Dube atavunja rekodi hizi Azam!

Sunday June 20 2021
dube pic

MSIMU wa 2014/14, Azam FC ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku mshambuliaji wao Kipre Tchetche akifunga mabao 17 akiwa ni kinara wa mabao ndani ya mataji hao wa ligi hiyo.

Si mashabiki wa Azam pekee waliokuwa wanakikubali kiwango cha Kipre bali hata mashabiki wa timu zingine walivutiwa na ubora wa mchezaji huyo awapo uwanjani.

Kutokana na uwezo huo, utajiri wa Azam hakunatimu yoyote kwa wakati huo iliyokuwa na uwezo wa kumng’oa pale Chamazi zaidi ya kuishia kumtamani tu.

Kuondoka kwake kulikuwa pigo kubwa sana ndani ya Azam FC, wengi hawakuona kwa haraka haraka ni nani ambaye angeweza kuziba pengo lake.

Baada ya kupambana kwa muda mrefu kusaka mbadala wa Kipre hatimaye mabosi wa Azam waliangukia Zimbabwe na kumpata Prince Dube kinara wa upachikaji mabao Ligi Kuu akiwa amefunga mabao 14 hadi sasa pamoja na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Dube amefanikiwa kwa kiasi kikubwa Azam wamsahau Kipre hakuna makosa anayoyafanya kila anapopata nafasi ndani au nje ya 18.

Advertisement

Pamoja na ubora wake lakini ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha anavunja rekodi za washambuliaji waliomtangulia wa kigeni na wa ndani ndani ya Azam.


KUTWAA TAJI LA LIGI KUU

Pamoja na moto alionao wa kutikisa nyavu ameshindwa kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutokana na timu hiyo kuishia nafasi ya tatu hata ikishinda michezo yote mitano haiwezi kutwaa taji hilo.

Hivyo rekodi ya ubingwa ameshindwa msimu huu labda kujipanga kwa msimu ujao ama miwili ijayo waliyomuongeza mkataba wake wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ambayo tangu imepanda imetwaa taji moja tu.


REKODI YA KIPRE, BOCCO

Kipre aliyekuwa mchezaji wa mwisho wa Azam FC kutupia mabao 17 kwenye ligi, msimu waliotwaa ubingwa wa ligi 2013/14. Rekodi hiyo kwa nyota wa kigeni hakuna aliyeweza kuifikia japo Dube anapewa nafasi hiyo kama atamaliza michezo iliyobaki baada ya kutikisa nyavu za wapinzani mara 14.

Zimebaki mechi tano kwao ili wamalize ligi, je Dube ana nafasi kuongeza mabao na kuitafuta rekodi ya klabu hiyo kwa msimu ambayo ni mabao 19, inayoshikiliwa na John Bocco tangu msimu wa 2011/12?.


MFUNGAJI BORA

Hadi sasa huu ni msimu wa 13 kwa Azam FC tangu wapande daraja mwaka 2008, imewahi kutoa wafungaji watatu bora, mara tatu mfululizo.

Rekodi ambayo ni muda sasa haijavunjwa na nyota mbalimbali waliopita hapo tangu msimu wa 2010/11, Mrisho Ngassa akifunga mabao 16, msimu wa 2011/12 Bocco alifunga mabao 19 na msimu wa 2012/13. Dube kwenye nafasi ya kuwa Mfungaji Bora ashindwe yeye kwani ana nafasi kutokana na kuongoza kwa upachikaji wa mabao ,michezo mitano iliyobaki anaweza kuongeza.


IMEANDIKWA NA CHARITY JAMES

Advertisement