Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Schurrle anahitaji kuondoka Chelsea

Muktasari:

Kabla kuhamia Chelsea, Schurrle alikuwa nyota wa timu yake ya Bayer Leverkusen na alikuwa kati ya wachezaji bora katika Ligi ya Ujerumani. Hata hivyo, ilikuwa wazi kwamba ingekuwa vigumu kwa Schurrle kuchukuwa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea.

KILA mchezaji wa mpira ana ndoto ya kucheza katika klabu kubwa barani Ulaya.

Ilikuwa ni ndoto hiyo iliyomsukuma Andrea Schurrle kuhamia na kusaini mkataba na Chelsea akiwa na umri wa miaka 21 tu mwaka 2013.

Kabla kuhamia Chelsea, Schurrle alikuwa nyota wa timu yake ya Bayer Leverkusen na alikuwa kati ya wachezaji bora katika Ligi ya Ujerumani. Hata hivyo, ilikuwa wazi kwamba ingekuwa vigumu kwa Schurrle kuchukuwa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea.

Ni kwa kuwa Chelsea ilikuwa na kikosi chenye upinzani mkubwa sana. Katika nafasi ya Schurrle, Chelsea ilikuwa pia imemsajili Willian kutoka Schaktar Donetsk.

Mwanzoni mwa msimu uliopita Schurrle na Willian wote walipewa nafasi za kucheza. Lakini baada  ya miezi kadhaa ilikuwa wazi kwamba Willian alikuwa chaguo la kwanza la Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho. Schurrle alijikuta  akisugua benchi.

Mourinho ni kocha mwenye falsafa ya kufanya mabadiliko machache katika kikosi chake cha kwanza.

Akishawajua wachezaji wake bora, basi atajaribu kuwapanga katika karibu kila mechi. Kwa mfano, kwa mtazamo wangu, Eden Hazard amekuwa mchezaji bora katika kikosi cha Chelsea msimu huu. Mchezaji huyu amepangwa katika kila mechi ya Ligi Kuu! Mfano mwingine ni Cesc Fabregas ambaye amepangwa katika mechi zote za Ligi Kuu kasoro moja tu. Tofauti na makocha wengine kama Arsene Wenger, Mourinho haamini kwamba anahitaji kuwapumzisha wachezaji wake katika ligi.

Kwa hiyo wachezaji kama Schurrle ambao wapo katika benchi wanapewa nafasi chache za kucheza.

Kuna mashindano mawili tu ambapo Mourinho anaweza kufanya mabadiliko katika kikosi chake cha kwanza na kuwapa wachezaji wengine nafasi ya kucheza.

Mashindano haya ni Kombe la FA pamoja na  Kombe la Ligi. Mourinho anawapa nafasi wachezaji wengine katika mashindano haya kwa sababu huwa kuna upinzani laini ingawa Chelsea ilifungwa na klabu ya daraja la tatu, Bradford Jumamosi iliyopita.

Schurrle siyo mchezaji wa kwanza kuathirika na falsafa za Mourinho. Kila mwisho wa msimu mashabiki wa Chelsea wanampigia kura mchezaji bora katika kikosi cha Chelsea.

Msimu wa 2012-2013 Juan Mata alipewa tuzo hiyo. Lakini hata hivyo Mourinho aliamua kumwacha mchezaji huyu benchi tangu mwanzo wa msimu uliopita.

Mourinho aliamini kwamba Oscar ni mchezaji bora kuliko Mata kwa kuwa mchezaji huyu anakaba zaidi. Mata kama ilivyo kwa Schurrle sasa, alijikuta akisugua benchi.

Kutokana na kupewa nafasi chache sana za kucheza, Juan Mata alihamia Manchester United, wakati usajili wa dirisha dogo ulipofunguliwa. Kwa sasa dirisha dogo lipo wazi kabisa na mchezaji kama Schurrle ambaye ana kipaji cha kutosha anaweza kuondoka. Kinachompasa  kufanya mchezaji huyo ni kujiunga na timu ili apate nafasi ya kucheza mechi nyingi zaidi.

Binafsi nina matumaini kwamba Schurrle naye atafuata mfano wa Mata wa kukubali kuondoka Chelsea na kwenda kwenye timu nyingine, kwani chini ya Mourinho mchezaji huyu hatapata nafasi ambayo anastahili kuipata.