Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PRUDENCE KIBAYA:Tunda jipya la Tusker Project Fame 4

PRUDENCE KIBAYA

PHILIP MUYANGA WENGINE hupotea kabisa katika nyanja ya sanaa wanazojihusisha nazo hususan wakiwa wanashiriki michezo ya kutafuta chipukizi bora, al maarufu “talent search events”, na kwa wengine huwa ndio mwanzo wa mafanikio. Ingawa alianza kuimba kabla ya kushiriki katika mashindano ya Tusker Project Fame Season 4, Prudence Kibaya ni mmoja wa wasanii chipukizi ambao maisha yao ya kimuziki yanatarajiwa kuwa bora zaidi siku za usoni. Baada ya kushiriki kwenye mashindano hayo ya TPF4, mwanamuziki huyo chipukizi alitoa kibao kiitwacho 'Nataka Cheza' akimshirikisha mwanamuziki maarufu wa mjini Mombasa aitwaye Labalaa. Licha ya kuwa alikuwa anapenda kuimba, Prudence alijitosa katika dunia ya muziki miaka miwili iliyopita akiwasaidia wasanii wengine katika studio za kurekodia muziki. Katika mahojiano na Mwanaspoti, Prudence anasema kuwa baada ya kusaidia wasanii wengine katika studio, alikuwa akifurahi sana kusikia sauti yake mwenyewe kila mara. Katika kipindi hicho, Prudence pia alifanya 'kolabo' na msanii wa Mombasa, Husler J katika wimbo uitwayo 'Minyororo ya Haki'. Kwa sasa wakati kibao chake kipya kiitwacho 'Shuka' kinavuma nchini, Prudence anakubali kuwa fursa aliyoipata ndani ya TPF4 ilimpatia mafunzo mengi kuhusu muziki. “Mafunzo niliyoyapata katika TPF4 yalikuwa ni mazuri mno, natamani ningekaa humo kwa muda mrefu,” anasema Prudence akiongeza kuwa anatumia aliyojifunza katika TPF4 kuhakikisha anafikia malengo yake katika fani hiyo. Akiwa mwanafuzi wa taaluma ya habari katika Chuo Kikuu cha Mombasa Polytechnic, Prudence anasema kuwa anatayarisha albamu ambayo ananuia kuizindua mwishoni mwa mwaka. Ingawa alizindua kibao 'Shuka', mwanamuziki huyo chipukizi anasema kuwa yuko na vibao vingine ambavyo kwa sasa viko studioni. Kwa sasa, anasema, tayari ana mkataba wa kurekodi nyimbo tano na Grandpa Records huku akiongeza kwamba anajiandaa kufanya 'kolabo' na mwanamuziki mwingine maarufu Afrika Mashariki, Nyota Ndogo. Prudence anasema kuwa anaweza kufanya shoo za muziki katika sehemu yeyote nchini wakati wowote atakapohitajika, lakini akaongeza kwamba anafarijika kutokana na maoni mengi anayoyapata kutoka kwa mashabiki wake kupitia mtandao wa internet. Akaongeza kwamba ananuia kuanzisha bendi yake mwenyewe ya muziki ambayo itawahusisha wasichana peke yao na kuwa na matumaini kwamba huenda akaweka rekodi ya kuwa na kikundi cha wasichana pekee kitakachokuwa maarufu na kutoa burudani. “Kuna bendi nyingi nchini, kuwa na bendi ya wasichana peke yao itakuwa tofauti na zile zingine,” akasema. Prudence aliyekulia mjini Mombasa anasema kuwa anataka kufanya muziki mzuri ambao watu wataukubali na kuufurahia. Akiwa na miaka 23, Prudence anasema atajitahidi kufanya bidii ili kuongeza maarifa ili apande ngazi na kuwa muimbaji maarufu kama walivyo wengine nchini Kenya na ana hamu kubwa ya baadaye kutambulika kote Afrika Mashariki. Kuhusu masomo yake, anasema: “Muziki haujaathiri masomo yangu, naweza kusema kwamba nina wakati wa kutosha kudurusu vitabu vyangu na nina matumaini makubwa ya kufanya vyema masomoni.”