Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni mwaka wa furaha, penzi la Firmino, Larissa

SHOWBIZ Pict

Muktasari:

  • Philippe Coutinho ambaye aliwahi kucheza na Firmino kule Liverpool hadi mwanzoni mwa mwaka huo, ndiye alikuwa msimamizi (best man) wa ndoa hiyo. Pia wachezaji wenzake kama Alberto Moreno, Allan Souza na Lucas Leiva walihudhuria.

FURAHA na mapenzi, ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kile ambacho Roberto Firmino, 34, na mkewe Larissa Pereira, 33, wanatarajia mwaka huu, ikiwa ni baada ya kuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 10.

Firmino, mchezaji wa zamani wa Liverpool, alikutana Larissa kwa mara ya kwanza 2013 katika klabu ya usiku, na 2014  walianza rasmi uhusiano ambao hadi sasa unapeta. Wawili hao walifunga ndoa Juni 2017 katika sherehe ya kifahari iliyofanyika Maceio, Brazil, ambako wote wanatokea, na hata Firmino alishawahi kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyo. 

Philippe Coutinho ambaye aliwahi kucheza na Firmino kule Liverpool hadi mwanzoni mwa mwaka huo, ndiye alikuwa msimamizi (best man) wa ndoa hiyo. Pia wachezaji wenzake kama Alberto Moreno, Allan Souza na Lucas Leiva walihudhuria.

SHOW 03

Ikumbukwe Liverpool ilimsajili Firmino 2015 akitokea TSG 1899 Hoffenheim ya Ujerumani. Alifanya vizuri ndani ya kikosi hicho kilichopata mafanikio makubwa ndani ya misimu minane chini ya kocha Jurgen Klopp.

Kwa ujumla kati ya 2015 hadi 2023, aliichezea Liverpool mechi 362 akifunga mabao 111 na kutwaa mataji kadhaa likiwemo Ligi Kuu England (EPL), FA, EFL na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nyuma ya mafaniko ya Firmino uwanjani alikuwepo mwanamke mmoja. Naye ni Larissa ambaye anaisimamia vizuri nafasi yake akiwa rafiki, mshauri, mke na mama wa familia.

Larissa ni mwanamitandao mwenye umaarufu hasa Instagram. Pia ni mwanamitindo ambaye amefanikiwa kufanya kazi ya uanamitindo na chapa mbalimbali za mavazi ya kuogelea (swimwear).

SHOW 04

Mbali na urembo, Larissa pia ni mfanyabiashara. Ni mwanzilishi wa chapa ya mitindo ijulikanayo kama BeValen Store, chapa ambayo mara kadhaa huitangaza kupitia ukurasa wa Instagram. 

Kwa miaka mingi, Larissa ameonekana kuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Firmino. Yupo naye tangu kipindi anacheza Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga) hadi sasa akiwa na Al Sadd inayoshiriki Qatar Stars League.

SHOW 02

Desemba 12, 2025, Larissa aliadhimisha siku ya kuzaliwa akitimiza umri wa miaka 33, ambapo mumewe Firmino alitumia ukurasa wake wa Instagam wenye wafuasi milioni 15.1 kumtakia heri na kumtaja kama zawadi bora zaidi.

SHOW 05

"Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu!. Namshukuru sana Mungu kwa ajili ya maisha yako. Namshukuru yeye kila siku kwa kunipa zawadi nzuri kuliko zote nilizowahi kupokea," alisema na kuongeza:

"Asante kwa mwanamke uliyekua katika Kristo, kwa kuwa mama wa mfano katika familia yetu na mtumishi wa Mungu, mwenye kumcha Mungu, mwenye busara na aliyejaa roho mtakatifu.".

Hadi sasa wawili hao katika ndoa wamejaliwa kupata watoto wanne na wote wakiwa wa kike. Watoto hao ni Valentina (2014), Bella (2016), Clara (2018) na Mateo (2023). Novemba 2025, walitangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto wa tano na baadaye walitoa taarifa nyingine maalumu wakieleza kuwa wanatarajia mtoto wa kiume.

SHOW 06

Taarifa hiyo ilipokewa kwa furaha kubwa na mashabiki wao, hasa ikizingatiwa kuwa tayari wana mabinti wanne, hivyo kupata wa kiume ni kuzidi kuongeza furaha ndani ya nyumba. Hilo ndilo jambo ambalo wanalisubiri kwa hamu zaidi mwaka huu, na mara kwa mara Larissa kupitia Instagram ambapo ana wafuasi zaidi 500,000 amekuwa akiposti picha za ujauzito wake. 

Baada ya kutangaza ujauzito huo walipokea ujumbe mwingi wa pongezi. Miongoni mwa ujumbe huo ulisema: "Ah, furaha iliyoje rafiki yangu! Nimefurahi sana kwa ajili yenu, Mungu ambariki sana huyu mtoto."

Shabiki mwingine aliandika: "Hongera Lari!, Mungu awabariki zaidi kila siku, muwe na Afya njema tele, na hongereni. Hii ni habari njema na ya kusisimua." Akiwa kama mchezaji aliyefanikiwa kisoka na kiuchumi, Firmino anafurahia kuwalea watoto wake katika mazingira mazuri na kuwapatia mahitaji muhimu kitu ambacho yeye alikikosa.

SHOW 07

Firmino aliwahi kueleza kuwa huko kwao Brazil alikulia katika mazingira ya umaskini na eneo waliloishi lilikuwa lenye uhalifu wa magenge na matumizi ya silaha. Wazazi wake, Jose Roberto Firmino na Mariana Cicero walijitahidi kumlinda dhidi ya mazingira hayo na hata wakati mwingine kumzuia kutoka nje ili kulinda usalama wake.

Hata hivyo, kwa sasa mambo yamebadilika Firmino anaishi maisha mengine kabisa akitaka kuwa na familia kubwa ambayo anaweza kuihudumia na kuipa usalama wa uhakika.

SHOW 01

Kwa ujumla, maisha ya Firmino yanaonyesha safari ya kijana aliyekulia katika mazingira magumu, lakini akafanikiwa kupitia kipaji, juhudi na msaada wa familia. Leo hii, si tu supastaa mkubwa wa soka, bali pia ni baba mwenye upendo na mume anayethamini familia.