Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tajiri mo Dewji ametufikirisha sana

DEWJI Pict

Muktasari:

  • Ndipo hapa kijiweni tukaona ujumbe wa Mwekezaji wa Simba, bilionea Mohammed Dewji akihoji kuhusu mchakato wa mabadiliko ya muundo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

JUMANNE ya wiki hii, Simba ilikuwa na mkutano na waandishi wa habari pale maeneo ya Posta, Dar es Salaam kwa lengo la kutoa taarifa ya kurejeshwa kwa usajili wa wanachama na mashabiki.

Kama ilivyozoeleka kwamba kunapokuwa na jambo lolote linaloihusu Simba, kurasa zao za mitandao ya kijamii huwa zinachangamka kwelikweli.

Ndipo hapa kijiweni tukaona ujumbe wa Mwekezaji wa Simba, bilionea Mohammed Dewji akihoji kuhusu mchakato wa mabadiliko ya muundo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Ni swali ambalo limefikirisha wengi hapa kwenye kijiwe hasa ukizingatia nguvu na ukubwa ambao aliyeuliza anao ndani ya klabu hiyo.

Kwanza limetufanya tuhisi kwamba kuna mawasiliano duni baina ya viongozi wa klabu hiyo kwani yangekuwepo, bosi asingediriki kujitokeza hadharani na kuhoji jambo ambalo alipaswa kupata mrejesho angalau kutoka kwa wajumbe wa bodi kutoka upande wake yeye kama mwekezaji.

Jambo jingine ni kwamba kupitia swali lile, mwekezaji anatufikirisha kwamba kinachosemwa kuhusu yeye kutoafiki usajili wa wanachama na mashabiki ndani ya klabu hiyo ni jambo sahihi.

Hatua ya usajili wa wanachama na mashabiki ni miongoni mwa mambo muhimu katika mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu maana inasaidia kuipa thamani zaidi klabu.

Mwekezaji kuhoji kuhusu mabadiliko pasipo kusapoti usajili wa wanachama ni kututhibitishia kwamba kwake usajili wa wanachama na mashabiki sio kipaumbele ingawa ni hatua muhimu katika mchakato.

Yote kwa yote, kijiwe kinaamini kwamba viongozi wa Simba ambao ni wale kutoka upande wa wanachama na upande wa mwekezaji, wanapaswa kuimba lugha moja.