Penalti kila kona raundi ya 19 Ligi Kuu Bara

Saturday February 20 2021
PENATI PIC
By Yohana Challe

LIGI Kuu Tanzania Bara inaende-lea leo Jumamosi katika michezo ya mzunguko wa 20 na baadhi ya timu zikicheza mzunguko wa 19.

Katika michezo ambayo ilipigwa wikiendi iliyopita na ile ya katikati ya wiki kumeonekana ushindani mkubwa kwa timu katika kusaka alama tatu.

Hii ni michezo ya lalasalama am-bapo timu husaka kujinasua na kushuka daraja na vigogo wanaokimbizana kile-leni husaka alama ili kutwaa ubingwa.

Katika michezo iliyopigwa ndani ya wiki moja kumeshuhudiwa mambo mengi yakijitokeza ndani na nje ya uwanjani yakiwa gumzo, huku Ihefu SC ikijiondoa eneo la hatari taratibu na sasa ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo.


MECHI KALI YA WIKI

Advertisement

Mchezo ambao ulikuwa umejaa ushindani wa hali ya juu ni ule ulioikutanisha Yanga dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.Katika mchezo huo wenyeji, Yanga, ilikuwa na kazi kukomboa mabao baada ya kutanguliwa katika mabao matatu, kwa bao lililofungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 14 kwa mkwaju wa penalti.

Mabao mengine yalifungwa na Deus Kaseke dakika ya 30 na Mukoko Tonombe dakika ya 61 wakati yale ya Kagera Suga yakifungwa na Peter Mwalyanzi dakika ya 11, Hassan Mwa-terema dakika ya 24 na Yusuph Mhilu dakika ya 45+2. PENALTI ZATAWALA

Katika michezo hiyo imeshuhudia penalti sita zikitolewa na kati ya hizo nne zikiwa za timu wenyeji na wageni penalti mbili.Michezo iliyozaa penalti ni ule wa Mbeya City na Yanga penalti iliyofungwa na Pastory Atanas katika mchezo uli-omalizika kwa sare ya bao 1-1, Mwadui 1-2 Biashara United penalti ya Yusuph Athuman, KMC 2-1 Mwadui penalti ya Emmanuel Mvuyekure wa KMC.

Penalti nyingine zilifungwa na Tuisila Kisinda kwenye mchezo wa wiki hii uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3 na Kagera, Dany Lyanga wa JKT Tanzania kwenye sare ya bao 1-1 mbele ya Polisi Tanzania iliyosawazisha kwa penalti pia iliyofungwa na Marcel Kaheza. YANGA PRESHA

Yanga ipo kileleni lakini mara ya mwisho kupata ushindi ilikuwa Desemba 23 walipoichakaza Ihefu SC 3-0 kwa mabao ya Kaseke, Yacouba Sogne na Feisal Salum.

Baada ya hapo imecheza michezo mitatu na yote ikiam-bulia sare tena ikiwa inafanya kazi ya kukomboa mabao kwenye michezo miwili.Ilianza kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons pale Nelson Madela wati wenyeji wakipata bao kupitia kwa Jumanne Elfadhili dakika ya 52 na Yanga ikisawazisha dakika ya 85 kwa bao la Saidi Ntibaonkiza.

Kabla ya mchezo dhidi ya Kagera ilitoka kuam-bulia sare nyingine dhidi ya Mbeya City ya bao 1-1 ambayo ilisawazi-sha dakika za lala salama baada ya Yanga kuanza kupata bao lililofungwa na Kaseke, Pastory Atanas ikasawazisha kwa Penalti dakika ya 90.


WAAMUZI WABEBA LAWAMA


Katika michezo ya wiki hii lawama nyingi zimewaan-gukia waamuzi kwa kuzibeba timu wenyeji jambo ambalo linaonekana kuanza upya baada ya kuonekana kupotea kwa muda.Tangu msimu uanze waa-muzi walikuwa wakifanya kazi yao vyema bila matatizo wala lawama hizi, lakini sasa upepo umeanza kuwaangukia.

Presha za mashabiki, vi-ongozi na hata wenyewe waamuzi inaweza ikawa sababu ya kuonekana wanalaumiwa lakini kikubwa ni kuongeza umakini katika kutoa uamuzi wao.


 KAULI ZA MAKOCHA


Baada ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata Azam FC ikiwa nyumbani Uwanja wa Chamazi, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Bahati Vivier anasema ni ushindi muhimu kwao ambao una maana kubwa katika kuwania nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.“Tumekuwa kwenye wakati wa changamoto kubwa kwa michezo kadhaa ambayo tumecheza bila kupata ushindi, lakini leo (juzi) tumefanikiwa hii inasaidia kurejesha morali kwa wachezaji na hata timu nzima ambayo haikutulia kwa muda wote,” alisema.Kocha wa Yanga, Cedric Kaze baada ya sare ya mabao 3-3 na Kagera Sugar alisema sio matokeo ya kufurahisha upande wao, japo aliwapongeza vijana wake kwa kupambana na kupata alama moja ambayo inawasaidia kuendelea kukaa kileleni.

“Kuna wachezaji wengi hawakutoa kile ambacho nilitarajia kulikuwa na mabadiliko kama wache-zaji saba, lakini nilifanya wawili awali ili kuweza kuendana na mchezo kwa dakika 90,” alisema Kaze.

Hata hivyo, aliongeza kuwa bado wapo kwenye mbio za ubingwa licha ya kuona ushindani mkubwa hasa katika michezo iliyopo mbele yao ambayo inamfanya kupambania  alama tatu.

Advertisement