Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

New Stone ilivyofeli Ligi Kuu Zanzibar

STONE Pict

Muktasari:

  • Safari hiyo ya kilomita 34 kutoka ChakeChake hadi Konde ambayo inatumia takribani saa mbili kufika kutokana na hali ya barabara, hatimaye saa 3:10 asubuhi mwandishi wa Mwanaspoti inawasili eneo hilo na kukutana na wenyeji wake.

ILIKUWA ni saa 12:30 asubuhi, wakati ambao wananchi wa Kisiwa cha Pemba wakiendelea harakati za maisha za kujitafutia kipato, ndipo mwandishi wa Mwanaspoti anaanza safari ya kukitafuta Kijiji cha Konde kilichopo Wilaya ya Michewen  Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwenye Makao Makuu ya New Stone Town iliyodumu Ligi Kuu Zanzibar kwa msimu mmoja pekee na hatimaye kushuka daraja.

Safari hiyo ya kilomita 34 kutoka ChakeChake hadi Konde ambayo inatumia takribani saa mbili kufika kutokana na hali ya barabara, hatimaye saa 3:10 asubuhi mwandishi wa Mwanaspoti inawasili eneo hilo na kukutana na wenyeji wake.

Dhumuni la safari hiyo ni kuzungumza na viongozi wa New Stone kupata kiundani kilichowasibu baada ya kushiriki Ligi Kuu Zanzibar msimu huu 2025-2026 kwa mara ya kwanza na kujikuta wakishuka kutokana na hivi sasa timu hiyo ina pointi sita baada ya kucheza mechi 24, zimebaki mechi sita kukamilisha msimu ambapo hata ikishinda zote, haiwezi kutoka nafasi nne za chini kwenye msimamo.

STON 02

TIMU KUFANYA VIBAYA

Katika mazungumzo na viongozi wa New Stone Town, wamesema sababu kubwa ya kudumu kwa msimu mmoja pekee ndani ya Ligi Kuu Zanzibar ni ugeni waliokuwa nao.

Mbali na hilo, ukata wa fedha za uendeshaji wa timu nayo ni changamoto iliyochangia kufeli kwao huku wakieleza asilimia kubwa timu kutoka kisiwani Pemba hazina udhamini mbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo. Ofisa Habari wa New Stone, Saidi Ayoub Kijazi, anasema timu haikuwa na uzoefu wa ligi hiyo licha ya kufanya vizuri Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Pemba na kupanda daraja.

Anasema timu iliibeba dhana hiyo ya kuwa itafanya vizuri na kuhimili mikiki ya ligi kuu kama ilivyofanya Ligi Daraja la Kwanza, lakini mambo yakaenda tofauti na matarajio.

“Huku tulipotoka tulifanya vizuri, tukafikiria kwamba na Ligi Kuu itakuwa hivyohivyo, kumbe huku kuna mabadiliko makubwa, tukajikuta tunaambulia kipigo hadi tulifokia mechi 23 tulikuwa na pointi tatu tu,” anasema kwa masikitiko.

Kati ya mechi 24 ilizocheza timu hiyo, imeshinda mbili dhidi ya Zimamato na Junguni, huku ikipoteza 22, ikiruhusu mabao 68 na kufunga 18. Kwa maana hiyo, haina nafasi ya kubaki ligi kuu hata ikishinda mechi zilizobaki.

Kijazi anasema, awali walikuwa na matarajio makubwa ya timu kufika mbali lakini changamoto ya ugeni ndio sababu ya kushindwa kufikia lengo hilo.

“Uzoefu umechangia kwa kiasi kikubwa timu kupata matokeo mabaya na kushuka daraja, hivyo kwasasa hatuna uwezo wa kubaki ligi Kuu,” anasema.

Anasema, awali mikakati yao ilikuwa mizuri baada kufungwa mechi tatu za mwanzo hapo ndipo walipopoteza matumaini.

Kwa vipigo hivyo, na idadi ya mechi zilizosalia anasema tayari timu hiyo imeshashuka daraja na watajipanga wakati mwingine.

Si hayo tu, anasema maandalizi ya kuanza msimu yalikuwa dhaifu kwa timu kutokuwa na fedha na wachezaji waliopatikana hawakuwa na kiwango kilichokidhi mahitaji ya ligi.

STON 03

RASILIMALI FEDHA PASUA KICHWA

Miongoni mwa kilio kikubwa cha timu hiyo ni fedha, ambapo Kijazi anasema timu ingekuwa na udhamini wa kutosha wanaamini isingefanya vibaya wala kushuka.

