Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbuna: Pacha na SMG Yanga ilikuwa noma na nusu

JANA tuliona namna Fred Mbuna, beki wa zamani wa Yanga aliyedumu ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu kabla ya kustaafu akisimulia safari yake ndani ya timu hiyo.

Mbuna aliyesifika kwa kurusha mipira ‘kama kona’, ni mmoja ya manahodha wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni kocha wa vijana wa klabu hiyo na mwenye kiu ya kutaka kuona vijana wanaopitia mkononi mwake wanakuwa moto kama alivyokuwa yeye.

Leo tunaendelea naye katika hitimisho la mahojiano maalumu naye akianika jinsi walivyotengeneza kombinesheni ya kibabe Jangwani akiwa na pacha wake, Said Maulid ‘SMG’. Kivipi? Endelea naye!


MBUNA VS SMG

Anasema alimpokea Said Maulidi ‘SMG’ 2001-2007 akitokea Simba, alicheza naye miaka minne kabla ya kutimkia kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Onze Bravos ya Angola mwaka 2008-2012.

“Alikuwa winga hatari, malengo na kujitambua ndiko kumetufanya tukutane tena kama makocha wa timu za vijana Yanga, tukiwa na morali kubwa ya kuhakikisha tunawaandaa mastaa ambao watakuja kutikisa ndani na nje,” anasema Mbuna mwenye Leseni B ya ukocha na uongeza;

“Kwa kusaidiana na SMG tunawaelekeza vijana namna wanavyoweza kufurahia matunda ya vipaji vyao, waanzie kubadilika kwenye mitazamo yao kuliheshimu soka linalolipa zaidi kwa sasa, tofauti na zamani, tayari kuna wenzao wapo ligi kuu ambao ni Omary Chibada (Biashara United), James Gubezi (Dodoma Jiji), Abdul Karimu (Mlandege), wawili wapo Yanga ya wakubwa ambao ni Geofrey Magaigwa na Mohamed Msanga,” anasema.


ALIOMBA KUONDOKA YANGA

Anasema mwaka 2011 aliuomba uongozi umwachie, kwasababu alitumika kwa muda mrefu Yanga pamoja na timu za taifa za vijana na Stars yenyewe.

“Kama kuna mchezaji alicheza mechi nyingi za Yanga za timu za taifa mimi ni mmojawapo, nikaona ni wakati wangu sahihi kupata mapumziko, baada ya kuachana na Yanga tu, viongozi wa Moro United wakapata taarifa wakanifuata na kuomba niisaidie timu yao miezi sita, nikakubali,” anasema Mbuna na kuongeza;

“Nilipomaliza miezi sita, nilikaa miaka mitatu bila kucheza soka, baadaye Majimaji wakaniomba nikapandishe timu yao, nikacheza 2015 ikaja ikapanda 2016, nilivyomalizana nao nilikwenda kusomea ukocha, sasa nina Leseni B, ambapo nikafundisha Majimaji tena na timu mbalimbali.”


ALAMA ZA YANGA

Anasema hakumwaga jasho lake bure Yanga ndani ya miaka 11 aliyoichezea, alifanikiwa kujenga nyumba alizopangisha, nyingine anaishi, alinunua magari ya kutembelea na ya biashara aliyoyauza kwa sasa pia ana vitega uchumi vinavyomuingizia kipato.

“Watoto wangu wanasoma shule nzuri, yote hayo ni kutokana na pesa nilizozipata Yanga, bado wakanirejesha kama ‘kit meneja’ na sasa ni kocha wa timu za vijana, kiufupi Yanga ina historia kubwa na maisha yangu, huko kwingine nilipita tu,” anasema.

Mbuna ambaye ni baba wa watoto wanne, Claud (19), Luis (16), Willfred (10) na Junior (5), anasema wawili ndio wanafuata kazi yake ya soka.

“Luis ambaye kwa sasa yupo chuo, anapenda kudaka na Junior wa miaka mitano namchunguza maana mara amecheza hivi mara vile, bado sijajua nafasi inayomfiti zaidi,” anasema.


MASTAA WA SASA

Kutokana na kucheza nafasi tofauti, anawataja mastaa wanaomkosha kwa sasa ni Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba),Y assin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Shomari Kibwana, Farid Mussa, Denis Nkane (Yanga) na Adam Adam (Polisi Tanzania).

“Wananifurahisha sana aina ya uchezaji wao, nawashauri waanze kutazama kuvuka mipaka ya nchi, hilo litawasaidia kulijua zaidi soka la kisasa na wataleta vionjo vipya Stars,” anasema.

Anasema soka la sasa lina utofauti na zamani, miundo mbinu inawasaidia wachezaji kufanikisha ndoto zao kwa haraka endapo tu wakiamua kujituma na kujitambua, wakijua wanaowashangilia wanahitaji kazi zao nzuri na siyo kuvimba mitaani.

“Kuna vifaa vya kila aina vya kumfanya mchezaji kuwa vizuri, mambo ya kukimbia milimani yamepungua, kuna gym, viwanja vizuri, mitandao inayofanya kazi zao zionekane na kila mtu, siyo kama nyakati zetu wanatusimulia waliotuona, laiti kama kungekuwepo video wangejionea wenyewe,” anasema.


HAULE ATHIBITISHA JAMBO

Mwanaspoti likataka kujiridhisha zaidi kwa kumtafuta kipa Benjamin Haule namna alivyosaidiwa majukumu yake na Mbuna baada ya kulimwa kadi nyekundu na anakiri jambo hilo lilitokea kweli.

“Baada ya kupewa kadi nyekundu, nikavua jezi nikampa Mbuna na glovu, nilikuwa natetemeka kwa sababu Toto Africans ingetufunga ningekuwa kwenye wakati mgumu, licha ya kuokoa penalti katika mchezo huo,” Haule na kuongeza;

“Nilikuwa vyumbani, hivyo nikawa nafanya kazi ya kuchungulia huku nikiomba Mungu Yanga isifungwe, ajabu nilishangazwa na namna alivyokuwa anaokoa hatari za washambuliaji wa Toto African, jambo lililomfanya aongelewe na mashabiki wakimshangaa alichokifanya kama kipa.”