Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndauka, Shamsa wafikia pabaya

BIFU Pict

Imekuwa kama tamthilia ya ugomvi kati ya Muigizaji na mwanamuziki Rose Ndauka pamoja na rafiki yake Shamsa Ford wakirushiana maneno mara kwa mara mitandaoni.

Kiki, ukweli, wivu pamoja na ushauri hakuna kilichotambulika kwenye ugomvi wao uliopamba moto baada ya Rose Ndauka kuachia ngoma yake ya kwanza 2021 ndipo Shamsa Ford alipomshauri na kusema: “Rose Ndauka anapenda kuimba sio kwamba hajui, ana mwelekeo kidogo na muda utaongea zaidi ila kwangu mimi naona bado kabisa, anisamehe kwa hili bora tuendelee kufanya ‘movie’, mpaka huu mwaka uishe tutaona mengi muziki tuwaachie kina Maua Sama, Nandy na Rosa Ree” alisema Shamsa Ford.

Ila baada ya Rose Ndauka kuachia EP yake ya ‘Majibu rahisi’ mwishoni mwa 2024 maneno yalikuwa mengi shamsa pia aliongea yake akiongezea na ushauri alioutoa hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram jambo lililopelekea kumkwaza Rose na kumjibu kuwa “Ninaishi kwa mipango yangu na kumtanguliza Mungu.”

Kwa hali hiyo mashabiki  zao wamewaweka njiapanda kwa kudhani ni wanaugomvi kweli au ni Kiki ya kupushiana kazi iende mjini?

Huyu hapa Shamsa Ford “Jamani mie nilishasema yule rafiki yangu bado jamani kwenye kuimba haya maneno sio kiki ni siriaz au sipaswi kusema ukweli.”

Kwa upande wa Rose Ndauka hakutaka kuongelea hili suala zaidi ya kusema alichoandika ameshamaliza hivyo ujumbe umefika kwa mhusika ambaye hakumtaja kama ni Shamsa au nani.