Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma nzito: Hapa Mkongomani, kule Saleh Karabaka

LIGI KUU Pict

Muktasari:

  • Mabao matatu yaliyokamilisha idadi ya 188 yanayosemeka kwa sasa kupitia mechi hizo yametokana na ushindi wa mezani waliopewa Pamba Jiji dhidi ya Dodoma Jiji, lakini pia kukiwa na mabao saba ya wachezaji waliojiweka wenyewe hadi sasa.

LIGI Kuu Bara imesimama kupisha mechi za Kombe la Shirikisho (FA), lakini kama hujui ni kwamba hadi sasa zimeshachezwa mechi 102 kati ya 240, huku ikishuhudiwa mabao 185 kati ya 188 yakitinga nyavuni, lakini kuna vita nzito inaendelea baina ya mastaa wazawa na wale wa kigeni.

Mabao matatu yaliyokamilisha idadi ya 188 yanayosemeka kwa sasa kupitia mechi hizo yametokana na ushindi wa mezani waliopewa Pamba Jiji dhidi ya Dodoma Jiji, lakini pia kukiwa na mabao saba ya wachezaji waliojiweka wenyewe hadi sasa.

Wakati zikiwa zimesalia mechi 138 ili kukamilisha 240 za msimu mzima, tayari kuna vita ya ufungaji mabao inayoendelea kwa mastaa hao wa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo na kuashiria huenda mambo yakanoga msimu huu pengine kuliko msimu uliopita, japo hakuna mwenye uhakika kama idadi ya mabao itaizidi ile ya msimu uliopita iliyoshuhudiwa yakifungwa 571 kupitia mechi 240.

Kwa misimu mitatu mfululizo nyota wa kigeni ndio waliotawala kwa kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa ligi hiyo, lakini kasi waliyoanza nayo wazawa imeonyesha huenda msimu huu mambo yakawa freshi na kiatu cha dhahabu kikarudi mikononi mwao, japo wanatakiwa kupambana kweli.

LIGI 01

Takwimu zinaonyesha hadi mechi 102 za ligi ya msimu huu, nyota wazawa 69 wamechangia jumla ya mabao 123 kati ya 185, yakiwamo sita ya kujifunga, huku mapro wa kigeni 33 wenyewe wamechangia mabao 62 hadi sasa, likiwamo moja la kujifunga.

Wastani wa wachezaji wa kigeni 33 waliochangia mabao 61 ni kila mmoja 1.84, wakati kwa wazawa 69 waliochangia mabao 177 ni wastani wa 1.69, huku wastani wa kufungwa kwa mabao hadi sasa kupitia mechi hizo 102 ni 1.81 sawa na ile ya wachezaji wote waliochangia mabao hayo 185.

Katika orodha ya wanaoongoza kwa kufunga hadi sasa kinara ni nyota wa kigeni anayekipiga Namungo, Fabrice Ngoy aliyekwamisha mabao saba akifuatwa kwa karibu na nyota mzawa Saleh Karabaka wa JKT Tanzania aliyefunga mabao sita anayefuatiwa na wazawa wengine wawili.

Nyota hao wawili wanaopambana kukirejesha kiatu cha dhahabu kwa wazawa ni Paul Peter pia wa JKT Tanzania na Edgar William wa Dodoma Jiji ambao kila mmoja amefunga mabao matano, huku wakifuatiwa nyuma na wageni wawili, Prince Dube wa Yanga na Mathew Momanyi wa Pamba Jiji wenye mabao manne kila mmoja.

Kwa wachezaji wenye mabao matatu, nako kuna vita nzito ya wageni na wazawa, kwani jumla wapo 13, lakini tisa wakiwa wazawa na wanne wakiwa wageni kuonyesha msimu huu mambo ni moto katika kucheka na nyavu.

Wageni waliopo katika orodha hiyo ya wenye mabao matatu ni; Peter Lwasa (Pamba Jiji), Jonathan Sowah (Simba), Pacome Zouzoua na Laurindo Depu (wote Yanga), wakati wazawa wanaongozwa na Feisal Salum na Idd Seleman 'Nado' (wote wa Azam FC), Daruwesh Saliboko (KMC), Seleman Mwalimu (Simba), Valentino Mashaka (JKT Tanzania), Shiza Kichuya (Coastal Union), Fredrick Magata (Mtibwa Sugar), Cyprian Kipenye (Namungo) na George Mpole (TZ Prisons).

Nyuma ya wachezaji hao pia kuna orodha ya nyota 25 waliofunga mabao mawili kila mmoja, wakiwamo tisa wa kigeni na wazawa 16, kisha wakifuatiwa na wengine 60 wenye bao moja moja, 18 wakiwa wa kigeni na 42 wazawa.

Hata hivyo, kwa sasa mashabiki wanasikilizia na kutaka kuona kama kasi ya mabao itaongezeka kupitia mechi 138 zilizosalia ili kuja kupiku rekodi za msimu uliopita ambapo jumla ya mabao 571 yalifungwa kupitia mechi 240 za msimu mzima ikiwa ni wastani wa 2.37 kwa kila mechi.

Lakini msimu huo, wageni 64 walichangia jumla ya mabao 245 ikiwa ni wastani wa 3.82, wakati wazawa 119 walichangia mabao 307 ikiwa ni wastani wa 2.57 wakizidiwa na mapro wa kigeni, ikiwa na maana kwa sasa katika mechi 138 zilizosalia kufungia msimu yanahitajika yafungwe mabao 383 ili kufikia idadi ya mabao ya msimu uliopita.

