Miaka tisa ya dhahabu kwa Mo Salah Liverpool
Muktasari:
- Licha ya mwenendo wake kuchanganya msimu huu, anaondoka akiwa ni mwamba wa hadhi ya juu katika klabu hiyo na mmoja wa magwiji wa enzi zake katika Ligi Kuu England (EPL).
LIVERPOOL, ENGLAND: “KAMA hujafanikiwa mwanzo, jaribu tena na tena.” Kauli hiyo maarufu imekuwa kiini cha taaluma ya Mohamed Salah na pia safari yake akiwa Liverpool. Salah atahitimisha kipindi chake cha miaka tisa yenye mafanikio makubwa Anfield mwishoni mwa msimu huu, baada ya kutangaza kwa mshangao juzi, Jumanne usiku, kwamba imetosha na sasa anasepa zake.
Licha ya mwenendo wake kuchanganya msimu huu, anaondoka akiwa ni mwamba wa hadhi ya juu katika klabu hiyo na mmoja wa magwiji wa enzi zake katika Ligi Kuu England (EPL).
Rekodi yake inazungumza yenyewe; makombe mawili ya EPL, mawili vya Carabao, moja FA na medali ya ubingwa wa Mabingwa Ulaya. Pia ametwaa tuzo nyingi binafsi na heshima mbalimbali. Ana rekodi ya kushinda mara tatu tuzo ya Mchezaji Bora wa Kulipwa England (PFA) na mabao 255 aliyoyafunga kwa Liverpool yamemsaidia kushinda mara nne taji la Golden Boot EPL.
Hayo yote hayakuonekana 2016 wakati kipindi cha huzuni cha Salah Chelsea kilipomalizika. Januari 2014 alipotua, Salah alionekana kama mchezaji wa kawaida Stamford Bridge alipoondoka akiwa na mabao mawili.
KAZINI ITALIA
Kujijenga kwake kulianza akiwa Chelsea, ingawa The Blues hakupata faida yoyote mpaka alipotimkia AS Roma ya Italia kwa mkopo kabla ya kununuliwa jumla ambako alionyesha uwezo wake halisi. Mwaka mmoja baada ya kuhamia London Magharibi, Fiorentina ilikubali kumkopa Salah kwa miezi 18 ukiwa na mkopo wa awali alipotoka England.
Kabla ya kuondoka Fiorentina na kutimkia England, Salah aliibuka na mabao muhimu ikiwemo ushindi wa Europa League dhidi ya Tottenham Hotspur na yale aliyozifunga Juventus na Inter Milan.
Salah hatimaye alipata upendo wa kiwango cha juu kinachostahili kipaji chake, lakini kwa mshangao alikataa kuhamia Fiorentina moja kwa moja na baadaye akavunja mkopo huo kujiunga na AS Roma.
Labda, Fiorentina walikosa nafasi ya kummiliki Salah kutokana na mshauri wake wa zamani, Micah Richards, aliyesema: “Kwa kweli kuna mahojiano ambapo nasema mchezaji huyu ni bora sana kwa Fiorentina, hatupaswi kummiliki. Alikuja kwa mkopo na nilijua ni mchezaji wa kipekee. Kugusa kwake mipira, mbinu zake na jinsi alivyokuwa mnyenyekevu tu mbele ya goli ni vitu vya kipekee.
“Tulipokwenda Juventus katika Coppa Italia alikimbia futi 40 au 50 dhidi ya mabeki bora wa ligi wakati huo. Nilijua ni mchezaji wa kipekee.”
Hasara ya Fiorentina ilikuwa faida ya Roma, kwani Salah aliendelea kuonyesha kwanini alikuwa mchezaji aliyeteka mijadala. Msimu wake wa kwanza Roma ulimalizika akiwa mchezaji bora wa klabu hiyo na 2016/17 uliochanganya mafanikio na changamoto ulimalizika akiwa na mabao 19, akiisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya pili katika Serie A.
KURUDI KWA MFALME
Hii ilikuwa bora Liverpool, ambapo Jurgen Klopp, kocha wa zamani wa timu hiyo alimkaribisha tena katika Ligi Kuu England msimu wa majira ya joto 2017.
Baada ya uchunguzi, Klopp alihitaji kushawishiwa na timu ya uchambuzi ya Liverpool wakiamini Salah ndiye mchezaji bora eneo la ushambuliaji aliyekuwa anapatikana Ulaya wakati huo, huku Klopp awali akipendelea kumvuta Mjerumani mwenzake, Julian Brandt.
Uamuzi wa kumchagua Salah ulithibitishwa mara moja baada ya kushawishiwa kwa kocha huyo, ambapo alimvuta Mmisri huyo kikosini. Aliifunga Liverpool mabao 44 katika mashindano yote msimu wake wa kwanza akitengeneza ushirikiano mkubwa na washambuliaji wenzake, Sadio Mane na Roberto Firmino.
Msimu wa 2017/18 ulikuwa wa Salah akiondoka na tuzo yake ya kwanza ya ufungaji bora EPL maarufu kama Golden Boot na ile ya Mchezaji Bora wa Wachezaji wa Kulipwa England (PFA), huku Liverpool ikijenga timu yenye nguvu ya ushindani. Athari ya Salah pia ilihisiwa nje ya uwanja, ambapo baadhi ya Wamisri waliripotiwa kufikiria kumchagua kuwa rais wao katika uchaguzi mkuu wa 2018.
