Wema: Sina bifu na Zari
Muktasari:
BAADA ya kuzuka majibizano ya kwenye mitandao ya kijamii baina ya Wema Sepetu na Zari ‘The Boss Lady’ Hassan, staa huyo kutoka katika kiwanda cha Bongo Movies, amesema yeye hana tatizo na mtu.
BAADA ya kuzuka majibizano ya kwenye mitandao ya kijamii baina ya Wema Sepetu na Zari ‘The Boss Lady’ Hassan, staa huyo kutoka katika kiwanda cha Bongo Movies, amesema yeye hana tatizo na mtu.
Akizungumza na Mwanaspoti, Wema alisema kuwa yeye huwa hana sababu ya kujibizana na mtu yeyote na pia siyo mtu wa ‘bifu’ na haoni sababu ya kufanya hivyo ndio maana mashabiki wake wanamkingia kifua.
“Mi’ huwa sina bifu na mtu yeyote na ndio maana kama inavyoonekana huko mitandaoni watu wananikingia kifua, wanaamua kuununua ugomvi kwa kuwa wananijua mimi huwa siyo mtu wa ugomvi ugomvi kwa sababu hauna maana yoyote zaidi ya kujipa hasira sizizo na sababu.
Nina upendo kwa kila mtu, nashangaa mtu anaibuka na kuanza kusema kuwa nina shida ya chakula ndio maana nimekonda, hapana mimi sina shida na chakula ila nimeamua kuwa na mwili huu, waniache kwa sababu nimeupenda mwenyewe kwa kuwa najiona niko sawa, siumwi kitu chochote kwa hiyo simlazimishi mtu mwingine aupende, mwili wangu vile ulivyo nikijipenda mwenyewe inatosha,” alisema Wema.
“Na sijui binadamu huwa wakoje, nilipokuwa na mwili mnene walinisema, sasa nina mwili mdogo bado wananisema, sasa sijui huwa wanataka nini, nashindwa kuwaelewa. Waniache sipendi maneno maneno, “ alisema Wema.
Ugomvi wa Wema na Zari ulianza muda mrefu baada ya Wema kumtuhumu Zari kwamba ndiye aliyemchukulia mpenzi wake Diamond Platnumz miaka kadhaa iliyopita.