Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Christopher Tebandeke: Kuwakaba Libase, Oura sio rahisi

TABANDEKE Pict

Muktasari:

  • Matokeo ya mechi hizo yaliyomalizika kwa 0-0 dhidi ya Yanga na Simba, huku ile ya Singida Black Stars ambayo TRA United ilishinda 2-0, yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na safu ya ulinzi ya timu hiyo kulinda vizuri lango lao kwa kushirikiana na kipa Jean-Noël Amonome.

YANGA, Simba na Azam zinatajwa kuwa ndiyo zenye wachezaji wenye makali zaidi Ligi Kuu Bara msimu huu linapokuja suala la kucheka na nyavu, hilo linathibitishwa na msimamo wa ligi hiyo ulivyo upande wa ufungaji.

Ukiangalia chati ya ufungaji, Prince Dube wa Yanga na Fabrice Ngoy wa Namungo ndio wanaongoza kila mmoja ana mabao manane. Chini yao wenye mabao saba ni Pacome Zouzoua (Yanga), Mudathir Yahya (Yanga), Idd Seleman (Azam), Feisal Salum (Azam) na Saleh Karabaka (JKT Tanzania), kisha Seleman Mwalimu (Simba) na Laurindo Depu (Yanga) wenye sita kila mmoja.

Mbali na hilo, Yanga ndiyo inaongoza kwa kufunga mabao mengi msimu huu ambayo ni 44, ikifuatia Simba (32), kisha Azam (26). Namba hizo zinadhihirisha ni timu zenye wachezaji wa namna gani.

Hata hivyo, kitendo cha TRA United kuzikazia Simba, Yanga na Singida Black Stars zilipokwenda pale Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha kucheza mechi za Ligi Kuu Bara, imeifanya timu hiyo kutupiwa jicho, ina walinzi gani wanaoweza kuwasimamisha vigogo hao.

TABA 04

Matokeo ya mechi hizo yaliyomalizika kwa 0-0 dhidi ya Yanga na Simba, huku ile ya Singida Black Stars ambayo TRA United ilishinda 2-0, yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na safu ya ulinzi ya timu hiyo kulinda vizuri lango lao kwa kushirikiana na kipa Jean-Noël Amonome.

Miongoni mwa walinzi wanaounda safu ya TRA United, kuna beki wa kati, Christopher Tebandeke ambaye anaendelea kuzoea mazingira ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026 ukiwa ni wa kwanza kwake akitokea kwao Uganda.

Beki huyo akiwa tayari amekutana na Simba mara mbili, anasema si rahisi kukabiliana na wachezaji wa timu hiyo hasa wanaocheza safu ya mbele akiwamo Libase Gueye na Anicet Oura.

Msimu huu, TRA United imekutana na Simba mara mbili Ligi Kuu Bara. Mechi ya kwanza ilimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Seleman Mwalimu kwa penalti dakika ya 11, Neo Maema dakika ya 66 na Yusuph Kagoma dakika ya 89 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Elie Mpanzu.

Katika mechi ya pili iliyochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, timu hizo zilitoshana nguvu zikitoka bila kufungana.

TABA 02

Katika michezo yote miwili, Tebandeke alicheza sambamba na beki mwenzake Nasry Kombo ambaye ni nahodha wa kikosi hicho, wakijitahidi kuhimili mashambulizi ya wapinzani wao, ingawa ile ya kwanza hawakuwa na bahati.

Vita yao haijaisha kwani sasa macho yote yanaelekezwa kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB, ambapo TRA United itakutana tena na Simba kati ya Mei 16 na 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Akizungumzia changamoto ya kucheza dhidi ya Simba yenye mastaa kama Libase Gueye, Clatous Chama, Anicet Oura pamoja na Mpanzu, alisema nyota hao wanajua vizuri wanachofanya uwanjani, hivyo inahitaji umakini mkubwa kukabiliana nao.

"Ugumu nilioupata wakati nikicheza dhidi ya washambuliaji wa Simba ni kwa sababu ni timu kubwa hata washambuliaji wanajua nini cha kufanya na mimi kama beki changamoto pekee ninayoipata ni kila dakika inabidi niwe makini," anasema.

TABA 01

"Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wazoefu, ubora wao unanilazimu kuwa makini muda wote ninapokabiliana nao."

Anafichua, baada ya mwanzo kushindwa kukabiliana nao, marudiano aliongeza umakini na ndiyo silaha iliyombeba kuwazuia.

Akiwa anavaa jezi namba 4, mlinzi huyo raia wa Uganda tayari amecheza mechi 15, akianzia benchi mara tatu (moja Ligi Kuu Bara na mbili Kombe la Shirikisho la CRDB), huku akikosa mchezo mmoja pekee katika ligi kati ya mechi 19 za TRA United ilizocheza.

