JICHO LA MWEWE: Muda wa kumruhusu Mbwana Samatta kupumzika jumla?

HATUTAKUWA na nahodha Mbwana Samatta katika pambano jingine la kirafiki pale Azerbaijan. Nahodha wetu ameandika barua ya kutojumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars ambacho kimesafiri mpaka Ulaya Mashariki kucheza mechi za kirafiki za Fifa.

TFF waliafiki kwa niaba yetu. Kwa niaba yetu? Ndio, kwa sababu hata sisi tungependa Samatta apumzike zake. Kuna wanaotaka apumzike kwa vipindi vifupi kama hivi na kuna wanaotaka apumzike jumla. Kwamba labda wakati umefika Samatta akastaafu. Sijui mwenyewe anafikiria nini lakini ukweli wa kwanza ni huu hapa. Samatta yupo sahihi kuomba apumzike katika mechi kama hizi. Kuna namna mbili ambazo wanasoka huwa wanafanya pindi wanapofikisha miaka 31 kwa ajili ya kudumisha urefu wa maisha yako ya soka.

Njia ya kwanza ni kama hii ambayo Samatta anaitumia. Anataka kucheza soka kwa kipindi kirefu katika ngazi ya klabu kwahiyo anajipumzisha kijanja kwa kutosafiri umbali mrefu pamoja na kucheza mechi nyingi ndani ya kipindi kifupi. Njia ya pili ni kustaafu soka la kimataifa na kujikita zaidi klabuni kwako ambako unalipwa mkate wako. Samatta hajatumia njia hii. ameamua kutumia njia ya kwanza ambayo kiukweli kwa umri wake unaweza kusema inakubalika pia. Hauwezi kudai amekosa uzalendo kwa kukosa mechi hizi mbili.

Mwalimu mwingine pia angeweza kumuacha na kuwapatia nafasi vijana zaidi. Hata hivyo Samatta hakutaka kuwapa walimu wakati mgumu akaamua kuachia ngazi mwenyewe japo kwa muda. Na sasa ni wakati pia wa kuanza kutafakari hatima ya Samatta timu ya taifa.

Sisi wengine huwa tunaishia kutafakari tu lakini anayepaswa kutafakari zaidi ni yeye mwenyewe. Na Taifa lazima limpe heshima yeye mwenyewe kuchagua anachofikiri. Kwa taifa kama letu Samatta ni mchezaji asiyegusika. Amejitengenezea heshima hii. Chochote ambacho ataamua mwenyewe sisi tutasikiliza.

Inawezekana anatamani kucheza katika michuano ya Afcon mwakani pale Morocco. Inawezekana moyo wake unamwambia kuwa mwakani sio mbali sana. Lakini pia inawezekana anatamani kucheza katika fainali za michuano ya Afcon zitakazofanyika nyumbani mwaka 2027. Ni miaka mitatu ijayo na atakuwa na umri wa miaka 34 kwa mujibu wa Passport yake.

Hizi za mwakani zinafikisha zaidi. Za mwaka 2027 nadhani miguu itakuwa imemsaliti zaidi kuliko ilivyo sasa. Kama kwa sasa anaamua kutunza nguvu vipi kwa mwaka 2027? Na nadhani wakati huo akina Clement Mzize watakuwa moto zaidi. Na kama ataendelea kuwepo Taifa Stars kuanzia sasa hivi na kuendelea kitu ambacho anapaswa kukubali ni kuachiana nafasi na vijana hawa. Kwa roho ya Samatta ilivyo nadhani hana shida katika hili. Katika mechi za karibuni, hata zile za Afcon zipo nyakati Samatta alikwenda nje kumpisha mchezaji mwingine.

Nadhani hata yeye mwenyewe anajua kwamba miguu inamsaliti. Samatta yule ambaye alikuwa anakokota mpira kutoka nyuma mpaka mbele sio huyu.

Sishangai kuona kwamba huwa hanuni akitolewa nje tofauti na wachezaji wengine ambao kama wangekuwa katika nafasi kama yake katika taifa kama hili angehisi anashushiwa heshima. Na sasa hatima ipo mikononi mwake mwe-nyewe. Sijui anafikiria nini. Chochote ambacho anafikiria binafsi simdai chochote.

Samatta ni alama ya soka katika taifa letu. Inachosha kurudiarudia mara nyingi namna ambavyo aliheshimisha taifa letu kisoka. Zaidi ni kutoka Mbagala mpaka kucheza Ligi Kuu ya England. Kufunga mabao katika michuano ya Europa na Ligi ya mabingwa. Kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji na mengineyo.

Katika timu ya taifa Samatta ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Taifa Stars ambao wameiwezesha Tanzania kushiriki Afcon mara mbili. Ilikuwa ni baada ya miaka mingi ya ubabaishaji lakini hatimaye tulifanikiwa kwenda Misri na mwaka huu tulifanikiwa kwenda Ivory Coast.

Katika michuano ya Misri alifanikiwa kuondoka na bao katika pambano dhidi ya Kenya. Katika michuano hii ya Ivory Coast alifanikiwa kuondoka na pasi ya bao alilompasia Simon Msuva katika pambano dhidi ya majirani zetu Zambia. Unamdai nini mchezaji kama huyu?

Ninachojua ni kwamba inabidi atunze nguvu zake zaidi kwa sababu nahisi ana safari mbili za mwisho kisoka. Nguvu za Ulaya zikipungua anaweza kutimka Ugiriki akaibukia Uarabuni walau kuchota noti kadhaa za waarabu. Soko lao likipo wazi kwa wachezaji ambao wametamba Ulaya.

Bada ya hapo anaweza kurudi moja kwa moja barani Afrika. ni chaguo lake. Anaweza kuamua kurudi nyumbani au anaweza kuamua kucheza katika klabu yoyote ya Bara la Afrika. Nadhani hiyo inaweza kuwa safari yake ya mwisho kisoka kisha akastaafu.

Vyovyote ilivyo itakuwa moja kati ya safari ya kusisimua ambayo imewahi kufanywa na mwanasoka kutoka Afrika Mashariki.

 Achilia mbali Victor Wanyama hakuna mchezaji mwingine wa ukanda huu ambaye amekuwa na historia ya kusisimua kama Mbwana Samatta. Hatuna ambacho tunaweza kumdai. Tatizo letu kubwa ni lile lile tu. Tumeshindwa kumtengeneza Samatta mwingine katika soka.

Mpaka sasa sioni mtu ambaye anaweza kurithi mikoba yake kwa urahisi. Kule nje Kevin John anaonekana kusuasua na amekwama katika kikosi cha vijana cha Genk.

Hapa nchini Mzize yupo katika timu ambao kwa siasa za soka itakuwa ngumu kwake kwenda kucheza nje hasa kwa umuhimu huu anaouonyesha klabuni kwake. Nazifahamu vema siasa za Simba na Yanga.

Kwa Mzize alivyo sasa inahitajika nguvu kubwa kwumng’oa katika kucha za Yanga. Labda ije ofa isiyosameheka kwake lakini kama kuna muda mwafaka kwake kuondoka basi ni huu.