Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome hajaisha tusiangalie namba tu

Muktasari:

  • Mtu unakuta amemchoka tu mchezaji fulani au ameibuka mchezaji mwingine mzuri basi anaanza kutengeneza dhana ya kumfanya yule mchezaji wa mwanzo aonekane hafai.

WAKATI mwingine Tanzania tumekuwa tukiwapoteza wachezaji wazuri kwa sababu ya dhana tu ya watu wachache.

Mtu unakuta amemchoka tu mchezaji fulani au ameibuka mchezaji mwingine mzuri basi anaanza kutengeneza dhana ya kumfanya yule mchezaji wa mwanzo aonekane hafai.

Pia hata mchezaji akicheza kwa muda mrefu, Watanzania wengi tumekuwa na hulka ya kumfanya aonekane amechoka hata kama kiuhalisia haiko hivyo.

Kwenye kijiwe hapa tumeuone mjadala unaoendelea kuhusu kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua kiwango chake kimeporomoka.

Watoa hoja wamechagua mechi kadhaa chache ambazo hakucheza vizuri ndio wanazitumia kumpiga utosini Pacome.

Ila kiuhalisia Pacome hajaisha na miongoni mwa wachezaji bora na wenye mchango mkubwa zaidi katika kikosi cha Yanga.

Huyo Pacome ambaye watu wanasema ameshuka kiwango, msimu huu ameshachangia kupatikana kwa mabao 11 ya Yanga kwenye Ligi Kuu, akifunga saba na kupiga pasi nne za mwisho.

Lakini tukiachana na hizo namba, emu tuwe tujaribu kuangalia pia na vitu vingine vya muhimu ndani ya uwanja.

Inawezekana mchezaji akawa hafungi au hapigi pasi za mwisho lakini uchezaji wake ukawa ndio chachu ya kupatikana kwa hivyo vitu.