Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waghana hawaamini Kanumba amekufa

Mwigizaji nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Hashim Kambi 'Ramsey'

MWIGIZAJI nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Hashim Kambi 'Ramsey' amesikitishwa na hali iliyomtokea nchini Ghana baada ya kugundua kuwa pamoja na kuwa maarufu Bongo, lakini nchini Ghana hajulikani hata kwa waigizaji. Msanii huyo alishtukia hilo alipokuwa Accra hivi karibuni kurekodi filamu ya Day after Death na staa wa filamu za huko, Van Vicker. Alisema msanii wa Tanzania anayejulikana Ghana ni marehemu Kanumba lakini alikutana na kituko kingine pale walipomuuliza habari za Kanumba wakijua kuwa bado yupo hai, ambapo binti mmoja hakuamini kuambiwa kuwa Kanumba ni marehemu. ìTuna kazi kubwa sana kuitangaza sanaa yetu ya filamu, nikiwa Ghana wakati mwenyeji wangu Van Vicker alikuwa akizindua filamu yake nyingine katika ukumbi wa sinema waandishi walikuwa wakimhoji Van mimi ni nani naye alijibu kuwa mimi ni mwigizaji kutoka Tanzania, waandishi walishangaa sana,îanasema Ramsey. Katika filamu ya Day after Death Ramsey kaigiza kama Daktari. Ameigiza na msanii mwingine kutoka Ghana Lidya Forson ambapo kwa sasa Ramsey anasimamiwa na Richard Nwaobi kutoka Hollywood kwenye kazi zake na ameanza kumkutanisha na wasanii wakubwa wa Afrika.