kisha akahamia Ufaransa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Niort na mwaka 2021 alitua Ashanti Gold ya Ghana, kabla ya kwenda Botswana kuifundisha pia Township Rollers.

Mwaka 2022, alihamia Afrika Kusini kwa mara ya kwanza na kuifundisha Marumo Gallants, akiwa pia ndiye kocha mdogo zaidi katika Ligi Kuu ya Afrika ya Kusini, kisha baada ya hapo akaiongoza pia AmaZulu FC kuanzia mwaka 2022 hadi 2023.

Akiwa na Amazulu, Aprili 2023, alipewa jukumu la Mkurugenzi wa Ufundi, huku Agosti 2023, alijiunga na Horoya AC ya Guinea, kisha Julai 2024, alijiunga na Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini kama kocha msaidizi hadi Desemba 10, 2024.

Machi 2025 alijiunga na klabu ya Olympique Akbou inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria akiwa mkurugenzi wa michezo, nafasi ambayo aliitumikia hadi mnamo Julai 2025, kisha baada ya hapo akajiunga rasmi na Yanga akichukua nafasi ya Miloud Hamdi.

Baada ya kuondoka kwa Folz, uongozi wa Yanga ukamtangaza Kocha Msaidizi, Patrick Mabedi, kuongoza kikosi hicho kwa muda, huku mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu atakayeiongoza timu hiyo kumalizia msimu wa 2025-2026, ukiendelea kwa haraka zaidi.

Mabedi aliiongoza Yanga katika mechi moja tu ya ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Silver Strikers kutoka Malawi, Oktoba 25, 2025 na timu hiyo kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya ugenini kuchapwa bao 1-0. 

MAKO 04

Hata hivyo, Oktoba 25, 2025, uongozi wa Yanga ulimtangaza Pedro Goncalves raia wa Ureno kukiongoza kikosi hicho, ikiwa ni muda mfupi tangu timu hiyo ifuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 2025-2026.

Yanga ilimtambulisha Pedro ikiwa ni muda mfupi tu tangu ifuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0, dhidi ya Silver Strikers kutoka Malawi na kuiondosha kwa jumla ya mabao 2-1.

Pedro alijiunga na Yanga akiwa na rekodi nzuri pia ya kuifikisha timu ya Taifa ya Angola katika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), iliyofanyika mwaka 2023 na kushuhudia wenyeji, Ivory Coast ikitwaa ubingwa huo.

Mbali na hilo, ila Pedro aliiongoza Angola katika Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN), iliyofanyika mwaka 2024 katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda na timu hiyo ilitolewa mapema tu hatua ya makundi.

MAKO 07

Pedro alihudumu kama mng'amuzi wa vipaji, katika Klabu ya Sporting CP, kisha kituo cha kulelea vipaji cha timu hiyo kati ya mwaka 2000 hadi 2015, huku kwa mara ya kwanza Afrika aliwafundisha vijana wa Primeiro de Agosto mwaka 2015 hadi 2018.

Kocha huyo aliifundisha klabu hiyo na ile ya vijana chini ya miaka 20 hadi 2019, kisha timu ya Angola ya wakubwa na alifundisha kikosi hicho hadi mwaka 2025 na kuachana nacho rasmi na kujiunga na Yanga akichukua nafasi ya Romain Folz.

Katika kikosi cha Yanga ameanza na taji la Mapinduzi akiiongoza timu hiyo kutwaa bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa katika mechi nne walizocheza na ameifanya Yanga iongoze msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 baada ya mechi sita.