Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele, Hakimi kuna kitu, mchongo upo hivi

TUZO Pict

Muktasari:

  • Hafla hiyo inatarajiwa kuanza saa 3 usiku kwa saa za Tanzania huku majina ya mshambuliaji wa DR Congo na Pyramids, Fiston Mayele na Achraf Hakimi wa Morocco na PSG yakipewa kipaumbele katika kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Klabu Afrika na Mchezaji Bora wa Mwaka.

RABAT, MOROCCO: KESHO Jumatano, kuna hafla ya utoaji Tuzo za CAF 2025, itakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Mohammed VI Polytechnic (UM6P) kilichopo Rabat nchini Morocco.

Hafla hiyo inatarajiwa kuanza saa 3 usiku kwa saa za Tanzania huku majina ya mshambuliaji wa DR Congo na Pyramids, Fiston Mayele na Achraf Hakimi wa Morocco na PSG yakipewa kipaumbele katika kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Klabu Afrika na Mchezaji Bora wa Mwaka.

Baada ya mchakato wa awali kufanyika ambapo katika kila kipengele kulikuwa na majina kumi, sasa yamebaki matatu ya mwisho yaliyoingia fainali kila kipengele kuwania tuzo hizo zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na mchango mkubwa walioutoa mwaka huu.

Jopo la wataalamu linaloundwa na wajumbe wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya CAF, makocha wazoefu, Magwiji wa CAF na wawakilishi wa vyombo vya habari waliochaguliwa ndio waliofanya kazi kubwa ya kubakisha majina matatu kila kipengele. Kumbuka haohao ndio wale waliochagua wateule 10 wa awali.

TU 01

Katika vipengele vinavyoshindaniwa, kuna Mchezaji Bora wa Mwaka, Kipa Bora wa Mwaka, Mchezaji Bora wa Klabu Afrika, Kocha Bora wa Mwaka, Mchezaji Chipukizi Bora wa Mwaka, Timu ya Taifa Bora ya Mwaka na Klabu Bora ya Mwaka.

Vipengele hivi vimewekwa upande wa wanaume na wanawake. Pia kuna Tuzo ya Bao Bora la Mwaka inayowaniwa na pande zote mbili.

Mayele anatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kubeba Tuzo ya Mchezaji Bora wa Klabu Afrika kutokana na kile alichokifanya akiwa na Pyramids.

TU 02

Nyota huyo raia wa DR Congo, amemaliza msimu wa 2024-2025 akiwa mfungaji kinara kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akifunga mabao sita yaliyokuwa na mchango mkubwa katika kuiwezesha Pyramids kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Pia Mayele ameiwezesha Pyramids kutwaa ubingwa wa Kombe la FIFA la African-Asian-Pacific baada ya kufunga mabao yote matatu katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Al Ahli ya Saudi Arabia, Septemba 25, 2025.

Oktoba 18, 2025, akafunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 ilioupata Pyramids mbele ya RS Berkane na kubeba taji la CAF Super Cup.

TU 03

Washindani wake ni nyota mwenzake wa Pyramids, Mohamed Chibi ambaye pia anacheza timu ya taifa ya Morocco. Huyu ni beki wa kulia aliyeng'ara wakati Pyramids iliponyakua taji la Ligi ya Mabingwa Afrika 2024-2025, akiwa hodari wa kukaba na kupandisha mashambulizi.

Mwingine ni mshambuliaji wa RS Berkane na timu ya taifa ya Morocco, Oussama Lamlioui ambaye alifunga mabao matano yaliyoisaidia RS Berkane kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2024-2025. Pia alikuwa na mchango wa kuisaidia RS Berkane kushinda taji lao la kwanza la Botola Pro 2024-2025.

Katika hatua nyingine, Lamlioui aliiwezesha Morocco kutwaa taji la CHAN 2024, akiibuka pia mfungaji bora wa mashi-ndano hayo akipachika mabao sita.

TU 04

Katika kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka, Hakimi anashindanishwa na Mohamed Salah na Victor Osimhen ambao ameingia nao fainali.

Hakimi anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hii kutokana na mchango wake wa kuisaidia Paris St Germain kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu Ufaransa maarufu Ligue 1, Coupe de France na UEFA Super Cup, pamoja na kutinga fainali ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA, hayo yote yalikuwa ni msimu wa 2024-2025.

Pia ameisaidia Morocco kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026. Tuzo hizi zinafanyika kwenye ardhi ya nyumbani kwao, itakuwa furaha zaidi kwake kushinda.

Kwa upande wa Salah, ameisaidia Liverpool kutwaa taji la Ligi Kuu ya England msimu wa 2024-2025, akifunga mabao 29 na asisti 18 katika mechi 38, jumla amehusika katika mabao 47. Pia ameisaidia Misri kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026.

Osimhen ameifungia Galatasaray mabao 37 katika mechi 41 msimu wa 2024-2025. Kwa bahati mbaya, hivi karibuni alishindwa kuiwezesha Nigeria kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Hapa kuna vipengele vya wanaowania tuzo hizo ambapo kwa mujibu wa CAF, Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka wa Wanawake, Mchezaji Bora wa Mwaka wa Klabu Wanawake, Klabu Bora ya Mwaka ya Wanawake na Kocha Bora wa Mwaka wa Wanawake, mshindi atajulikana hapo baadaye kutokana na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wanawake inayoendelea nchini Misri.