Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mitindo iliyopitwa na wakati lakini bado inavaliwa sana

Muktasari:

  • Fasheni imebadilika lakini bado kuna mitindo ambayo imepitwa na wakati na watu wameikumbatia kama sheria. Hizi ni baadhi ya fashion mistakes zinazojirudia kila siku mitaani huku wenyewe wakiamini bado wanapendeza.

Kuna watu ukikutana nao mtaani unajiuliza wana kioo nyumbani au wanavaa kwa kumbukumbu za miaka ya nyuma. Suruali imebana hadi mifuko imechoka, rangi zimepigana kama timu mbili uwanjani halafu juu wamejaza hereni, miwani na mikufu kana kwamba ni maonyesho ya vifaa.

Fasheni imebadilika lakini bado kuna mitindo ambayo imepitwa na wakati na watu wameikumbatia kama sheria. Hizi ni baadhi ya fashion mistakes zinazojirudia kila siku mitaani huku wenyewe wakiamini bado wanapendeza.

Wataalamu wa mitindo mara nyingi husisitiza kuwa kuvaa vizuri si lazima kuiga kila kinachoonekana kwenye mitandao ya kijamii, bali ni kuchagua kile kinachoendana na mwili, mazingira na wakati uliopo. Hata hivyo, baadhi ya watu bado wameendelea kushikilia mitindo ambayo ilishapoteza umaarufu wake.


MAKOSA YANAANZAGA HAPA

Moja ya makosa yanayoonekana sana ni kuvaa nguo zisizoendana na mwili. Kuna watu wanaovaa suruali, mashati au magauni makubwa kupita kiasi wakiamini kuwa ndio mtindo, lakini mara nyingi huondoa mvuto wa muonekano. Mavazi makubwa yalikuwa maarufu sana miaka iliyopita, hasa kwenye mitindo ya hip hop, lakini sasa yanahitaji kuchaguliwa kwa umakini ili yaonekane ya kisasa.

RANGI SASA

Pia kuna suala la kuchanganya rangi bila mpangilio. Zamani baadhi ya watu walipenda kuvaa rangi nyingi kwa wakati mmoja bila kuzingatia muonekano wa jumla. Leo mitindo mingi imeelekea kwenye mchanganyiko wa rangi unaoleta utulivu na mpangilio. Kuvaa rangi nyingi sana kunaweza kufanya mtu aonekane kama amechanganya mitindo tofauti bila mpango.

Kwa upande wa wanawake, moja ya makosa ya kimitindo yanayoendelea kuonekana ni kutumia mapambo mengi kupita kiasi. Wakati mwingine vipodozi, hereni, mikufu na mavazi mazito vikichanganywa vinaweza kupunguza uzuri wa mtu badala ya kuuongeza. Mtindo wa sasa unaelekea zaidi kwenye muonekano rahisi lakini wenye ubora.

Kwa wanaume, baadhi bado wanaendelea na mtindo wa kuvaa nguo zenye maandishi makubwa sana mbele au nyuma bila kuzingatia ubora wa vazi. Miaka iliyopita mashati yenye nembo kubwa na michoro mingi yalikuwa yakitawala, lakini sasa wengi wamehamia kwenye mavazi yenye muonekano safi na rahisi.


VIATU BALAA

Tatizo jingine ni kuvaa viatu ambavyo havilingani na mavazi. Kuna watu wanavaa aina fulani ya kiatu kwa sababu tu kimekuwa maarufu, bila kuangalia kama kinaendana na suruali au shati walilovaa. Wakati mwingine kiatu kizuri kinaweza kupoteza mvuto kama hakijawekwa kwenye muunganiko sahihi wa mavazi.

Mitindo ya zamani kama suruali zilizobana kupita kiasi pia bado inaonekana mitaani. Ingawa kulikuwa na kipindi ambapo jeans nyembamba sana zilikuwa gumzo, sasa mitindo mingi imeanza kurudi kwenye suruali zenye nafasi kidogo na zinazompa mtu uhuru wa kutembea.

MITINDO YA NYWELE

Kuna mitindo ya nywele ambayo zamani watu walikuwa wanachana au kusuka lakini sasa inerudi kivingine tena wengine wakitengeneza kama wigi lakini zamani iliitwa Bambucha au zile rasta za vitungu vinene au nywele za mkono zilizochorwa vizuri kichwani kama zigizaga.

Kwa sasa mitindo hiyo imegeuka na kuwa kama mipya hivi hasa kwa vijana wa mwaka 2000, lakini wazee wenzangu wanaelewa kuwa zamani mitindo hii waliibana sana.


USIIGE KILA KITU

Hata hivyo, si kila mtindo wa zamani ni mbaya. Baadhi ya mitindo hurudi baada ya miaka mingi ikiwa imeboreshwa. Mfano mavazi ya zamani yanaweza kuonekana ya kisasa ikiwa yamechanganywa na vitu vipya. Tofauti kubwa ipo kwenye namna mtu anavyoyatumia.

Wataalamu wa mitindo wanaamini kuwa kosa kubwa si kuvaa kitu kilichopita muda wake, bali ni kuvaa bila kuzingatia mazingira na mabadiliko ya wakati. Mtu anaweza kuwa na nguo chache lakini akawa na uwezo wa kuzichanganya vizuri na kuonekana mwenye mvuto.