Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba haikustahili ‘kufa kiume’, iliidharau Kaizer Chiefs

Muktasari:

Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali kuhusu kuondolewa kwa Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya kushindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani na hivyo kushindwa kwa jumla ya mabao 4-3.

Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali kuhusu kuondolewa kwa Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya kushindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani na hivyo kushindwa kwa jumla ya mabao 4-3.

Mijadala hiyo imejaa sifa kwa Simba kutokana na jinsi ilivyojikakamua kwenye Uwanja wa Mkapa na kufunga mabao matatu ambayo hayakutosha kugeuza matokeo ya mechi ya kwanza iliyofanyika Afrika Kusini ambako Simba ililala kwa mabao 4-0.

Na kwa wale wenye ushabiki, yule aliyekosoa mkakati wa Simba katika mechi hizo mbili alishambuliwa vikali na kuitwa majina yaliyokuwa karibu katika midogo ya watoaji sifa. Wengi walitaka washiriki wa mijadala waeleze jinsi Simba ilivyokaribia kufuzu, lakini ikakosa bao moja ambalo lingefanya timu hizo zilingane kwa idadi ya mabao na hivyo kuongezewa muda au mikwaju ya penati ambayo imani ilikuwa Simba ingeshinda kama ilivyowahi kuitoa timu nyingine ya Afrika Kusini huko nyuma.

Sifa hizo na ukali huo umezuia wengi wenye mawazo tofauti kuzungumzia kasoro za Simba katika mechi hizo mbili zilizosababisha kwa mara nyingine iishie robo fainali. Kwa hiyo sentensi inayokubalikana inayopendeza masikioni mwa wengi ni “Simba imekufa kiume”.

Lakini kufa ni kufa. Awe mwanamke amekufa au mwanaume, wote wanakuwa wamepoteza maisha na hawaishi tena duniani.

Katika fasihi tunafundishwa kuwa muhusika mkuu huwa hafi katikati ya hadithi. Ni lazima awepo hadi mwisho hata kama alikutana na balaa lililomjeruhi vibaya, ni lazima aonekane hadi mwisho na kazi iliyosababisha ajeruhiwe, ikionekana kuzaa matunda mwishoni mwa hadithi.

Mtunzi akimuua mapema muhusika mkuu, basi huchukuliwa kama hadithi hiyo haikuwa na mwisho mzuri au anti-climax.

Tangu mechi ya kwanza, Simba haikuonekana kuwa na mkakati mzuri wa kucheza mechi za mtoano na hili limejirudia katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kutolewa na TP Mazembe katika hatua hiyo miaka mitatu iliyopita.

Kaizer Chiefs ni timu ambayo inachukuliwa kuwa haitishi wapinzani wake, lakini ni hatari inapokuwa uwanjani. Na wengi wamejikuta wakidhurika kwa kuamini kuwa hawatapata shida kwa vigogo hao wa Afrika Kusini. Na kwa mwenendo wao kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini, ni rahisi kuchukulia kuwa si timu kali, achilia mbali staili yao ya kucheza mpira ambayo si ya kurefusha mambo, bali kwenda moja kwa moja kwa kitu inachokitaka.

Pengine ni imani hiyo iliyomfanya kocha Didier Gomez aone kuwa angeweza kupata ushindi ugenini na nyumbani na hivyo kucheza mechi ya kwanza akishambulia tangu filimbi ya kwanza hadi ya mwisho. Kaizer walipopata bao la kwanza, Gomez hakuchukua tahadhari. Akaendelea kushambulia kwa nguvu zote, huku umiliki wa mpira ukionekana kumpa moyo kuwa alikuwa na kazi nyepesi.

Hata wenyeji walipopata bao la pili, Gomez hakujifikirisha. Aliendelea kuwashambulia kwa nguvu zote, akiamini kuwa bao la ugenini lingemrahisishia kazi nyumbani. Kumbe alikuwa akijichimbia shimo refu zaidi baada ya Wasauzi kutundika mabao mengine mawili na hivyo kuwa mlima mrefu kwake. Angefanya nini mechi ya pili? Hakuwa na njia nyingine bali kuendelea kushambulia tangu filimbi ya kwanza. Na hapo ndipo wengi wanapoangalia kwa kuwa mashambulizi yalizaa matunda ambayo hayakutosha.

Lakini mwenzake alijua kuwa ameshamaliza mchezo baada ya ushindi mkubwa wa nyumbani. Huku alipania kuanza kwa nguvu ili kuizuia Simba isipate bao la mapema kwa kuwa aliiheshimu na alijua uwezo wa vigogo hao wa Msimbazi. Hadi dakika ya 20, alikuwa amepunguza muda wa Simba kupata ushindi mnono.

Kikubwa zaidi akawa ameongeza pressure kwa wachezaji, ambao walijua kuwa wana muda mfupi wa kufanya maajabu. Hali hiyo siku zote husababisha wachezaji kutofanya maamuzi sahihi wanapokuwa maeneo muhimu, kwa hiyo haikuwa ajabu akina Bocco na Mugalu kutofanya maamuzi sahihi mbele ya lango huku dakika zikiyoyoma.

Mabadiliko ya mapema ya kumuingiza Bernard Morrison na yale ya kulazimishwa ya kumtoa Joash Onyango na Lwanga yalipunguza wigo wa kufanya mabadiliko muhimu waati muhimu. Katika hali ya kawaida, kocha hawezi kubadili beki wa kati na kiungo wa nyuma, labda pale anapoona kuna haja ya kufanya mabadiliko ya kimkakati kwa kumtoa kiungo wa nyuma na beki na kuingiza wachezaji wenye akili ya kuishambulia Zaidi ili kuongeza uwezekano wa kupata mabao. Huku akiwa na muda mfupi na akiwa amemaliza mabadiliko, Gomez alisubiri zaidi miujiza kuliko mbinu na kujikuta akitumbukiza katika shimo lilelile la miaka mitatu iliyopita.