Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Bayern mwenye asili ya Bongo ataja sababu kutimkia Uswisi

Muktasari:

  • Irankunda ni mzaliwa wa Tanzania mkoani Kigoma ambako alizaliwa Februari 9, 2006 na wazazi walioingia kama wakimbizi kutokea Burundi, kabla ya familia hiyo kutimkia Australia ambako ndiko inakoishi.

WINGA wa Bayern Munich, Nestory Irankunda mwenye asili ya Tanzania ametolewa kwa mkopo na klabu hiyo kwenda Grasshopper Club Zurich ya Uswisi.

Irankunda ni mzaliwa wa Tanzania mkoani Kigoma ambako alizaliwa Februari 9, 2006 na wazazi walioingia kama wakimbizi kutokea Burundi, kabla ya familia hiyo kutimkia Australia ambako ndiko inakoishi.

Winga huyo ambaye kwa sasa ana uraia wa Australia, alijiunga na mabingwa hao wa zamani wa Ujerumani akitokea Adelaide United ya Ujerumani aliyoitumikia kwenye timu za vijana za U-19, 21.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Bayern Munich, Jochen Sauer anasema lengo la kumtoa kwa mkopo kwenda Uswisi ni kumpatia uzoefu wakiahidi kumsaidia kwa karibu katika safari yake ya soka. “Nestory ameweza kujiunga vyema baada ya kuhamia kutoka Australia hadi Ulaya, na mara kadhaa ameonyesha kipaji kikubwa akiwa na timu yetu ya akiba,” anasema Sauer.

“Tunaamini atachukua hatua nyingine muhimu za kisoka katika ligi ya juu ya Uswisi akiwa na GC Zurich. Kama Bayern tutaendelea kumsaidia kwa karibu katika safari yake.”

Baada ya kutambulishwa wiki iliyopita na mabingwa hao wa Uswisi waliowahi kuishia hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 1977-78, Irankunda anasema anafurahi kuwa sehemu ya timu hiyo yenye historia nchini humo.

“Nina furaha kuwa hapa, kuungana nanyi kama familia na naamini tutashirikiana kuhakikisha tunafikia mafanikio ya klabu hii kubwa, asante,” anasema.

Nyota huyo alikipiga kwa msimu mmoja Bayern Munich akiwa mchezaji wa akiba akicheza mechi 15, kufunga mabao manne na kutoa asisti nne.

Katika Ligi ya Vijana ya Uefa alicheza mechi tatu na timu ya vijana ya Bayern Munich U19 akifunga bao moja..


HIKI KIMEMUONDOA

Akizungumza na chombo kimoja cha habari Ujerumani, Irankunda anasema sababu ya kuondoka Bayern Munich ni kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza, akiishia kuambulia benchi.

“Nilizungumza na kocha muda mrefu. Nilitaka kucheza kwenye kiwango cha juu, ligi kubwa na katika klabu nzuri. Nilijadiliana na klabu na makocha kuhusu kwenda kwa mkopo (sehemu nyingine) kwa sababu nilihisi itakuwa bora kwangu,” anasema.

“Lazima nicheze, siwezi kuendelea kucheza katika timu ya wachezaji chini ya miaka 23 kila wiki.” Hata hivyo, anaeleza kwamba licha ya kutocheza, lakini alifurahia kufanya mazoezi na wachezaji maarufu.

“Kumuona Vincent Kompany, kocha, ilikuwa kama ndoto. Yeye ni gwiji, halafu, bila shaka kuwaona wachezaji kama Harry Kane na Leroy Sane ni bora zaidi kwa sababu wao ni wachezaji wa viwango vya juu.”


NDANI YA BAYERN

Akiwa Bayern Munich, Irankunda hakupata nafasi kubwa ya kucheza kutokana na ushindani, ingawa awali kuhamia kwake klabuni hapo kulipokewa kwa shangwe kubwa nchini Australia wakati timu ya taifa ya taifa hilo (Socceroos) ikijivunia kipaji chake.

Hata hivyo, Irankunda anaamini Bayern Munich ilimpa uzoefu mkubwa licha ya kutopata namba akikaa benchi kushuhudia mechi kubwa za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Irankunda pia alijizolea sifa kwa maonyesho yake wakati wa mazoezi ya kabla ya msimu ambayo yaliibua matarajio kumuona akiwa na kikosi cha kwanza cha Bayern Munichi..


MATARAJIO YA USWIZI

Irankunda anajiunga na Grasshoppers ambayo iko kwenye hali mbaya ya kutopata matokeo mazuri kwenye Ligi Daraja la Kwanza.

Grasshoppers iko nafasi ya 11 kati ya timu 12 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikishinda michezo mitatu, sare sita na kupoteza michezo tisa.

Malengo ya timu hiyo ni kusalia angalau katika ligi hiyo ikiamini uwepo wa Irankunda utaongeza chachu kwenye eneo la ushambuliaji.

Uwezo wa nyota huyo unatabiriwa kuongeza ushindani kwani hadi raundi ya 18 timu hiyo haijaonyesha makali ikizingatiwa kwamba haina straika mwenye bao.