Martha: Msuka boli anayetamani kuwa mama ntilie

DODOMA. MMOJA ya wachezaji wakongwe wanaotikisa katika Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) ni pamoja na Martha John, aliyeitumikia timu hiyo kwa zaidi ya miaka saba.
Amekuwa chachu ya mafanikio ya klabu  hiyo tangu ianzishwe mwaka 2015 na Mwenyekiti wa timu hiyo, Innocensia Massawe na Idrisa Kuffor.

Msimu huu amecheza michezo yote ya Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) akianzishwa katika kikosi cha kwanza na Kocha Juma Ikaba na msaidizi wake Shaka Titus.
Martha amekuwa mhimili wa timu hiyo katika vipindi vyote iwe shida ama raha ambapo katika mahojiano yake na gazeti hili amefunguka mambo mengi ikiwemo ombi lake la idadi ya makocha wa kike kuongezwe.

Kisa makocha wa kike
“Sisi ni watoto wa kike tunapokuwa tunaletewa wa kiume kuna nyakati tunakuwa hatuendani nao kwa sababu ni wanaume na sisi ni wanawake,tunaomba sana hata kwa makocha wasaidizi wawe wa kike.

“Ikiwa hivyo inakuwa afadhali unaweza kumwambia kama mwanamke mwenzako kwamba kuna hichi kuna hichi tunaomba sana hili ni muhimu,”anasema beki huyo aliyemtaja nahodha wa Yanga Amina Ally na ndiye aliyemvutia na kuupenda mchezo wa soka.

“Nikiwa nyumbani nilikuwa namfuatilia licha ya kwamba tunacheza namba tofauti  yeye ni kiungo na mimi ni beki lakini nilimpenda na nikajikuta naanza kucheza soka,”anasema beki huyo.

Mama ntilie wakishua
“Napenda sana kuwa Mamantile ambaye nasambaza chakula au nina sehemu yangu nakuwa nauza hii ndio ndoto yangu kubwa ambayo ninayo.

“Baadae nataka pia niwe na mgahawa mkubwa ambao watu watakuwa wakija kununua chakula,hili nataka litimie na kikubwa Mungu aendelee kutupa uzima,”anasem ma kusimulia katika mchezo wa Ligi Kuu ya wanawake dhidi ya Yanga Princess ambapo mshambuliaji wa Yanga Princess Preciuous Christopher alikuwa akimfungisha tela mara kwa mara.
Mchezo huo ulimaliza kwa Yanga Princess kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na  Preciucius mara baada ya kumkimbiza Martha.

“Alinipa wakati mgumu kwa sababu mimi natutumia mguu wa kulia yeye anatumia mguu wa kushoto halafu mwepesi na akipata mpira anakimbilia kwenye 18.

“Kukweli nilishindwa kumkaba lakini kuna nyakati ilinilazimu kucheza rafu,”anasema Martha.
Pia anasema amekuwa akikutana na wakati mgumu kukabana na mashambuliaji wa Simba Queens Oppah Clement kutokana na uwezo wake wa kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga.
Katika kitu asichokipenda ni kufanya mazoezi kwa bidii na mwishowe kutotumika na kufafanua'

“Huwa ninaumia kama mchezaji nimefanya mazoezi nimepambana halafu sipewi nafasi ya kucheza na naona anaecheza ana kiwango kidogo kuliko mimi unajua huwa inakatisha sana tamaa.

Miaka 7 ya Baobab
“Tumepitia misukosuko mingi sana kuna kipindi gari  iliwahi kuwaka moto wakati tukielekea kanda ya Ziwa tulipambana tukatoka wachezaji wote.
“Baadae tuliendelea na safari mpaka tukafuka Kanda ya Ziwa lakini kila mmoja akiwa na hofu.

“Nawapongeza sana viongozi wa Baobab wamejituma na kuipambania timu kuna kipindi familia zao zimelala njaa kwa sababu yetu ili mambo yaende tunashukuru hadi leo timu ipo na maisha yanaenda,”anasema beki huyo ambaye humudu pia kucheza nafasi ya beki wa kati.
Alipulizwa kuna mabadiliko gani kwa maisha yake ya soka na kufafanua;

“Nakumbuka zamani unaweza ukacheza msimu mzima ukapata 40,000 tu na hakuna aliyekuwa akilalamika suala la fedha lilikuwa sio lazima lakini sasa hivi mambo yamebadilika.
“Tunaona wachezaji wa kulipwa wanakuja wanalipwa vizuri na baadhi ya wachezaji wenzetu wanalipwa vizuri tofauti na miaka ile.

Usajili wa Sh 50,000
“Nilipewa 50,000 nilifurahi kwa sababu ndio nilikuwa naanza kucheza nilikuwa nina hamu ya kucheza na soka la wanawake lilikuwa wala halipewi nafasi kubwa tofauti na sasa hivi. Kipaji changu waligundua,Kakolanya Mwambegere  na mwalimu wa shule ya Msingi Mlezi aliyekuwa akiitwa Luhamo.

“Hawa siku zote walikuwa wakinitaka kukazana lakini kipindi hicho zilihitajika juhudi na nilikazana mpaka leo bado naendelea kucheza.
Anamtaja mchezaji Halima Mwaigobole ambaye anacheza nao Baobab kuwa  amekuwa akiwachekesha wakiwa kambini hasa timu inapofungwa ama kupata ushindi.

Aitamani Yanga Princess
“Natamani kuchezea  Yanga kwa sababu naipenda  ina wachezaji wazuri naamini nikienda naenda kupata nafasi moja kwa moja ya kucheza.

“Kulingana na mfumo wao na mimi ninavyocheza naona kabisa pale ni sehemu sahihi kucheza mimi na natamani sana muda huo ufike,”anasema mchezaji huyo anayeweka bayana kwa beki aliyekamilika ni yule anayejua kupiga krosi tamu.

“Mimi nimekuwa bora kwenye krosi kwa sababu nafanya sana mazoezi ukiachana na kwenye  mazoezi ya timu lakinin nami nimkuwa nikifanya mazoezi binafsi.
“Lengo langu   nataka niwe na  mchango katika timu hivyo ni lazima ufanye vitu kwa usahihi,”anasema Martha

Timu ya Taifa
Anasema kutooneshwa kwa ligi ya wanawake kuna wanyima fursa ya kuonekana kwa makocha wa timu za Taifa.
“Natamani sana ligi ioneshwe itaongeza kitu kwetu hata kocha