Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMKM, Azam kuna mtu atashangazwa, rekodi zinaongea

FAMILIA Pict

Muktasari:

  • Timu hizo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar zimepangwa kukutana Oktoba 18, 2025 kwa mechi ya kwanza KMKM ikiwa mwenyeji na kurudiana Oktoba 24, 2025 jijini Dar es Salaam, Azam mwenyeji.

KIMAHESABU hadi sasa Tanzania imeshajihakikishia nafasi moja kati ya nne za kutinga makundi ya michuano ya kimataifa inayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa msimu huu. Nafasi hiyo moja ya uhakika ipo katika michuano Kombe la Shirikisho Afrika.

Hii ni kutokana na ratiba kuzikutanisha Azam FC dhidi ya KMKM katika mechi za raundi ya pili ya michuano hiyo.

Timu hizo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar zimepangwa kukutana Oktoba 18, 2025 kwa mechi ya kwanza KMKM ikiwa mwenyeji na kurudiana Oktoba 24, 2025 jijini Dar es Salaam, Azam mwenyeji.

Nafasi nyingine ya kucheza makundi kupitia Shirikisho Afrika ipo mikononi mwa Singida Black Stars iliyopangwa kuvaana na Flambeau du Centre ya Burundi.

Simba na Yanga zenyewe zitakuwa na vita yao ya kusaka tiketi ya makundi kwa mara nyingine kupitia Ligi ya Mabingwa Afrika.

AZA 01

Timu hizo nazo zimefuzu raundi ya pili, zikipangwa kila kukitana na mpinzani kutoka Ukanda wa Kusini mwa Afrika (Cosafa).

Yanga imepangwa kuvaana na Silver Strikers ya Malawi, wakati watani wao wamepewa, Nsingizini Hotspurs ya Eswatini (zamani Swaziland).

Klabu hizo sambamba na Singida Black Stars zinapaswa kufanya kweli katika mechi zao, ili kupenya makundi na kuandika historia kwa mara ya kwanza Tanzania kuingiza timu nne kwenye michuano ya CAF.

Tayari uhakika upo katika pambano la ‘wanandugu’ wa Azam na KMKM moja kutinga makundi na kuwa rekodi kwa klabu mojawapo, kwani timu hizo hazijawahi kucheza hatua hiyo.

AZA 02

Hata hivyo, wapo baadhi ya mashabiki wa soka wakiipa nafasi kubwa Azam kutinga hatua hiyo kwa mara kwa kwanza, ingawa rekodi zake kwa KMKM, lolote linaweza kutokea.


KWANINI?

Azam na KMKM ni timu zinazofahamiana na mara kadhaa zimeshakutana katika mechi tofauti za kimashindano na hata kirafiki na hakuna anayeweza kumcheka mwenzake.

Mabaharia wa majini wa visiwani ambao kirefu cha jina lao la KMKM ni Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo, katika mechi mbili za mwisho za kimashindano imewanyanyasa Azam.

Ukiachana na mechi za kirafiki za hivi karibuni, rekodi zinaonyesha timu hizo zilikutana mara ya mwisho katika michuano ya Kagame 2021 na zote Azam ilipasuka.

AZA 03

Ilianza kukutana zikiwa Kundi A mechi iliyopigwa Agosti 11, 2021 na Azam kuduwazwa kwa kunyukwa mabao 3-2, licha ya kumaliza kama kinara wa kundi mbele ya KMKM iliyokuwa ya pili.

Azam iliyomaliza mechi hizo za makundi ikiwa na pointi sita, ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Idd Kipagwile dakika ya 41, kipindi kwa kwanza.

Hata hivyo, KMKM ilirudi kipindi cha pili kibabe kwa kupindua meza kwa kusawazisha bao hilo kupitia Haji Simba Salim dakika ya 54 kisha Hasim Ali kuongeza la pili dakika ya 67 na Adam Ibrahim Abdalla akapigilia msumari wa tatu dakika ya 73.

Azam ilipata bao la pili la kufutia machozi dakika ya 83 kupitia Paul Peter aliyepo kwa sasa JKT Tanzania akitokea Dodoma Jiji.

AZA 04

Siku chache baadaye timu hizo zilikikutana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu baada ya kupasuliwa kwenye nusu fainali na Express Uganda iliyobeba taji la msimu huo na Big Bullets ya Malawi.

Katika mechi hiyo iliyopigwa Agosti 14, 2021, Azam ililambwa tena bao 1-0, lililowekwa kimiani dakika ya 77 kupitia Iliyas Mohammed na kuifanya KMKM kulipa kisasi cha kulala mabao 4-0 katika mechi ya makundi ya Komne la Kagame 2014.

