Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshahara wa Aziz KI ulimkimbiza bosi Simba

KOCHA Sebastian Mkoma alidumu ndani ya Yanga Princess kwa miezi minne na kutimuliwa baada ya timu hiyo kutokuwa na matokeo mazuri kwenye Ligi ya Wanawake Tanzania (WPL).

Tangu hapo ambapo ilikuwa ni Machi mwaka huu, Mkoma hajasikika kuwa na timu nyingine. Ukimya wake ndiyo ulioivuta Mwanaspoti imtafute na kufanya naye mahojiano.

Katika mahojiano hayo, Mkoma anaeleza mambo mengi katika soka kwa ujumla kwani amewahi kufundisha hata timu za wanaume zilizowahi kucheza Ligi Kuu Bara miaka ya nyuma kama Polisi Moro. Na haya ndiyo mahojiano yetu;


HATAKI TENA TIMU ZA WANAWAKE

“Kwa sasa sifikiri kurudi kufundisha timu za wanawake kwa maana ya soka la wanawake, nilichokifanya huko kinatosha ni muda wa makocha vijana sasa kuendeleza pale nilipoishia, nimefanya mengi kwa kweli.

“Tangu niachane na Yanga Princess najishughulisha na mambo ya kituo changu cha soka la vijana kwa wasichana na wavulana kilichopo Tabata-Segerea kinaitwa Wakala Msomi. Hiki ni kituo changu mwenyewe nilikianzisha miaka ya nyuma na kimezalisha vijana wengi wanaocheza ligi za mikoa, First League na Championship.

“Nawaza kufundisha timu za wanaume hasa Championship ikitokea timu ya Ligi Kuu nitashukuru pia, kuhusu JKT Queens haikuwa rasmi kama ilivyokuwa Simba Queens walivyosema nataka kurudi.

“Wakala Msomi kimetoa wachezaji 15 wa kike kucheza timu mbalimbali. Kwasasa siwauzi ila nataka wacheze wapate uzoefu. Muda wa kuwauza bado, nimesoma ukocha kufundisha jamii, jamii inaingia sehemu zote wanawake na wanaume,” anasema na kuongeza;

“Niliifundisha ile Serengeti Boys ya Gabon, niliitengeneza mimi na baadaye nikahamia timu ya taifa ya wanawake iliyokuwa inaenda kucheza michuano ya CECAFA timu haikuwa na kocha.”


UTAWALA NA UFUNDI

“Kitengo cha ufundi kinachoangalia vijana nadhani hakipati sapoti ya kutosha ama hakina weledi, tumeandaa AFCON 2019 ya U17 hapa je, wale vijana kuna anayeonekana hadi muda huu?

“Hebu angalia hadi sasa ile Serengeti Boys ya Gabon vijana gani tena wamezalishwa, maana naona ni wale wale wanaocheza ligi waliotoka Serengeti Boys ya Gabon kina Kibwana Shomari, Dickson Job, Kabwili nini kimetokea hapo kati.

“Inawezekana kwenye Utalawa na Ufundi hakuna mawasiliano mazuri, kama ufundi hawana cha kuwapelekea watawala basi utawala hakuna watakachokifanya.

“Mchezaji amekaa hajui cha kufanya anatakiwa asaidiwe, inashindikanaje kutengeneza ‘cream’ nzuri ya vijana ya nchi.

“Sioni kama kuna watu wanafuatilia hata ligi daraja la tatu wanacheza wenye umri wao cha kushangaza wanaocheza ni wale walioshuka kutoka Ligi Kuu.

“Huku nyuma tulikuwa na mwendelezo mzuri, TFF kila mwaka inakuwa na timu mpya yaani vijana wanapatikana lakini baada ya hapo wanapokewa na nani? Mtibwa Sugar ndio wenye mwendelezo mzuri kila mwaka kwasababu wana uwezo wa kuibua na kukaa na watoto.”

“Kamati ya Ufundi iwe na mtu maalumu wa kuwafuatilia hawa vijana wanakokwenda kucheza maana wanaishia kupotea tu.”


SIMBA, YANGA WAO MBELE TU

“Simba, Yanga zenyewe malengo yao ni makubwa wanataka mafanikio, hawawezi kupandisha vijana wengi na kuwapa nafasi ya kucheza ndio maana unaona timu zao za vijana hazina nguvu.

“Makocha wa hizi timu sasa hivi wana shinikizo la kufanya vizuri michuano ya CAF, akikuta kuna gepu anasema niletewe mchezaji kutoka nchi fulani mwenye uwezo wa kumpa matokeo mazuri sio kumvumilia apate uzeofu.

