Rayvanny kutumbuiza tuzo za MTV EMA 2021

Tuesday November 09 2021
Ray PIC
By Peter Akaro

Msanii wa Bongofleva toka Next Level Music (NLM), Ryamond Mwakyusa maarufu , Rayvanny huwenda akawa ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza katika tuzo za MTV Europe Music Awards  (MTV EMA) 2021.

Hii ni baada ya leo Juamnne Novemba 9,2021, taarifa ya MTV EMA kueleza msanii Maluma toka Colombia atatumbuiza siku hiyo kwa mara ya kwanza wimbo wake, Mama Tetema ambao amemshirikisha Rayvanny.

Tuzo hizo za MTV EMA zinatarajiwa kufanyika Jumapili ya Novemba 14, 2021 nchini Hungary katika ukumbi wa Budapest Spotarena.

Katika tuzo hizo pia msanii Diamond Platnumz, amechaguliwa kuwania katika kipengele cha Best African Act, ambapo kipengele hicho atachuana na Wizkid (Nigeria), Tems (Nigeria), Amaarae (Ghana) na Focalistic (Afrika Kusini).


Advertisement