Kwa wanaokumbuka, mechi hiyo ya Kundi A ilipigwa Agosti 10, 2014 na John Bocco aliwashtukiza maafande hao wa majini kwa bao la dakika ya kwanza kabla ya straika kutoa Haiti, Leonel Saint Preux kuongeza la pili dakika ya 18 na jingine la tatu dakika ya 29.

Bocco aliongeza chuma cha nne kilichozamisha jahazi la KMKM katika dakika ya 52 na kusababisha mabaharia hao kuaga michuano kwa aibu.

AZA 05

ZINAJUANA

Ukiacha rekodi hizo za kimashindano kupitia Kagame, lakini hizi ni timu zinazojuana na kibaya zinacheza viwanja ambavyo imevizoea na kuleta ugumu kwa kila timu.

Timu hizo zimekutana mara kadhaa katika mechi za kirafiki iwe kwenye Uwanja wa Amaan uliopo Unguja, Zanzibar au Azam Complex, Dar na kila moja imewahi kutoka na ushindi na mechi nyingine kuisha kwa sare.

Licha ya kwamba kwa kuangalia ubora wa vikosi na hata wasifu za makocha kwa anga la kimataifa, Azam kuonekana kuwa juu, lakini soka huwa na matokeo ya kikatili na sikushauri kubeti pambano hili.

Azam inayonolewa na Kocha Florent Ibenge mwenye rekodi tamu katika michuano ya CAF akiwa na timu tofauti, ndiye aliyebeba tumaini la timu hiyo mbele ya KMKM ya Mohammed Hababuu.

Pia Azam inaundwa na wachezaji wenye majina makubwa na rekodi nzuri katika mechi za kimataifa, akiwamo Jephté Kitambala, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Issa Fofana, Barakat Hmid na wengineo.

Hata hivyo, KMKM iliyoasisiwa mwaka 1965 ikiwa na umri wa miaka 60, sio ya kubezwa kwa matokeo iliyopata raundi ya kwanza mbele ya AS Port ya Djibouti.

AZA 06

KMKM ilishinda kwa jumla ya mabao 4-2, ikishinda ule wa kwanza kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini licha ya kuchezwa Amaan na ule wa marudiano kama wenyeji pia ilishinda 2-1.

Timu hiyo ilifika hapo kutokana na msaada mkubwa wa nyota ilionayo akiwamo kipa Nassor ‘Cholo’ Abdullah, nahodha Ahmed Is-haka, Mohammed Hassan, Jumah Khalfan, Abeid Masoud, Mukea Allen, Martin Ather, Mukrim Hassan, Ibrahim Is-haka na wengineo.


HAZICHEKANI SANA

Kizuri zaidi kwa timu hizo ni kwamba hazicheki kwa anga la kimataifa, kwani hakuna iliyowahi kutinga makundi wala kubeba ubingwa wa michuano yoyote ya CAF.

Rekodi kubwa ya Azam katika CAF ni kutolewa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho 2013 na FAR Rabat ya Morocco kwa mabao 2-1 iliyofungwa ugenini baada ya awali kutoka suluhu jijini Dar es Salaam.

Katika raundi ya awali Azam ilipata ushindi wa kishindo wa mabao 8-1 dhidi ya El Nasir ya Sudan Kusini kisha kuitupa nje Barrack Young Controller II ya Liberia kwa mabao 2-1.

Mara nyingine zote zikishiriki Kombe hilo na  Ligi ya Mabingwa Afrika imeishia njiani na safari hii ni sehemu ya kuandika historia kama itachanga karata mbele ya maafande wa KMKM.

Kwa KMKM imerudia mechi za CAF kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 14 ilipocheza mara ya mwisho Kombe la Shirikisho Afrika na kutolewa raundi ya awali kama ilivyokuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2005, 2014, 2015, 2020 na 2022 ilipojitutumua na kung’oka raundi ya kwanza.

Hata kwa mataji iliyobeba timu hizo hazitofautiana sana, japo KMKM inaonekana kuwa bora zaidi kulinganisha na Azam.

KMKM imebeba mataji tisa ya Ligi Kuu Zanzibar ikiwa kinara ikifanya hivyo 1984, 1986, 2004, 2013, 2014, 2019, 2021, 2022 na 2023, pia imetwaa Nyerere Cup mara tatu 1977, 1982 na 1983 na Kombe la Zanzibar (FA) mara mbili 2002 na 2024, mbali na Ngao ya Jamii ikiwamo ya msimu huu.

Hii inaifanya iwe imekusanya zaidi ya mataji 14, ilihali Azam imetwaa taji moja la Ligi Kuu Bara 2014, mawili ya Kombe la Kagame 2015 na 2018 na matano ya Kombe la Mapinduzi ikiwa kinara ikifanya hivyo 2012, 2013, 2017, 2018 na 2019.

Pia imebeba Kombe la Shirikisho (FA) mara moja 2019 na Ngao ya Jamii mara moja 2016.