Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Corazone ndiye Chama wa Simba Queens

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kiungo Clatous Chota Chama, ni mmoja wa wachezaji wanaovutia kuwatazama, msimu hadi msimu amekuwa na kiwango cha juu na siyo jambo la kushangaza kuona akigombewa na miamba ya soka nchini na nje ya nchi hadi sasa akicheza Yanga akitokea kwa watani zao wa jadi, Simba.

NI nadra kuona mchezaji akiwa na mwendelezo wa kiwango msimu hadi msimu. Ni wachache sana na kwa kuangalia viwango vyao, kila msimu wanatabiriwa kufanya makubwa na inakuwa hivyo.

Kiungo Clatous Chota Chama, ni mmoja wa wachezaji wanaovutia kuwatazama, msimu hadi msimu amekuwa na kiwango cha juu na siyo jambo la kushangaza kuona akigombewa na miamba ya soka nchini na nje ya nchi hadi sasa akicheza Yanga akitokea kwa watani zao wa jadi, Simba.

Kwenye soka la wanawake kuna kiungo Vivian Corazone. Tangu ametua Simba msimu wa 2021/22 amekuwa na muendelezo mzuri wa kiwango chake akiwa na uwezo wa kuamua mchezo muda wowote.

Uwezo wa kupiga mashuti ya mbali na namna ya kulitawala dimba la kati linaendana na Clatous Chama ambaye alicheza Simba kwa mafanikio makubwa hususani kwenye michuano ya kimataifa.

Mwanaspoti limekuandikia makala kuhusu nyota huyo wa timu ya taifa ya wanawake ya Kenya ‘Harambee Starlets’.


New Content Item (1)
New Content Item (1)

KAMA CHAMA WA SIMBA

Tangu msimu huo, nyota huyo amekuwa mhimili mkubwa wa Simba kwenye eneo la kiungo ambalo hadi sasa ana utawala wake.

Kama ilivyokuwa kwa Chama ambaye aliweka ufalme wake kwenye eneo la kiungo kiasi ambacho alipokosekana baadhi ya mashabiki waliamini mchezo ungekuwa mgumu.

Ndivyo ilivyo kwa Corazone ambaye anapokuwa uwanjani basi macho ya baadhi ya mashabiki yapo kwake wakimtazama akisakata kabumbu safi.

Mwanadada huyo anapocheza eneo la kiungo wa kati ni ngumu wapinzani kupita eneo hilo kwani anacheza kwa nidhamu kubwa hasa kuzuia.

Uwezo wa kuzuia na kushambulia kwa wakati mmoja unamtofautisha na viungo wengine na kumfanya aendelee kutawala eneo hilo ambalo hadi sasa Simba haijapata mbadala wake.

Kwenye eneo analocheza kuna Riticia Nabbosa raia wa Uganda ambaye amekuwa akianzia benchi kwenye baadhi ya mechi.

New Content Item (1)
New Content Item (1)


ANACHOKIFANYA

Tangu alipotua unyamani msimu huo ambako alikimbia nchini Kenya kutokana na janga la Covid -19 nyota huyo amekuwa na muendelezo mzuri.

Ubora wake umeipa Simba mataji matatu kati ya manne iliyochukua timu hiyo tangu ilipoanzishwa ligi hiyo mwaka 2017.

Misimu miwili nyota huyo alibahatika kuwa miongoni mwa wachezaji waliochukua ubingwa 2021/22 na 2023/24.

Mbali na mataji hayo ya ndani lakini aliifikisha Simba Queens nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu 2022 ukiwa msimu wake wa kwanza kucheza Tanzania.

Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Starlets’ maisha yake ndani ya Simba hayatofautiani na Chama ambaye alikuwa na wakati mzuri akiwa unyamani akiifanya timu hiyo kufika robo fainali tano.

New Content Item (1)
New Content Item (1)


MABINGWA

2017 - Mlandizi Queens

2017/2018 - JKT Queens

2018/2019 - JKT Queens

2019/2020 - Simba Queens

2020/2021 - Simba Queens

2021/2022 - Simba Queens

2022/2023 - JKT Queens

2023/2024 - Simba Queens

2024/2025 - .........?

New Content Item (1)
New Content Item (1)


Rekodi zake

Katika misimu yake akiwa Simba, msimu wa wa 2022/23 alifunga mabao manne na sisti sita, msimu uliofuata alifunga mabao sita na asisti sita, huku msimu huu akiwa amefunga mabao mawili na sisti mbili.


MITINDO

Mbali na kuvutia akiwa uwanjani lakini ni miongoni mwa wachezaji wa kike wenye mvuto hata nje ya uwanja na hapa anaeleza.

“Napenda kuvaa kupendeza, ni mtu ninayependa mitindo na mavazi ambayo naona yatanifaa lakini hata urembo kama hereni na cheni,” anasema Corazone.

Kuhusu ishu ya wachezaji wa kike kujiweka muonekano wa kiume, anasema haoni kama ni suala zuri kwake kwani kipaji ndiyo kinaonekana uwanjani na siyo muonekano wa kiume.

Alisema kuna baadhi ya sehemu huwa wanatumia majina yasiyofaa kwa wachezaji wa kike na kuitaka jamii ichukulie soka ni kama ajira nyingine kwa vijana ambao wanapambania ndoto zao.

“Mimi ni binti sina haja ya kuhangaika na muonekano wa kiume sababu tayari Mungu kaniumba hivi, nitasuka, nitapendeza soka isiwe sababu ya kubadilisha mambo mengine,” anasema Corazone.

New Content Item (1)
New Content Item (1)


HATA KIPA FRESH TU

Corazone mwenye umri wa miaka 24 anasema kutokana na kulipenda soka mara nyingi akiwa mazoezini anafanya vitu vyote ili ikitokea siku mchezaji anaumwa anaweza kuimudu nafasi hiyo.

Nyota huyo anasema mapenzi aliyonayo kwenye soka hata ikitokea kapangwa kucheza eneo la kipa anaweza kukiwasha vyema.

“Watu wamezoea nikicheza kama kiungo, sio hivyo tu, nacheza namba zote uwanjani hata kipa kwa sababu ndiyo kitu nilichochagua kutoka moyoni mwangu,” anasema Corazone.


ALIKOPITA

Soccer Queens (2016/19), Atlético Ouriense ya Portugal (2020/21), Gaspo Youth (2021/22).