Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MTU WA MPIRA: Skudu, Konkoni dah!

Yanga imefanya usajili mzuri msimu huu. Iko wazi. Wachezaji kama Yao Kouassi, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Nickson Kibabage ni wachezaji mahiri. Lazima tuwapongeze kwa sasa.

Lakini tumesahau kubwa katika usajili wa Yanga, nyota aliyepewa jina kubwa alikuwa Skudu Makudubela. Huyu walimtoa Marumo Gallants ya pale Afrika Kusini.

Usajili wake uliwalaza watu usiku wa manane. Watu wa Yanga walimsifia kama nyota ambaye hajawahi kutokea. Akapewa na jezi namba sita iliyokuwa ikivaliwa na Feisal Salum.

Nini kimetokea baada ya hapo? Pale Algeria juzi Ijumaa nilimuona Skudu akiwa jukwaani kama mtazamaji. Ni kama vile ambavyo imekuwa katika mechi nyingi za ligi.

Mchezaji aliyesajiliwa kwa kelele nyingi, ameshindwa kuingia katika kikosi cha kwanza cha Yanga. Ameshindwa kuingia katika wachezaji muhimu kwenye timu wanaoingia kutokea benchi kwenda kubadilisha matokeo.

Pengine sifa kubwa alizopewa Skudu wakati anasajiliwa zimemmaliza mapema.

Matarajio yakawa makubwa kuliko uwezo wake. Uwanjani, namba zinamkataa.

Hata katika mechi ambazo Yanga walifanya vizuri sana, alipoingia hakuwa na madhara makubwa. Hakuongeza kitu kikubwa sana.

Vipi kuhusu Hafidh Konkon. Sijui Yanga walimtoa wapi huyu mchezaji. Ni mzito kama anacheza akiwa ameweka vitu mfukoni. Hanyumbuliki.

Hakai kwenye nafasi sahihi. Hana kasi. Hapigi pasi nzuri. Yaani ni kama mchezaji wa timu ndogo aliyefika timu kubwa kwa bahati mbaya.