YouTube wampa tuzo Anjella wa Harmonize

Monday June 07 2021
anjela pic
By Nasra Abdallah

Mtandao wa youtube umempa tuzo msanii Anjella aliyesainiwa na lebo ya Kondegang Worldwide  kwa kufikisha watazamaji 100,000.
Anjella ambaye kwa sasa anatesa na kibao chake cha ‘Nobody’, alionyesha tuzo hiyo kwa mashabiki zake jana Jumapili Mei 7, 2021.
Akiambatanisha picha ya tuzo hiyo ambayo ni ya silver,  ameandika ”Haikuwa kazi rahisi toka nimeianza safari yangu ya mziki rasmi nimeuona upendo wenu wa dhati mashabiki zangu ambao mmejitolea muda wenu kufatilia kazi zangu.
“Asanteni sana upendo wenu umekuwa somo kubwa sana katika maisha yangu na hili limethibitika baada ya kufikisha wafuatiliaji 100,000 kwenye YouTube akaunti yangu (Silver Button Award ),” ameandika Anjella.
Anjella alisainiwa rasmi Machi mwaka huu na lebo ya Kondegang inayomilikiwa na msanii Abdul Rajab ’Harmonize’  na mpaka sasa wameshatoa naye nyimbo mbili ikiwemo ile ya ‘All Night’ na ‘Kama’.

Advertisement