LIGI 02

Rekodi zinaonyesha tangu George Mpole alipotwaa tuzo ya Mfungaji Bora msimu wa 2021-2022 akimpokea mzawa mwenzake John Bocco, hakuna nyota wa Kitanzania aliyebeba tuzo hiyo tena, kwani wageni wametawala kwa kubeba mara tatu mfululizo.

2022-2023 nyota wawili wa kigeni, Fiston Mayele aliyekuwa Yanga na Saido Ntibazonkiza aliyekuwa Simba walinyakua tuzo kila mmoja akifunga mabao 17 na kupokewa na Stephane Aziz KI aliyekuwa Yanga aliyefunga mabao 21 akimpiku Feisal Salum wa Azam aliyemaliza na mabao 19.

Msimu uliopita nyota mwingine wa kigeni, Jean Charles Ahoua aliyekuwa Simba aliibuka kidedea kwa kufunga mabao 16 na kabla ya Bocco kubeba tuzo 2020-2021, tuzo hiyo kwa misimu mitatu mfululizo pia ilikuwa mikononi mwa wageni.

LIGI 03

Emmanuel Okwi alibeba msimu wa 2017-2018 akiwa Simba kabla ya Meddie Kagere aliyekuwa pia Simba kutwaa mara mbili mfululizo kwa mabao yake kwenye misimu ya 2018-2019 (23) na 2019-2020 (22) kabla ya Bocco aliyekuwa Simba na Mpole aliyekuwa Geita Gold kuwabeba wazawa kwa kutwaa mara mbili mfululizo.

Kwa msimu huu, ni mapema mno kutabiri kutokana na kasi ya ufungaji baina ya wachezaji wa kigeni na wazawa, lakini huenda ikashuhudiwa mfungaji bora wa safari hii akiwa na mabao mengi kuliko yaliyofungwa na Ahoua msimu uliopita aliyekwamisha 16.

LIGI 04

Kwani kwa sasa Ngoy anahitaji bao tisa tu kufikia idadi ya mabao yaliyompa Ahoua ufalme wa msimu uliopita, wakati Karabaka ambaye amekuwa na msimu mzuri akisaka mabao 10 tu. Ngoja tuone!


WAFUNGAJI BORA MISIMU MiNANE ILIYOPITA

2017/18

Emmanuel Okwi (Simba) Mabao 20

2018/19

Meddie Kagere (Simba) Mabao 23

2019/20

Meddie Kagere (Simba) Mabao 22

2020/21

John Bocco (Simba) Mabao 16

2021/22

George Mpole (Geita Gold) Mabao 17

2022/23

Fiston Mayele (Yanga) & Saido Ntibazonkiza (Simba) Mabao 17

2023/24

Stephane Aziz KI (Yanga) Mabao 21

2024/25

Jean Charles Ahoua (Simba) Mabao 16


ORODHA YA WAFUNGAJI SASA

7 Fabrice Ngoy      (Namungo)- DR Congo

6 Saleh Karabaka   (JKT Tanzania)

5 Paul Peter (JKT Tanzania)

  Edgar Williams     (Dodoma Jiji)

4 Prince Dube        (Yanga)- Zimbabwe

  Mathew Momanyi (Pamba Jiji)- Kenya

3 Peter Lwasa       (Pamba Jiji)-  Uganda

  Jonathan Sowah  (Simba)- Ghana

  Feisal Salum        (Azam FC)

  Pacome Zouzou   (Yanga)- Ivory Coast

  Laurindo Dupe     (Yanga)- Angola

  Idd Seleman 'Nado'        (Azam FC)

  Daruwesh Saliboko (KMC)

  Seleman Mwalimu (Simba)

  Valentino Mashaka (JKT Tanzania)

  Shiza Kichuya      (Coastal Union)

  Fredrick Magata (Mtibwa Sugar)

  Cyprian Kipenye   (Namungo)

  George Mpole      (TZ Prisons)

2 Rushine de Reuck         (Simba)-Afrika Kusini

  Matheo Antony     (Mbeya City)

  Athuman Makambo(Coastal Union)

  Vitalis Mayanga    (Mbeya City)

  Mundhir Vuai       (Mashujaa)

  Maxi Nzengeli       (Yanga)- DR Congo

  Andy Boyeli          (Yanga)- DR Congo

 Maabad Maulid      (Coastal Union)

  Clatous Chama    (Singida BS)- Zambia

Yassin Mgaza         (Dodoma Jiji)

  Japhte Kitambala           (Azam FC)- DR Congo

 Mudathir Yahya     (Yanga)

 Joseph Akandwanaho (TRA United)- Uganda

  Ismail Mhesa       (Mtibwa Sugar)

  Eliud Ambokile     (Mbeya City)

   Shassiri Nahimana (Pamba Jiji)-  Rwanda

  Adilly Buha           (Mbeya City)

  Said Mkopi (Mtibwa Sugar)  

  Cleophas Mkandala (Coastal Union)

  Baraka Msimu      (Coastal Union)

  Libasse Gueye     (Simba)- Senegal

  Faraji Kayanda     (Dodoma Jiji)

  Jaffar Kibaya       (Mashujaa)

 Oscar Mwajanga   (TZ Prisons)