Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NGASSA: Fundi aliyeanzisha mwendo Chan

NGASSA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi ya kundi dhidi ya Ivory Coast, Ngassa aliifungia Stars bao wakimaliza mechi kwa sare ya bao 1–1. Tanzania haikuweza kutinga makundi na safari yake iliishia hapo.

UKITAJA majina ya mastaa waliowahi kuichezea timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Ligi Kuu Bara kwa mafanikio huwezi kumuacha Mrisho Ngassa ambaye alishiriki katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwa mara ya kwanza 2009 akiichezea Taifa Stars.

Katika mechi ya kundi dhidi ya Ivory Coast, Ngassa aliifungia Stars bao wakimaliza mechi kwa sare ya bao 1–1. Tanzania haikuweza kutinga makundi na safari yake iliishia hapo.

Unapolitaja jina la Ngassa kwenye mashindano ya Afrika takwimu zake uwanjani zitakupa jibu kuwa alikuwa staa wa aina gani.

Hapa Tanzania unaposikia fainali za CHAN zinazoendelea nchini, basi huyu ndiye Mtanzania wa kwanza kufunga bao tangu Stars ianze kushiriki.


CHAN YA KWANZA

Ngassa ana rekodi ya kucheza mechi za kwanza CHAN na anaeleza maandalizi yalivyokuwa wakati huo akikumbuka sapoti kubwa waliyopewa na TFF na serikali.

“Wakati huo ilikuwa nzuri kwa sababu tulijiandaa. Licha ya kwamba tulicheza mbali na nyumbani ila bado mwamko ulikuwa mkubwa na mashabiki walionyesha ushirikiano uliotufanya tujiamini zaidi,” anasema.

NGASS 01

TOFAUTI ILIPO

Ngassa anasema ofauti ya miaka ya nyuma na sasa ni mwamko, lakini mashindano ni yaleyale ila mashabiki wa siku hizi wanauelewa zaidi wa mpira wa miguu jambo lililopunguza lawama kwa wachezaji.

“Kipindi hicho mpira ulikuwa hauna mwamko mkubwa kama ilivyo sasa. Hata ukiangalia Rais Samia Suluhu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mashindano yanakuwa na uzito,” anasema.

“Mapenzi ya mpira kwa mashabiki sasa yamekuwa makubwa hata elimu sio kama ya wakati wetu ule... mtu alikuwa anataka ushindi tu ila unaona hata mkipoteza lawama hazipo kwa ukubwa.

“Kwa hiyo ni kitu kizuri ambacho kinafurahisha, lakini pia kinawapa morali wachezaji kucheza kwa ubora wa hali ya juu na hata wakipoteza huoni mashabiki wakiwaponda, ila wanaelewa ni mchezo ambao unaamuliwa na viwango.”


KILICHOWABEBA

Ngassa anasema kuwa mashindano hayo wakati yanaanza yalikuwa mageni na licha ya Stars kutofika mbali lakini yapo mambo ambayo yaliwabeba na kuwafanya waweke rekodi ya kucheza mara mbili.

“Viongozi wa TFF na serikali walikuwa karibu sana na sisi ingawa hatukufikia malengo ya kutinga fainali. Kwetu ilituumiza ila tuliamini ipo siku nafasi itapatikana ya kurudi tena kwenye hii michuano na kufanya makubwa Mungu amesaidia tena sasa tunacheza kwetu na ninaamini tutafika mbali.”

NGASS 02

FAIDA KWA STARS

Mongwe huyo anasema wakati ambao Stars ikicheza mechi ya kwanza ya ufunguzi jana dhidi ya Burkina Faso kuna faida ambazo Watanzania iwapo watazitumia vyema watanufaika na mashindano. “Ujue unapocheza uwanja wa nyumbani kwanza kujiamini kunaongezekaasikwambie mtu, ugenini hapajawahi kuzoweleka kwa sababu wote hampafahamu kila kitu kwenu ni kipya.

“Hakuna changamoto kubwa kama ya kiwanja kipya, jambo ambalo Stars haikutani nalo kwa sasa ndio maana mpinzani yeyote ukimfunga kwao uwezekano wa kumpiga kwako ni mkubwa kwa sababu unapajua,” anasema.


KIKOSI BORA

Akiuzungumzia kikosi cha Stars, Ngassa anasema: “Kikosi chetu ni bora. Mpaka sasa tumeshajua ushindi una raha gani. Kwangu nikipewa nafasi ya kupanga kikosi basi itakuwa kazi ngumu kwa sababu wachezaji wote ni bora, lakini bahati mbaya au nzuri wanatakiwa waanze wachezaji 11.”


CAF SIO TFF

Mchezaji huyo anagusia pia ushiriki wake katika mambo kadhaa yanayohusiana na CAF akisema: “Muda mwingi ni kweli naonekana huko hata juzi tu nimetoka, lakini ni mipango ya Mwenyezi Mungu tu. Pia rekodi ambazo zipo ndizo zinaendelea kunibeba.

“Mimi sio bora sana kuzidi wenzangu na tupo wengi ila bahati tu imedondokea kwangu na kukaa vizuri na TFF ambayo inatambua mchango wangu nilioutoa kwenye timu ya Taifa.”

