Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu unaweza kuwa mwaka mzuri kwa Brazil

Muktasari:

  • Nchi hizo ni Ujerumani, Hispania, Ufaransa na Argentina lakini timu moja ambayo nitaifuatilia kwa karibu zaidi ni Brazil.

MSOMAJI, fainali za Kombe la Dunia zinakaribia kwa kasi.

Hakika hakuna sherehe kubwa zaidi ya soka duniani kama fainali hizi. Ndani ya wiki mbili macho yote ya mashabiki wa soka ulimwenguni yatakuwa Urusi. Mwaka huu kuna timu nyingi zenye uwezo wa kushinda Kombe la Dunia.

Nchi hizo ni Ujerumani, Hispania, Ufaransa na Argentina lakini timu moja ambayo nitaifuatilia kwa karibu zaidi ni Brazil.

Kwa kweli nitashanga kama sitaiona timu hii katika nusu fainali ya michuano hii ya fainali za Kombe la Dunia. Wote tunakumbuka anguko kubwa la Brazil katika Kombe la Dunia lililopita.

Na hakuna mshabiki wa Brazil ambaye atasahau jinsi nchi yake ilivyofungwa mabao saba kwa moja katika nusu fainali dhidi ya Ujerumani huku wakiwa katika ardhi yao ya Brazil. Lakini, kisaikolojia naamini Brazil imeweza kurudi kutoka aibu ya Kombe la Dunia lililopita.

Katika mashindano ya Olympic yaliyofanyika Brazil mwaka 2016, Brazil ilifanikiwa kurudisha heshima yake ilipoifunga Ujerumani katika fainali na kushinda medali ya dhahabu katika soka.

Bila shaka wachezaji wa Brazil wana hamu kubwa kulipiza kisasi na kushinda Kombe la Dunia mwaka huu na hivyo watacheza kwa moyo mkubwa.

Mwaka 2014 Brazil ilikuwa na kikosi kizuri lakini mwaka huu kikosi chake ni imara zaidi kuliko kile kilichoshiriki fainli zile na kufungwa mabao 7-1 na Ujerumani.

Katika kila nafasi Brazil ina wachezaji wenye viwango vikubwa na itakuwa na wachezaji wengi wenye uwezo wa kubadili sura ya mchezo katika benchi la ufundi kama Douglas Costa, Firmino na Paulinho. Kikosi cha Brazil ni kipana sana mpaka wachezaji kama Hulk, Oscar na Fabinho hawakupata nafasi. Kocha wa Brazil, Tite, amefanikiwa kutengeneza balansi nzuri katika timu yake.

Kama kawaida Brazil inacheza mpira wa kushambulia ikiwa na kati ya washambuliaji bora duniani kama Neymar, Jesus na Coutinho. Lakini, nguvu kubwa ya timu hii ya Brazil ni kwamba nyuma ya washambuliaji kuna wachezaji wenye uwezo mkubwa sana wa kusoma mchezo na kukaba kama Casemiro na Fernandinho.

Viungo hawa wa kati wote ni wakabaji na katika idadi kubwa ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia Tite aliwachezecha pamoja.

Ni kwa kuwa timu nyingi zinapata tabu sana kuanzisha mashambulizi za kushtukiza dhidi ya Brazil kama wachezaji hawa wawili watakuwapo uwanjani.

Na wanawapa washambuliaji uhuru mkubwa zaidi wa kushambulia. Hivyo, naamini Brazil itakuwa timu ambayo itacheza mpira wa kuvutia sana katika michuano hii ya Kombe la Dunia na kutokana na timu yake kuwa na kikosi bora cha Brazil katika miaka mingi naamini ina kila nafasi kutinga fainali na kurudisha heshima ya nchi yao.