Mbali na majukumu yake ya msingi ya ulinzi, pia amechangia bao moja alilofunga Aprili 4, 2026 dhidi ya Singida Black Stars, jambo linaloonyesha mchango wake pande zote mbili za uwanja ambazo ni ulinzi na ushambuliaji.

Katika kipindi cha mwanzo wa Aprili 2026, Tebandeke alitajwa miongoni mwa mabeki waliopata alama za juu zaidi, akishika nafasi ya kwanza kwa alama 9.4 sambamba na Augustino Nsata wa Dodoma Jiji. Wengine walioingia kwenye orodha hiyo ni Ismail Toure wa Simba (alama 9.2), Lusajo Mwaikenda wa Azam (alama 8.8) na Memory Pillar wa Mbeya City (alama 8.3). Takwimu hizi za Soka Metrics, zinaonyesha wazi ushindani mkubwa uliopo katika nafasi ya beki ndani ya ligi hiyo.

TABA 05

Katika kikosi cha TRA United, mbali na Tebandeke, kuna nahodha Nasry Kombo na Chamou Karaboue anayecheza hapo kwa mkopo akitokea Simba. Hawa wote ni mabeki wa kati wanaocheza kwa kupokezana.

Chamou ambaye ameingia TRA United dirisha dogo la usajili la Januari 2026, ameenda kuongeza nguvu na ushindani eneo la ulinzi ndani ya kikosi hicho ambapo hivi sasa juhudi zako uwanja wa mazoezi, ndiyo unakubeba kucheza mechi.

Hata hivyo, Tebandeke anasema yeye anaridhishwa na maendeleo yake kutokana na nafasi ya kucheza aliyoipata tangu mwanzo na hadi sasa licha ya kwamba inahitaji kujituma zaidi ili kuendelea kuaminiwa.

Beki huyo pia anajivunia kuwa miongoni mwa wachezaji kutoka Uganda anayefanya vizuri katika ligi ya Tanzania, akisisitiza mafanikio yake hayajatokana na juhudi binafsi bali pia mchango wa wachezaji wenzake, benchi la ufundi pamoja na uongozi wa klabu ya TRA United.

"Ninajihisi mwenye fahari kwa kuwa vile nilivyo leo kama mchezaji wa Uganda ninayecheza eneo la beki ndani ya TRA United. Inanifanya nijihisi mwenye furaha lakini si kwa juhudi zangu pekee bali pia wachezaji wenzangu na shukrani za kipekee kwa makocha wangu na siwezi kusahau kuwataja mabosi wa timu yangu kwa sababu wanatoa vifaa vya timu kwa wakati. Kwa kweli, hatupungukiwi. Ndiyo, kwa kweli, hatupungukiwi," anasema.

TABA 03

TOFAUTI YA TANZANIA NA UGANDA

Tebandeke ambaye huu ni msimu wake wa kwanza kucheza Ligi Kuu Bara, amezungumzia tofauti kati ya Ligi Kuu ya Tanzania na ile ya Uganda.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Ligi Kuu Bara inashika nafasi ya tano kwa ubora Afrika, huku ile ya Uganda ikiwa nafasi ya 22. Kwa maoni yake, tofauti kubwa ipo katika uwekezaji na namna ligi zinavyoendeshwa.

Tibandeke anaeleza, licha ya Ligi Kuu ya Uganda kuwa na ushindani, bado haijafikia kiwango cha Tanzania hasa katika suala la uwekezaji na matangazo ya televisheni.

Anabainisha, Uganda, baadhi ya mechi hazionyeshwi, jambo linalowakosesha wachezaji fursa ya kuonekana na kujitangaza kimataifa, lakini upande wa Tanzania, mechi zote za ligi zinaonyeshwa, hali inayosaidia kukuza vipaji na kuongeza ushindani.

TABA 06

"Uganda wakati mwingine mechi nzuri hazionyeshwi kwenye televisheni jambo ambalo linawanyima nafasi wachezaji kujulikana. Kwa hapa Tanzania haipo hivyo, wao wanaonyesha kila mechi. Hilo ndilo ninaloweza kuona kama maoni yangu na tofauti kati ya Ligi ya Uganda na Ligi ya Tanzania," anasema Tebandeke.


WASIFU WAKE

Jina: Christopher Tebandeke

Taifa: Uganda

Nafasi: Beki wa kati

Jezi: Namba 4

Mechi: 15

Benchi: 3 (Ligi Kuu 1, FA 2)

Mechi amekosa: 1 (Ligi Kuu)

Bao: 1 (vs Singida BS)

Timu ya Zamani: UPDF FC