Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namungo, Simba ilikuwa shoo ya Kibabe

Muktasari:

Mchango mkubwa wa Chris Mugalu katika ushindi wa mabao 3-1 ambao Simba iliupata ugenini dhidi ya Namungo huko Ruangwa, Lindi ni uthibitisho tosha wa namna vita ya washambuliaji inavyoinufaisha Simba.

Mchango mkubwa wa Chris Mugalu katika ushindi wa mabao 3-1 ambao Simba iliupata ugenini dhidi ya Namungo huko Ruangwa, Lindi ni uthibitisho tosha wa namna vita ya washambuliaji inavyoinufaisha Simba.

Wakati mjadala wa kupungua kwa makali yake ukiwa ndio kwanza umeanza kushika kasi, Mugalu ametumia miguu yake kuwajibu wakosoaji wake baada ya kuhusika katika mabao mawili kati ya matatu ambayo Simba ilifunga katika mchezo huo.

Baada ya kukosa mabao ya wazi katika mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs ambao Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 ambao hata hivyo haukutosha kuwapeleka nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, juzi Mugalu aliwapa furaha mashabiki wa Simba kwa kazi nzuri aliyofanya

Mshambuliaji huyo alifunga bao la kusawazisha akiunganisha pasi ya Shomari Kapombe kabla ya baadaye kupiga pasi iliyozaa bao la pili lililopachikwa na John Bocco na Bernard Morrison akaja kufunga la tatu wakati bao pekee la Namungo likifungwa na Nzigamasabo Styve.

Ubora wampa jeuri Gomes


Kwa mara nyingine tena, ubora wa kitimu ktika kufanyia kazi mbinu na uwezo wa mchezaji mmojammoja wa Simba uliendelea kuifanya kazi ya kocha Didier Gomes Da Rosa kuwa nyepesi.

Kitendo cha wachezaji Hassan Dilunga, John Bocco na Morrison kwenda kubadili aina ya mchezo wa Simba ni ishara tosha ya namna benchi la ufundi la Simba lilivyo na kazi rahisi kulinganisha na timu nyingine.

Tofauti na awali ambapo Simba ilichelewa kufika kwa haraka katika lango la Namungo kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuchelewa kuuchia mpira, Bocco, Dilunga na Morrison waliifanya Simba icheze kwa haraka jambo lililoipa wakati mgumu Namungo.

Ukuta umeiangusha Namungo

Pamoja na ubora wa Simba, walinzi wa Namungo kwa upande mwingine walichangia timu hiyo kupoteza mchezo wa juzi.

Mawasiliano baina yao hasa wale wa kati na nidhamu ya mbinu ilikosekana kwao jambo lililopelekea wawape mwanya wapinzani wao kucheza kwa uhuru jirani na lango lao na kutengeneza nafasi nyingi ambazo mbili kati ya hizo zilizaa mabao mawili ya Simba.

Lakini pia mabeki wa pembeni wa Namungo walionesha kutokuwa na msaada katika ulinzi kwa kuruhusu Simba wapige krosi nyingi kutokea pembeni wakati huo wakishindwa hata kupanda mbele kusaidia mashambulizi.

Mabadiliko hayakuisaidia Namungo

Wakati Simba wakinufaika vilivyo na mabadiliko ya wachezaji waliyoyafanya katika mchezo huo, hali ilikuwa tofauti kwa Namungo FC.

Wachezaji watatu walioingia, Stephen Sey, Abeid Athuman na Lucas Kikoti kuchukua nafasi za Shiza Kichuya, Ibrahim Abdallah na Abdulhalim Humud walishindwa kutoa msaada kwa timu na kujikuta wakielemewa na Simba

Sey aliwapa uhuru mabeki wa kati wa Simba kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma wakati Kikoti hakuipa uimara Namungo katika eneo la kiungo na Abeid Athuman muda mwingi alicheza kibinafsi pembeni na hivyo kukosa madhara langoni mwa Simba.

Bao la Morrison saluti

Bao la mshambuliaji Bernard Morrison ni ishara tosha ya jinsi nyota huyo wa Simba ambavyo akili yake inafanya kazi kwa haraka pindi awapo uwanjani

Mara baada ya kupokea mpira kutoka kwa Lwanga Taddeo akiwa jirani na mstari unaogawa uwanja, Morrison alimtazama kwa haraka kipa Jonathan Nahimana na kubaini amesogea mbele na alivyofundua hilo akapiga shuti la mbali ambapo mpira ulimshinda kipa huyo na kujaa wavuni.

Linaweza kuwa bao lililofungwa kwa umbali mrefu zaidi katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu lakini huenda likawa miongoni mwa mabao yatakayowania tuzo ya bao bora la msimu.