Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Gamondi wajiandae kisaikolojia wakikubaliana

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Kuna hadi makocha waliowahi kuifundisha Simba hapo nyuma na wengine wana uzoefu na soka la Tanzania ambalo kulitumikia kwa nyakati tofauti.

ZA ndani ambazo kijiwe kimezinasa katika mchakato wa Simba kusaka kocha mkuu mpya ni kwamba kuna kundi kubwa la makocha wa nje na ndani ya Afrika ambao wameomba kazi hiyo.

Kuna hadi makocha waliowahi kuifundisha Simba hapo nyuma na wengine wana uzoefu na soka la Tanzania ambalo kulitumikia kwa nyakati tofauti.

Tetesi zinaripoti kwamba miongoni mwa makocha waliotuma maombi yao ya kazi kwa uongozi wa Simba ni kocha wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi ambaye kwa sasa ni Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars.

Gamondi ni kocha aliyejijengea heshima kubwa sana katika soka la Tanzania hasa kutokana na jinsi alivyoiongoza Yanga kufanya vizuri alipoifundisha kabla ya kuachana nayo na kuhamishia majeshi Singida.

Hatujui uongozi wa Simba kama utaamua kumpa kazi Gamondi au utaamua kumtosa, lakini ikiwa Muargentina huyo atakula ajira kwenye timu hiyo, kila upande unatakiwa ujiandae kisaikolojia.

Simba itapaswa kufahamu kwamba inamchukua kocha ambaye ana misimamo na hapendi kuingiliwa mara kwa mara katika utendaji wake wa kazi huku pia akipenda kutoa uhuru kwa wachezaji.

Lakini Gamondi atatakiwa aelewe kwamba anaenda katika timu ambayo mashabiki wake hawatokuwa marafiki wa kudumu na watahitaji timu yao ipate matokeo mazuri hasa katika mechi dhidi ya watani wao Yanga.

Ikitokea Gamondi akapewa timu na ikapoteza dhidi ya Yanga tena kwa kucheza vibaya, haohao mashabiki watamtazama kwa jicho la tofauti na huenda asidumu ndani ya timu hiyo.

Mfano wa Dimitar Pantev unaweza kuwa mzuri zaidi. Alitua Simba kwa mbwembwe, lakini hakufikisha hata mechi sita.