Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Mexico kulindwa kwa droni, mbwa wa roboti

MEXICO Pict

Muktasari:

  • Mexico, Marekani na Canada zinatarajiwa kuandaa fainali hizo kuanzia Juni 11 hadi July 19, 2026, lakini suala la usalama limekuwa mjadala mzito katika siku za karibuni kutokana na nchi mbili kati ya tatu kujikuta katika migogoro ya kisiasa ambayo inatishia usalama wakati wa mashindano hayo makubwa kabisa kwa ngazi ya nchi kwenye soka duniani.

MEXICO CITY, MEXICO: MIPANGO mipya ya usalama ya Mexico kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kupigwa katika nchi tatu za Amerika inaonyesha kwamba kutakuwa na ulinzi mkali utakaoambatana na vifaa mbalimbali vya teknolojia ya kisasa, huku maandalizi yakiwa yameshika kasi.

Mexico, Marekani na Canada zinatarajiwa kuandaa fainali hizo kuanzia Juni 11 hadi July 19, 2026, lakini suala la usalama limekuwa mjadala mzito katika siku za karibuni kutokana na nchi mbili kati ya tatu kujikuta katika migogoro ya kisiasa ambayo inatishia usalama wakati wa mashindano hayo makubwa kabisa kwa ngazi ya nchi kwenye soka duniani.

Zikiwa zimesalia takriban siku 70, Marekani iliyo vitani kwa sasa dhidi ya Iran, inajiweka katika hatari ya kukumbwa na mashambulio ya makundi ya kigaidi wakati wa fainali hizo iwapo haitasimama kidete kuhakikisha hali ya usalama inaboreshwa zaidi, huku Mexico ikiwa katika mzozo wa ndani wa kisiasa kufuatia kifo cha mmoja wa wafanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya.

Lakini, kinachoelezwa ni kwamba Marekani imeimarisha usalama kuanzia katika viwanja vya ndege ambapo kwa sasa hata sindano tu unayokuwa nayo ndani ya mizigo yako inaweza kukusumbua kuingia nayo nchini humo, kwani ukaguzi wa abiria umeimarishwa zaidi.

Kwa Canada, hali ya usalama ni juu, lakini hakuna matishio makubwa yanayofikiriwa kwa sasa kutoka ndani au nje, lakini ukaribu wake na Marekani kimipaka unaweza kuwa tatizo. Hata hivyo, vyombo vya usalama vya nchi hiyo viko makini.

Wakati hali katika nchi hizo ikiwa hivyo, Mexico imeamua kuwekeza katika teknolojia ambapo imeanzisha maabara maalumu za uundaji vifaa vya ulinzi vya kisasa ikikusudia kuwa na droni, ndege za kisasa na helkopta za ulinzi pamoja na mbwa roboti.

MEX 04

Kumekuwepo na mashaka kuhusu uwezo wa Mexico kuandaa Kombe la Dunia kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa kundi maarufu la biashara za dawa za kulevya ambaye aliuawa na vyombo vya ulinzi vya nchi hiyo.

Kwa sasa mpango mkubwa wa usalama wa Mexico kwa Kombe la Dunia umewekwa wazi kufuatia kuibuka kwa vurugu za magenge ya dawa hizo za kulevya yanayopigana yenyewe kwa yenyewe.

Watu wengi walipoteza maisha katika operesheni ya kumkamata Nemesio Oseguera Cervantes, kiongozi hatari wa kundi la Jalisco New Generation linalojihusisha na dawa za kulevya, pamoja na vurugu zilizofuatia baada ya kifo chake.

Kifo chake kilisababisha ghasia kubwa kutoka kundi hilo zikiwemo kufungwa kwa barabara na kuchomwa moto kwa magari. Wimbi hilo la machafuko lilisababisha wito kwa Mexico kuondolewa haki ya kuandaa Kombe la Dunia.

MEX 03

Nchi hiyo imepangwa kuandaa mechi 13 katika miji mitatu ya Mexico City, Guadalajara na Monterrey. Mexico City itakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi, huku ikipewa uwezekano wa England kukutana na Mexico katika hatua ya 16 bora.

FIFA imekuwa na wasiwasi kiasi cha kutuma ujumbe maalumu kutathmini maandalizi na hatua za usalama za mashindano hayo. Hata hivyo kwa upande wa serikali imelihakikishia shirikisho hilo kwamba itapeleka askari 100,000 kutoka jeshi, polisi na vyombo binafsi ili kulinda mechi zote.

Zaidi ya hayo, magari ya kijeshi 2,100 yatakuwa yakifanya doria katika miji hiyo mitatu, huku ndege 24 za ulinzi na droni 33 zikitumika karibu na viwanja vya michezo. Mexico pia inatumia mifumo ya mawasiliano kuwahakikishia usalama watalii takribani milioni 5.5 wanaotarajiwa kutembelea nchi hiyo wakati wa mashindano.

MEX 02

Kufuatia mipango hiyo, nchi imetangaza kuwa iko tayari kikamilifu kuandaa mashindano hayo.

Kabla ya kuibuka kwa vurugu hizo, maofisa wa Jimbo la Nuevo Leon ambalo Monterrey ni mji mkuu wake walizindua mbwa roboti watakaotumika kuwasaidia maofisa wa usalama wakati wa mashi ndano.

Mbwa hao wa mashine zenye miguu minne zinazoitwa kikosi cha K9-X, zitatumia kamera kuchunguza hatari kabla ya maofisa wa polisi kuingia katika maeneo hatarishi. Mbwa hao waliopangwa kwa programu maalumu watakuwa mstari wa mbele wa ulinzi kwa kutoa taarifa za awali kuhusu hatari zinazoweza kujitokeza.

MEX 01

Baada ya mkutano na maofisa wa FIFA wiki hii, Waziri wa Usalama wa Mexico, Omar Garcia Harfuch aliandika kwenye mtandao wa X: "Tulipitia mifumo ya kiintelijensia, kinga na utekelezaji itakayowekwa wakati wa tukio hili la kimataifa."

Mwishoni mwa Februari, rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum aliwahakikishia mashabiki wa soka dunia kuwa hakuna hatari kwa mashabiki na kwamba, “usalama wote umehakikishwa”  kwa mechi zitakazochezwa Guadalajara.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino anasema ana amani moyoni mwake kwamba, mambo yatakuwa mazuri na mashindano yataendelea kama yalivyopangwa.