“Kwa mfano hivi sasa kocha wa Yanga amepoteza kombe la kwanza, hapo presha tayari na malengo ya kutumia vijana ndio yamepotea kabisa. Niliwaona vijana wa Mtibwa wamecheza mechi vizuri tu ya Simba, kwasababu wanafuatilia watoto.

“Hawa makocha wa Simba na Yanga sidhani kama mmoja atafika Krismas ama Nyerere Day, wanaishi kwenye presha kubwa sana, wamepewa majukumu magumu.”

“Nilipopewa Yanga Princess nilizungumza wazi kuwa hatuwezi kuchukuwa ubingwa, unapoteza pointi tano unategemea kuzitoa kutoka kwa nani upewe wewe, ni kuwadanganya mashabiki kuwa tunachukuwa ubingwa wakati kitu hakiwezekani.

“Hiyo kauli yangu ilileta shida, maana watu hawapendi kuambiwa ukweli, hata leo hii Simba ikifungwa mechi moja, Yanga naye akapoteza moja unadhani watapoteza kwa nani mwingine ili mwingine achukuwe ubingwa?

“Mashinikizo kama haya yanatakiwa kutengenezewa menejimenti ya kutengeneza timu ya kudumu kuanzia timu za vijana, Simba pale ameondoka Joash Onyango amekuja Che Malone mtu ambaye ameingia kikosini moja kwa moja, Yanga ametoka Yanick Bangala kaletwa Pacome Zouzoua na wote ni wa gharama.

“Leo hii kocha apoteze mechi hata mbili ambazo zitawaondoa kwenye mbio za ubingwa unabakije ndani ya Simba na Yanga, mpira wetu umekuwa mgumu.”


NI VIBE, PESA

Hivi karibuni imetangazwa kuwa Ligi Kuu Bara imeshika nafasi ya tano kwa ubora Afrika, Mkomwa anafafanua;

“Tunasema ligi yetu ni bora kwa Afrika kwa lipi? Ubora umepimwa kwa lipi? Kama ni kwa vibe na ufadhili hapo sawa, maana siku hizi kwenye klabu kuna ufadhili na TFF nao wanajitahidi kusaka ufadhili lakini kwa ubora wa kiufundi uwanjani bado. Tumewekeza kwenye pesa ila hatujatengeneza ligi nzuri.

Ukija upande wa ratiba, kwa Afrika sio tatizo maana kalenda ya CAF ikichelewa kutoka basi hata ratiba huchelewa pia kwa Ulaya kila kitu kinatolewa mapema tu lakini hapa kwetu hata kalenda ya CAF ikitoka bado kuna shida.

“Inaonekana kabisa kuna shida kwenye menejimenti, baada ya kalenda ya CAF kutoka, je wenye ligi walikaa na watu sahihi kupanga hiyo ratiba, mechi mbili au tatu zinachezwa kunakuwa na mapumziko ya siku kama 20.

“Ratiba haijakaa vizuri, mfano Simba hawana mechi kwasasa ya ligi ukiachana na hiyo ya CAF kiufundi watapoteza mechi fitinesi, unapokuja kiutawala angalia Kagera Sugar waliweka kambi Morogoro, wakaenda kucheza mechi Kigoma, imeenda Ihefu halafu anarudi nyumbani kucheza mechi moja.

“Hivi waliokuwa wanapanga ratiba wanafahamu jiografia ya nchi ilivyo? Kiufundi Kagera kufikia mechi ya nne wachezaji watakuwa wameshachoka.

“Coastal Union wamecheza mechi mbili unaambiwa wanapumzika siku 14, wanakuja Simba kuomba wachezaji wanakatiliwa kwa madai kuwa wametawanyika, inawezekana wamevunja kambi kutokana na uchumi mdogo, ama watu hawajatatua matatizo yao kama Kitayosce.”


MZAMIRU, KIBWANA MMH

“Kiufundi timu ya taifa tunasema atacheza mchezaji mzalendo leo hii mfano kama Mzamiru Yassin unamleta mchezaji wa kigeni, pale yupo Kanoute na Fabrice Ngoma, mzawa anakosa nafasi ya kucheza, kuna Kibwana ameletewa Kouassi Yao ameingia kwenye vita nyingine kubwa, Stars ya sasa huwezi kuwaacha Bakari Mwamnyeto, Job na Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ wote wana vita ndani ya timu yao, wanakosa mwendelezo mzuri wa kucheza, ubora wao utatoka wapi na viongozi wamekaa kimya.

