ATM YA WIKI: Curry anatisha uwanjani, benki

ATM YA WIKI: Curry uwanjani, benki

Muktasari:

  • BAADA ya michuano ya NBA kumalizika na Golden State Warriors kuibuka mabingwa, tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo ilienda kwa Stephen Curry.

LOS ANGELES MAREKANI. BAADA ya michuano ya NBA kumalizika na Golden State Warriors kuibuka mabingwa, tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo ilienda kwa Stephen Curry.

Mbali yakuwa bora kiwanjani, Curry, 34, ni miongoni wanamichezo wenye utajiri wa kutosha dunia ni kwa sasa ambapo anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 160 milioni.

Mwanaspoti inakutembeza kwenye kuzitazama mali na biashara mbali mbali anazomiliki na jinsi anavyopiga pesa ndani na nje ya uwanja.


ANAPIGAJE PESA

Kwa sasa anashikilia nafaso ya tano kwenye orodha ya wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani akiwa na wastani wa kuchukua mkwanja wa Dola 92 .8 milioni kila mwaka ambapo Dola 45.8 milioni kati ya hizo zinatokana na mshahara wake huku Dola 47 milioni zinatokana na dili zake zingine ya nje ya uwanja.

Kwa sasa amesaini mkataba mpya na Golden state ambao utamuwezesha kukunja Dola 215 milioni ndani ya miaka minne ambapo kwa miaka mitatu ya kwanza kila mwaka atakuwa anakunja Dola 48 milioni na mwaka wa mwisho msimu wa 2025-16 atapata Dola 60 milioni.

Kwenye sekta ya mikataba mengine minono nje ya kikapu jamaa ni balozi wa Under Armour tangu mwaka 2013 na hapo kila mwaka alikuwa akipata Dola 4 milioni lakini kutokana na ushawishi wake uliozalishia kampuni hiyo faida maradufu mwaka 2017 alisaini mkataba mpya wa pesa ndefu.

Mwaka 2015 pia alisaini mkataba wa ubalozi na kampuni iitwayo Brita, pia ana ubalozi wa kampuni za Unilever/Degree, JPMorgan Chase, Palm, CarMax, Callaway Golf, 2K Sports, na Rakuten.

Ukiachana na madili hayo ya ubalozi fundi huyu pia anatumia pesa zake kuwekeza na kununua hisa kwenye makampuni mbali mbali.


MJENGO

Huenda ndio mchezaji wa kikapu mwenye mjengo wenye thamani zaidi kwani anamiliki nyumba inayokadiriwa kuwa na thamani ya Dola 50 milioni huko Malibu, California, tangu April 2021.

Jumba hilo la kifahari ndani yake lina vitu vingi vya kuvutia ikiwa pamoja na bwawa kubwa la kuogelea, ukumbi wa sinema na sehemu ya kuchezea kikapu.Mbali yake hiyo ambayo ina thamani zaidi Curry pia anamiliki mijengo mingine kibao inayopatikana Atherton, Menlo Park, California ambayo aliripotiwa kuwa anaiuza mapema mwaka huu.

Pia nyumba yake nyingine yenye thamani kubwa ni ile ya San Francisco aliyoinunua kwa Dola 8 milioni.

NDINGA

Tesla Model X 90D- Dola 93,500; Infiniti Q50-Dola 42,100; Porsche 911 GT3 RS-Dola 416,500; Kia Sorento-Dola 39,190; Range Rover Sport LWB -Dola 211,000;

Cadillac Escalade ESV-Dola 79,295; Porsche Panamera Turbo S -Dola 190,200 na

Mercedes-Benz G55-Dola 156,450.


MSAADA KWA JAMII

Mbali ya stori yake ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa NBA mwaka huu, stori nyingine inayoonekana kushika vichwa vya habari duniani kote ni kitendo cha staa huyu kuchangia Dola 100,000 kwenda kwa shule moja huko Ohio ambazo zitatumika kununua vifaa na kulipa makocha wa kufundisha kikapu kwenye shule hiyo.

Mbali uya hilo jamaa amekuwa akisaidia taasisi na kampeni mbali mbali zinazosaidia jamii, miongoni mwa kampeni na taasisi alizowahi kuzisaidia hadi sasa ni Animal Rescue Foundation, Boys & Girls Clubs of America, Brotherhood Crusade, Eat. Learn. Play. Foundation. NBA Cares, Nothing But Nets, Partnership for a Healthier America, United Nations Foundation, V Foundation for Cancer Research


BATA NA UHUSIANO

Yupo kwenye ndoa tangu mwaka 2011 na mrembo mwigizaji Ayesha Curry ambaye wamefanikiwa kupata watoto watatu ambao ni Riley Elizabeth Curry, Ryan Carson Curry na Canon W. Jack Curry.