Anasema, endapo timu zote zilizopanda daraja zikipata udhamini mzuri zina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye ligi na kunusurika kushuka daraja kwa sababu timu itakuwa na wachezaji wenye viwango.

Anasema, kila jitihada inaongozwa na fedha na sio maneno kwa maana hiyo viongozi walifanya jitihada mbalimbali ila huwezi kutoa maneno matupu bila ya fedha kwani wachezaji wanataka mahitaji yao.

Anasema, uongozi imara unasimama kwakuwa na fedha kwani zitatoa mahitaji ya wachezaji kwa ufanisi.

STON 04

KUFELI USAJILI

Kijazi anasema wachezaji waliosajiliwa hawakuwa na viwango vya kucheza Ligi Kuu Zanzbar, baadaye ikalazimika kuwaacha na kutafuta wengine.

Anasema, usajili uliofanywa dirisha dogo ulikuwa mzuri zaidi lakini ilikuwa tayari wamec helewa akiamini kwamba kama wangepatikana mwanzo uhakika wa kubaki ligi kuu ungekuwepo.

Hata hivyo, anaeleza kwamba, timu nyingi zinazotokea kisiwani Pemba hazina mashabiki kwani ushindani wa timu hizo ni mdogo.


TATU ZILIZOIPOTEZA

Anasema, kitendo cha kupoteza mechi tatu dhidi ya Mlandege, Chipukizi na Polisi, kilivuruga kwa kiasi kikubwa hesabu zao na kuanzia hapo, hali ikawa mbaya zaidi. Kijazi anasema timu hiyo ilikuwa na uwezo mkubwa wa kushinda mechi hizo, lakini ilipotokea kinyume chake hali ikawa mbaya zaidi.

Anasema wamejifunza kuwa maandalizi ya kwanza ndio yanayoleta matokeo mazuri na kuanza kujinusuru kushuka daraja.

Hivyo, anasema timu hiyo inarudi kujipanga kurejea Ligi Kuu kwa kutafuta wachezaji wenye viwango vya kuipambania timu.

STON 01

MAANDALIZI LIGI DARAJA LA KWANZA

Anasema shughuli ya timu hiyo inaanza mapema kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Pemba msimu ujao na wana uhakika wa kurudi Ligi Kuu Zanzibar.

Kijazi anasema wakipata nafasi ya kurudi tena watajiandaa kuepuka aibu hiyo kwani wameshatambua namna ya ligi hiyo inavyoendeshwa.

Anaongezea, hawataki kupita njia ambayo waliipita msimu huu, hivyo watabadilisha kwa kuepuka kipigo cha paka mwizi.


WITO

Kijazi anatoa wito kwa mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Zanzibar kuongeza fedha timu zinazoshiriki ligi hiyo ili kupambana vizuri.

Anasema, wachezaji wa Zanzibar wakipata nafasi ya kuchukuliwa kwenye timu za Tanzania Bara na kukaa benchi wanaridhika kutokana na masilahi yanayopatikana.

Hivyo, ameliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kuongeza udhamini wa ligi hiyo ili kuwa bora zaidi.


SAFARI YA NEW STONE

Akitoa historia fupi ya jina hilo, muanzilishi wa timu hiyo, Mohamed Said ‘Sona’ anasema timu hiyo ilianzia maskani baada ya kuwepo vijana kumi wanaojua mpira akiwemo yeye na hapo ndipo waliapoamua kuanzisha timu.

Anaeleza kuwa, awali timu hiyo waliipa jina la Stone Town kwani ndio ambalo lilikubalika zaidi mtaani hapo na kufanya vizuri.

Anasema, katika miaka kadhaa timu hiyo iliyumba na kushuka Ligi Daraja la Pili ikatokea timu ya New Star ambayo ilikuwa wenyewe imewashinda na kuichukua, hapo ndipo walipoibadilisha jina na kuita New Stone Town.

Sona anasema, waanzilishi wa timu hiyo walikuwa wakitafuta wachezaji na kuwalipa wenyewe kuanzia mshahara, chakula na nauli.

“Timu ilipanda daraja baada ya kuikatia rufaa timu ya Wawi Star waliochezesha wachezaji wageni waliosajiliwa kuwa Wazanzibar, hapo tulianza kufuatilia na kupata ushahidi wa kutosha ndio ikafikia hapo,” anasema.