“Zamani ilikuwa wachezaji wa kigeni watano, watatu wanacheza wawili wanakaa nje sasa hivi 12 ambayo ni timu nzima, halafu mtu anakwambia anaongoza mpira wakati timu ya taifa inapoteza ubora, mpira unataka ukuletee sifa kwa kulinda vipaji vya wachezaji wako.

“Sikubaliani na haya madai ya kwamba wazawa wanabweteka, kama viongozi wamefanya amefanya semina gani kwa wachezaji wazawa, wazungumze nao na wawape majukumu ya kuibeba nchi naamini wanaweza.

“Naamini wanaokuja kutoka Magharibi wanafuata vibe na pesa na hawataki kwenda Ulaya. Mfano mwingine kipa Ally Salim anayekuja vizuri sasa na tutegemee baadaye kuwa na msaada kwenye taifa ameletewa mtu, mnadhani akipona Aishi Manula yeye atakuwa kipa wa ngapi.

“Manula akirudi anakuwa wa pili wakati anaendelea kuwa sawa, Salim wa tatu huyo mwingine Hussein Abel atakuwa jukwaani anazidi kushuka kiwango, mnategemea tunatengeneza nini. Kwa umri wa Ally na Abel sio tena wachezaji wanaoweza kucheza U20 wanakwenda wapi baada ya hapo.


AACHIWA MEZA SIMBA

Msimu uliopita akiwa Simba Queens na wakati huo ameongezwa kwenye benchi la ufundi la timu ya wanaume ilipoenda kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa nchini Malawi dhidi ya Big Bullets, waliporudi alikutana na bosi wa Simba, kilichotokea anasimulia;

“Nakumbuka tulikutana na CEO wa wakati huo kujadili namna ya kuboresha kikosi ili kufika nusu fainali, pendekezo la kwanza lilikuwa ni Victorien Adebayor ambaye ofa yake ilikuja mezani ya Dola 400,000 na mshahara kwa mwezi Sh50 milioni, kukawa na dili la Azizi Ki kwa Dola 200,000 na mshahara wa Sh24 milioni kwa mwezi.

“Aisee bosi aliniacha meza kisa hana bajeti hiyo, nilienda kwa mwenyekiti naye alisema hana bajeti na hapo ilitakiwa wachezaji hata saba wa maana hao wawili wasingetosha, mambo yakaishia hapo Azizi Ki akaenda Yanga.”


SIMBA QUEENS

“Najivunia Simba Queens ni kutimiza malengo ya kuchukuwa ubingwa na kufanya vizuri CECAFA, pia wachezaji mikataba yao inaboreshwa, niliondoka mchezaji aliyekuwa akipata mshahara mdogo ilikuwa ni Sh 500,000 lakini wakati nafiki nilikuwa mishahara hadi ya Sh300,000 na mshahara wa juu ilikuwa Sh700,000.

“Niliwabadilisha wachezaji waishi maisha yenye hadhi ya Klabu ya Simba, niliwaambia kila mmoja anunue simu nzuri na kweli walifanya hivyo, niliwafundisha namna ya kutunza pesa zao kwa kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima maana kila kitu kilipatikana ndani ya Simba hadi bonasi zilitolewa.

“Nilifanikiwa kuwarejesha kikosini wachezaji watano muhimu waliokuwa wameondoka baada ya kushindwa kuelewana na mabosi akiwemo Opah Clement.”


VYETI, MKATABA

2017 alipata cheti cha CAF Leseni A ambacho kilimruhusu kusimama kama kocha mkuu kwenye michuano yote ya Ligi Kuu Bara pamoja na michuano ya kimataifa.

Mwaka huu akiwa na makocha wengine ambao walisoma wote kwa mwaka huo walipata ‘reflesher course’ ya vyeti vyao pamoja na Juma Mgunda ambaye pia awali alidaiwa hakuwa na vyeti.

“Mimi na Mgunda, Wilfred Kidao, Malale Hamsini, Mecky Mexime tumesoma darasa moja hadi Simba wananichukua nilikuwa nimeishalipia Sh300,000 kilichotokea kwa Mgunda cheti chake kilikuwa hakijaingizwa kwenye mfumo.

“Ndio maana niende Malawi na Angola. Nilienda kufanya kazi yangu ningepewaje timu za taifa wakati sina vyeti? Sema hizi timu kubwa zikiamua kukuchafua unachafuka kweli.

“Wakati Simba Queens wanaenda Morocco, Mohamed Dewji aliniambia niende huko tukazungumze juu ya mkataba wangu maana ulikuwa umeisha, niligoma naendaje Morocco wakati ofisi za klabu zipo hapa?