Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulaya kumechangamka, Ronaldo akitikisa Saudia

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Bayern Munich ilipata ushindi wa tabu dakika za jioni ikiwa ugenini dhidi ya Freiburg katika Bundesliga, ikitoka nyuma kwa mabao 0-2 na kushinda 3-2.

MUNICH /RIYADH: KWA mashabiki wa Barcelona, Bayern Munich na PSG ni mwendo wa vicheko tu baada ya timu zao kuwa hatua chache kutwaa ndoo za Ligi Kuu katika mataifa yao huku vigogo wa soka Italia wakiendelea na hesabu za vidole.

Bayern Munich ilipata ushindi wa tabu dakika za jioni ikiwa ugenini dhidi ya Freiburg katika Bundesliga, ikitoka nyuma kwa mabao 0-2 na kushinda 3-2.

Bao la mwisho la ushindi lilifungwa dakika ya tisa ya nyongeza na Lennart Karl, baada ya krosi ya Alphonso Davies.

Freiburg ilikuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya bao la Johan Manzambi katika dakika ya 46 na kuongeza lingine la Lucas Holer dakika ya 71.

Matokeo hayo yaliwafanya mashabiki wa Freiburg  kuamini wanaweka historia dhidi ya miamba hiyo ya soka la Ujerumani, hata hivyo, Bayern hawakukata tamaa. Tom Bischof alianzisha safari ya kuchomoa mabao hayo kwa Bayern dakika ya 81 wakati mechi hiyo ikiwa katika muda wa nyongeza, kwa kusawazisha na kufanya mzani kuwa sawa 2-2 kabla ya Karl kupiga msumari wa tatu na kuwaacha wenyeji wakiwa hawaamini kilichotokea.

Ushindi huo, umeifanya Bayern kufikisha pointi 73, wanaongoza msimamo wa Bundesliga wakiwa juu kwa tofauti ya pointi tisa dhidi ya Dortmund ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 64 huku ikiwa imesalia michezo sita.

Bayern inahitaji ushindi wa mechi tatu na sare moja ili kutwaa Bundesliga kwa mara ya 35.

RONA 01

Hali hiyo ya Bayern ilikuwa tofauti na ile ya Barcelona ambayo ilikabiliana na Atletico Madrid, moja ya mechi zilizokuwa na patashika wikiendi iliyopita. Mashabiki wa La Liga walishuhudia ushindi wa mabao 2-1 kwa Blaugrana (Barca) huku Robert Lewandowski akiwa shujaaa kwa timu hiyo, bao la kwanza likifungwa na Marcus Rashford, bao la Atletico lilifungwa na Giuliano Simeone na vijana hao wa Diego Simeone iliwabidi kumaliza pungufu mchezo huo kufuatia kadi nyekundu ya Nicolas Gonzalez.

Matokeo hayo yameiweka Barcelona kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa La Liga, wakiwa pointi saba mbele ya Real Madrid ambao wikiendi haikuwa nzuri kwa upande wao, wakichapwa huko Mallorca kwa mabao 2-1.

Kwa upande wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1, PSG imeendelea kutawala baada ya kuichapa Toulouse mabao 3-1 huku nyota wake Ousmane Dembele akicheka na nyavu mara mbili na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 63 huku ikiwa mchezo mmoja nyuma ulinganisha na timu nyingine.

RONA 02

Katika Ligi ya Ufaransa kumesaliwa na michezo sita hivyo PSG inayoongoza kwa tofauti ya pointi nne inahitaji ushindi katika mechi nne ili kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya tano mfululizo.

Wakati hali ikiwa hivyo katika ligi hizo kwa upande wa Italia vigogo wote, walikuwa mzigoni jana, Jumatatu kupiga hesabu za vidole.

Kwa upande wa Saudia, Cristiano Ronaldo alisherehekea kurudi kwake baada ya kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kutokana na majeraha kwa kufunga mabao mawili katika kipindi cha pili huku Al Nassr wakiendelea na mfululizo wa ushindi kwa kushinda mabao 5-2 dhidi ya Al Najma, timu iliyoko katika nafasi ya mwisho, katika msimamo wa ligi hiyo.

RONA 03

Mshambuliaji huyo wa Kireno, ambaye amekuwa nje tangu Februari, alikuwa amekosa mechi mbili za awali za ligi za Al Nassr na hakuwemo katika mechi za kirafiki za Ureno dhidi ya Mexico na Marekani mwezi uliopita.

Ushindi huo wa 13 mfululizo wa ligi kwa Al Nassr umewafanya kuwa kwenye kilele cha msimamo kwa pointi 70, wakiwa na tofauti ya pointi tano mbele ya Al Hilal walio katika nafasi ya pili.

Al Nassr imesaliwa na mechi saba mbele yao hivyo kama watafanya vizuri katika mechi hizo huenda akashuhudiwa Ronaldo akitwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo, 2023.

Kwa upande wa wafungaji huko Saudia kwa sasa Ronaldo anashika nafasi ya tatu akiwa na mabao 23 nyuma ya Toney wa Al Ahli SC na Quinones wa Al Qadsiah kila mmoja akiwa na mabao 26.