Mwajuma Chaupepo kuleta 'kula ushibe'

MSANII mpya chipukizi wa muziki wa singeli Mwajuma Othman amesema anatarajia kufanya kazi yake ya muziki chini ya kampuni ya michezo na burudani ya Peaktime.
Peaktime awali ilijikita katika masumbwi na sasa imeamua pia kuingia katika muziki na kuanza na msanii huyo. Msanii huyo anayetumia jina la kisanii 'Mwajuma Chaupepo' sambamba na kutambulisha EP yake mpya itakayozinduliwa Ijumaa Ukumbi wa Small Planet Tabata, Dar es Salaam.
Akizungumzua ujio wa Msanii huyo wa pekee katika mziki wa singeli Mratibu wa matukio Bakari Khatibu amesema wameamua kuleta ushindani wa wasanii wanawake katika muziki huo Jumamosi uzinduzi utahamia Lunch Time Manzese.
Aidha Khatibu amesema licha ya peaktime kushughulika na mchezo wa masumbwi hivi sasa wanaleta burudani nyingine ya tofauti kwa mashabiki na wadau wote wa michezo kwani hata mchezo wa Masumbwi umekua ukichagizwa sana na mziki wa singeli.
Mwajuma Chaupepo amesema hadi sasa hajaona Mwana muziki yeyote Mwanamke wa Singeli anayeweza kumpa changamoto kwa upande huo.
EP hiyo yenye jumla ya nyimbo saba ambazo ni 'Ndoa', 'Ndala', 'Hatufanani 'Fresh', 'Singeli Tamu', 'Tatizo Noti', 'Vibe' na 'Baby imehusisha nyimbo binafsi na zile alizoshirikisha wasanii mbalimbali akiwemo Kinata MC, Khalidi Chokoraa, Man Fongo, Seneta na Nini.
Hata hivyo Chaupepo amewaomba watanzania na wadau muziki kumpokea na kusapoti kazi zake ili kufika mbali na kuleta ushindani katika soko la muziki nchini.