Utafiti wa Chuo Kikuu cha Stanford ulionyesha Salah huenda alichangia kupungua kwa uhasama dhidi ya Waislamu Liverpool, huku visa vya chuki dhidi ya Waislamu vikipungua kwa asilimia 18.9 kati ya Juni 2017 na Juni 2019. Mnamo 2019, aliingizwa kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani na jarida la Time, na kutumia jukwaa hilo kutetea mabadiliko ya jinsi wanawake wanavyotendewa Mashariki ya Kati.
USIMKATIE TAMAA
Kila kitu alichogusa Salah kiligeuka kuwa bao, lakini msimu wake wa kwanza Anfield haukuwa bila changamoto.
Mwisho wa msimu Liverpool ilipoteza kwa huzuni dhidi ya Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa, mechi ambayo Salah alianza, lakini hakumaliza.
Kuondoka kwake kwa huzuni uwanjani kulizingirwa na mzozo, ambapo Sergio Ramos, nahodha wa Real Madrid wakati huo, alimshika Salah kwa njia isiyo ya kawaida na kumjeruhi shingo eneo jirani na bega la kushoto. Liverpool walipoteza fainali na jeraha la Salah likawa kikwazo cha msimu wake wa joto.
Na hapo alifanikiwa kuonekana mara mbili tu katika Kombe la Dunia, lakini timu ya Misri iliyojengwa kumzunguka Salah aliyejeruhiwa ilimaliza kama kikundi kilichokuwa na uchungu. Msimu wake wa pili Liverpool ulikuwa wa ajabu. Hakufunga kama awali akiwa amepoteza mabao kwenye mechi nane mfululizo. Lakini, mabao 27 msimu huo bado yalikuwa mengi ikizingatiwa na hali halisi.
Liverpool, baada ya uwekezaji mkubwa katika uhamisho wa wachezaji walikuwa tayari kuendana na Manchester City ya Pep Guardiola. Ligi ya ndani ilimalizika kwa huzuni tena, Liverpool ikipoteza taji kwa City licha ya kupata pointi 97 ambazo zingetosha kushinda ubingwa wa ligi katika takriban misimu yote mitatu ya historia ya mashindano hayo kwa miaka 34.
Hata hivyo, Klopp na wachezaji wake walisherehekea ubingwa wa Ligi ya Mabingwa baada ya kuifumua Spurs katika fainali iliyopigwa jijini Madrid, Hispania. Mchakato wa Liverpool kubeba ubingwa ulipata mwanga katika nusu fainali kutokana na ushindi dhidi ya Barcelona ilipoibanjua mabao 4-0 huko Anfield, na kushinda 4-3 kwa jumla ya mabao.
Salah, aliyejeruhiwa na ambaye hakucheza vyema mechi hiyo baadaye alivaa fulana ya rangi nyeusi yenye maneno ‘Never Give Up’ ambayo kwa kweli iliwavutia mashabiki wengi uwanjani. Ushindi wa Ligi ya Mabingwa ulimtia moyo pamoja na Liverpool kushinda taji la EPL msimu uliofuata, ukimaliza kipindi cha miaka 30 bila kuwa mabingwa.
SALAH WA MAKOMBE
Makombe mengine yalifuata kwa Liverpool ikishinda ligi msimu uliopita na kujaribu kupambania matato 2021/22.
Liverpool ilipitia misimu michache yenye changamoto mwishoni mwa enzi ya Klopp, lakini Salah alikuwa kielelezo cha nguvu timu inayoweza kumtegemea kubadilisha matokeo uwanjani.
Mabao yaliendelea kupita katika miguu yake, 16 kati yake dhidi ya Manchester United akiweka rekodi ya mchezaji anayefunga mabao mengi katika mchezo huo wa watani wa jadi England. Hata hivyo, ulimwengu haukumtambua kikamilifu. Kutokuwa kwenye nafasi za juu tatu za Ballon de Or kila mwaka kutabaki kuwa kitisho cha mashabiki wa Liverpool.
Hata hivyo kinachombeba ni umakini wa utunzani mwili wake, mazoezi makali ya gym nyumbani au katika kituo cha mazoezi cha Liverpool Kirkby pamoja na lishe bora vinamsaidia kudumisha kiwango cha juu hata akiwa na umri wa zaidi ya miaka 30.
SALAH BAADA YA KLOPP
Klopp aliwahi kufafanua katika filamu ya BBC ‘Never Give Up’ kwamba Salah kila msimu mpya alikuja na mbinu mpya na ndiyo iliyokuwa siri pekee ya mafanikio yake, lakini baada ya kuondoka kwa kocha huyo 2024, mrithi wake Arne Slot alifaidi kw amuda ubora wa Salah katika kuendelea kuboresha mchezo.
Msimu uliopita, aliifunga Liverpool mabao 34 na kutoa asisti kwa wachezaji wenzake mara 23. Msimu huu umekuwa mgumu kwa Salah. Upungufu wa mabao (10 hadi sasa), kushindwa kuathiri mechi, na muda mdogo wa kucheza kulizalisha mzozo na kocha wa sasa wa Liverpool.
Salah alijitenga na baadhi ya mashabiki, na kulikuwa na mjadala kuhusu kuondoka kwake kabla ya kumalizika kwa mkataba kutokana na uhusiano mbaya na viongozi. Lakini mara uchungu huo utakapopoa, Salah atakumbukwa kama ‘Mfalme wa Misri’ aliyeongoza safari ya Liverpool kurudi kileleni na atabaki kuwa katika hadithi ya klabu isiyosahaulika.