Selengo: Sanaa ni maisha inahitaji uhalisia

Monday June 13 2022
ben pic
By Olipa Assa

Msanii wa filamu na vichekesho,  Ben Branco Selengo amesema  anapendwa na mashabiki wake, kutokana na kuigiza kwa kuvaa uhalisia kulingana na matukio yanayokuwepo mbele yake.

Selengo anayetamba kwenye tamthilia ya Huba, amesema kazi ya sanaa inatoka ndani ya damu, hivyo anaifanya kwa moyo wa kupenda na kufurahia.

"Ninavyoigiza kuna mashabiki wanadhani ndio maisha yangu halisi, kulingana na kuvaa uhusika inavyotakiwa, nafanya hivyo kwa lengo la kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii," amesema na ameongeza,

"Sanaa ni kazi yenye heshima kubwa duniani, kwasababu licha ya kuburudisha inafundisha namna jamii inavyotakiwa kukaa kwenye mstari.
Amesema kupitia tamthilia ya Huba anapokea maoni ya mashabiki wengi wanaodhani anaishi hivyo maisha yake ya kawaida.

"Niwaambie tu mashabiki ninachoigiza ni tofauti na maisha yangu ya kazi, ingawa ni mcheshi na mtu wa watu," amesema.

Advertisement