NGASS 03

REKODI NOMA

Ngassa ndiye mchezaji pekee ambaye mpaka sasa ana rekodi ya kufunga mabao mengi katika timu ya Taifa akiwa nayo 25, huku kwa sasa anayepambana kuifikia ni Saimon Msuva mwenye 23.

“Ujue rekodi inaweza kuvunjwa kwani mimi niliwezaje kufunga hayo mabao? Kwa hiyo kila mchezaji mwenye malengo anaweza kufika hapo hata Msuva anasogea yuko karibu.

“Msuva akifika au mwingine yeyote ni jambo jema ila furaha yangu itakuwa kubwa kama atatokea atakayeipita, ni heshima kwake na kwa Taifa..Tanzania tutakuwa juu na naamini muda si mrefu litatimia,” anasema.


USHAURI STARS

Mchezaji huyo anawashauri wachezaji wa Stars akisema: “Wajitume sisi Watanzania tuko nyuma yao na tunawategemea wao kwa sababu wanaingia uwanjani kutuwakilisha wao ingawa Taifa lina wachezaji wengi.

“Kwanza watoe wasiwasi wako nyumbani hiyo ni faida. Lakini, tunaweza kuweka mguu sawa na wakalitoa Taifa kimasomaso katika michuano hii muhimu. Wakiweka nguvu sawa wachezaji wote ni wazuri ndio maana wamechaguliwa, hivyo waondoe papara wajiamini kwamba wanaweza na watafanya makubwa.”


MTAANI KUKOJE

Wakati hamasa zikiendelea, Ngassa anasema watu wamekuwa na mwamko kutokana na matangazo kwenye runinga na mitandao ya kijamii.

“Ujue wakati wetu ilikuwa ngumu kuwa na hamasa kama ya sasa kwa sababu kila mtu anaangalia televisheni na mitandao ya kijamii ambako huko taarifa zote zipo. Hivyo mwamko ni mkubwa na tutegemee mashabiki kujaa uwanjani, lakini walio mbali kufuatilia mechi kwani upatikanaji wa taarifa ni mwepesi.

“Kwa walio mjini natamani waje (uwanjani) asiwepo wa kubaki nyumbani labda wale ambao sio mashabiki wa mpira wa miguu ila wana kitu cha kujifunza na hasa kipindi hiki cha usajili wanaosemwa ndio wako kwenye timu ya Stars.”

NGASS 04

ISHU YA USAJILI

Ngassa pia aligusia masuala la usajili akisema ni suala jingine ambalo linalolipaisha soka la Tanzania, “nafahamu soka la Bongo wakati wa usajili na mechi za dabi na kimataifa ndio muda ambao masikio ya watu muda mwingi yanakuwa huko na wanataka kujua nani anaenda wapi.

“Lakini kiukweli kabisa sijafuatilia suala lolote la usajili kati ya hizi timu kubwa tatu ambazo ni Simba, Yanga na Azam FC ingawa nafahamu kuwa ni lazima watasajili wachezaji wa ndani na nje. Nilikuwa katika mambo ya CAF ndio maana haya yamenipita kidogo.”


BENO NGASSA

Ngassa hivi sasa ana mdogo wake aitwaye Beno ambaye anacheza nafasi kama ya kaka yake akikipiga winga na msimu uliopita aliumaliza akiwa na kikosi cha Tanzania Prisons.

“Ni mchezaji mzuri anacheza kwa kiwango bora simsifii kwa sababu ni mdogo wangu ila anachokifanya kinaonekana ndio maana kapata ofa kutoka Dodoma Jiji imemsajili na kumpa mkataba wa miaka miwili.

“Huwa nazungumza naye kama kaka na kila mechi lazima tuzungumze kabla ya kwenda uwanjani, kwa sababu nampa mbinu za kukabiliana na wapinzani na anazifanyia kazi.”


MRITHI WAKE

Mojawapo kati ya wachezaji waliowahi kuzisumbua Simba na Yanga ni Ngassa na hapa analiambia Mwanaspoti kuwa warithi wake ni wengi, ila bado hawajafahamika kwa ukubwa kama aliokuwa nao.

“Warithi wapo wengi Tanzania kwa sababu wote wanacheza vizuri ukiangalia Nkane (Denis)anafanya vizuri Beno pia ana usongo wa kucheza Taifa Stars.

“Ni suala la muda nadhani wapo mawinga wenye viwango bora na hadhi hata kunizidi ila tu hawajapata nafasi ya kuonekana katika timu kubwa au za Taifa na mashabiki wakawafahamu,” anasema.

Mkongwe huyo pia aliwazungumzia wazawa akisema  wanaposajiliwa timu kubwa halafu wanaanza kushuka viwango sio kwamba wanajisahau bali ni upatikanaji wa nafasi unakuwa mgumu kwao.

“Unaona mtu kama Nkane, Mkude (Jonas) na Sure Boy wamekuwa wakifanya vyema kila wanapopata namba.

“Timu ndogo unaona wazawa wengi wanacheza kwa sababu hawana wageni wengi, ila hizi kubwa unaona kabisa kipaumbele kipo kwa hao wa nchi zingine.”