Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vazi la Wema Gigy atajwa, mwenyewe aruka!

Muktasari:

  • Kitu ambacho mashabiki wake walishakisahau kitambo kuonekana akiwa amevaa mavazi yaliyoacha wazi baadhi ya sehemu za mwili, Wema Sepetu sasa amevaa kwenye pati ya tuzo aliyoshinda nchini Kenya iliyofanyika Uncles Masaki jijini Dar es salaam.

Baada ya juzi kuvaa nguo flani hivi, staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu amewatolea uvivu baadhi ya watu ambao wameibuka kwa wingi mtandaoni wakidai chanzo cha yote ni Gigy Money.

Kitu ambacho mashabiki wake walishakisahau kitambo kuonekana akiwa amevaa mavazi yaliyoacha wazi baadhi ya sehemu za mwili, Wema Sepetu sasa amevaa kwenye pati ya tuzo aliyoshinda nchini Kenya iliyofanyika Uncles Masaki jijini Dar es salaam.

Vazi hilo limekuwa gumzo huku baadhi ya watu  wakijiuliza Wema amepatwa na nini, huku wengine wakidai huenda Gigy Money ndiye aliyemshauri wavae hivyo kwani nguo zao zilikua zinafanana kasoro rangi  ambapo Wema alivaa rangi ya bluu ilhali Gigy akivaa  nyekundu.

Wapo waliodai wawili hao siku za nyuma waliwahi kuwa marafiki kabla ya kila mmoja kuchukua hamsini zake.

Wakizungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti, Wema na Gigy walizungumzia vivazi vyao, ambapo Wema alidai: "Hivi watu kwanini (watu) huwa wananionaga mimi sina akili na naomba niwaulize leo hao wanaonishambulia wanaojiona miungu watu walitaka nivae baibui kwenye parti kama ile?

"Maadili gani niliyovunja mimi wakati sehemu zangu za faragha hazijaonekana? Kwa taarifa yao sasa sitaacha kuvaa nguo za hivyo maana nimeona wameipenda

"Halafu sipendi kuambiwa Gigy Money kuwa ananiharibu, kwani mimi ni mtoto mdogo? Wamuache Gigy wala hahusiki na vazi langu na hawezi nishawishi wala kuniharibu, watu wapunguze kamdomo."

Naye Gigy amesema: "Watu sasa wa'shaanza fitina, majungu na masuuria. Yaani nimharibu Wema kwa umri alionao? Hivi kipi hakijui kizuri na kibaya pale alipo? Kwanza zile nguo ziko fresh kama nguo zingine acheni kuharibu furaha za watu."

Mwanaspoti imemuuliza Gigy kwa kumkumbusha maneno machache ambayo aliwahi kusema kipindi cha nyuma walipokuwa marafiki na Wema kwamba anapenda kufeki maisha, leo hii inaonyesha urafiki wao umerudi na imekaaje.

"Tatizo watu hampedi amani. Mimi na Wema tulishasameheana kitambo sana na tunapendana. Yale ya zamani ni maneno ya hasira tu lakini Wema ni mtu 'real' hana feki za kijingajinga kama baadhi ya wasanii wengine," amesema Gigy.