Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tundaman kutoka maokoto ya soka hadi muziki

Muktasari:

  • Tayari ametoa albamu mbili, Neilah (2007) na Nipe Ripoti (2009), huku akipita katika makundi mawili ya muziki, Lafamilia lake Chid Benzi na Tip Top Connection alipotolea albamu yake ya pili. Fahamu zaidi.

TUNAWEZA kusema Tundaman ni miongoni mwa wasanii wachache wa Bongofleva walioweza kubadilika kadri muziki unavyokua kitu kilichomfanya kuwepo masikioni mwa mashabiki kwa takribani miaka 20 sasa tangu atoke.

Tayari ametoa albamu mbili, Neilah (2007) na Nipe Ripoti (2009), huku akipita katika makundi mawili ya muziki, Lafamilia lake Chid Benzi na Tip Top Connection alipotolea albamu yake ya pili. Fahamu zaidi.


1. Kwa Tundaman, ndoto yake kimuziki iliiva zaidi akiwa kidato cha kwanza sekondari ya Forodhani mwaka 2001, msanii wa Bongofleva aliyekuwa anamkubali sana wakati huo alikuwa ni Ferooz ambaye alikuwa anatamba kundi la Daz Nundaz.


2. Siku moja Dully Sykes alikwenda shuleni kwao na kuimba wimbo wake ‘Julieta’, Tundaman alipousikiliza kwa makini akaona mbona hata yeye anaweza kufanya kitu kama hicho, ndipo akazidi kutia bidii katika muziki.

Utakumbuka ‘Julieta’ unatajwa kuwa ndio wimbo wa kwanza wa Bongofleva wa kuimba ingawa wengine wanazitaja nyimbo za Daz Nudaz, ‘Kamanda’ na ‘Barua’ kama ndizo za kwanza.


3. Alijiunga na sekondari ya Makongo kutokana na kipaji chake cha kucheza mpira, baada ya kumaliza akaichezea Friends Rangers ya Magomeni kama kipa. Kacheza sana ndondo unaambiwa fedha kubwa aliyowahi kupata katika ndondo ni Sh50,000 tu. 


4. Tundaman baadaye akakutana na Matonya ambaye tayari alikuwa ameshatoka kimuziki. Matonya akakubali uwezo wa Tundaman na kumshauri waunde kundi lao wawili.


5. Basi Tundaman akakubali wazo hilo, wimbo wa kwanza wa kundi ukawa ni ‘Vailet’ ambao Tundaman ndiye aliuandika tangu kitambo wakaenda studio G Records kwa Roy ili kurekodi, Matonya akarekodi vesi yake vizuri tu.

Changamoto ikaja kwa Tundaman maana alikuwa hajawahi kurekodi, kila akirekodi akawa anashindwa na kukosea mwisho wa siku akaamua Matonya arekodi pekee yake wimbo huo ambao ulikuja kumpa umaarufu mkubwa.


6. Kufuatia wimbo ‘Vailet’ kufanya vizuri Matonya akawa anamchukua Tundaman na kwenda naye kwenye shoo. Kuna kipindi wakaenda Kenya huko mambo hayakwenda vizuri upande wa Tundaman, akaamua kurudi peke yake na kuendeleza harakati zake.

Ikumbukwe wimbo huo (Vailet) ulijumuishwa katika albamu ya pili ya Matonya, Siamini (2006) iliyokuja baada ya kutoa Uaminifu (2003) iliyotengenezwa na Miika Mwamba.


7. Baadaye Tundaman akaja kuibuka Baucha Records na kukutana na Bob Manecky ambaye walikuwa wanajuana tangu muda, hapo akarekodi wimbo wake, Neilah (2006) ila Manecky akamshauri wamtafute msanii wa Hip Hop aweke vesi moja.

Mara akapata wazo la kumshirikisha Professor Jay maana alikuwa anakutana naye kwenye mechi za  Friends Rangers, mwisho wa siku akakutana na Jay na kumsikilizisha wimbo huo na kumuomba ashiriki.


8. Alichofanya Professor Jay ni kumuita Chid Benzi na kumwambia sikiliza wimbo huu (Neila), nataka uweke vesi yako hapa, Chid akakubali kesho yake akaibuka studio na akarekodi, wimbo ulipotoka ukamtambulisha Tundaman.


9. Promota Bonga ambaye pia alikuwa Meneja wa Alikiba wakati huo, ndiye mtu wa kwanza kumlipa Tundaman fedha nyingi za show baada ya kutoa wimbo Neilah, Tunda alikabidhiwa Sh400,000, fedha ambayo alikuwa hajawahi kuishika.


10. HJayati Abdu Bonge ndiye alimshawishi Tundaman kujiunga na Tip Top, alipojiunga akaulizwa ni wimbo gani upo tayari, akasema ‘Nipe Ripoti’ akiwa amemshirikisha Ferooz, Bonge akasema Ferooz katika show atawasumbua hivyo Spark achukue nafasi hiyo.

Wakaenda duka la kanda na kuchukua Sh3 milioni kwa ajili ya kurekodi albamu, na Madee hakupaswa kuwepo katika wimbo huo bali baada ya kuusikia aliupenda na kuamua kuweka vesi yake na ulipotoka ukawa gumzo kila kona na ndio ulibeba jina la  albamu ya pili ya Tundaman.