Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msaga sumu apata ajali, alazwa MOI kwa matibabu

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwananchi, meneja huyo amesema katika ajali hiyo Msaga Sumu ameumia eneo la usoni.

Meneja wa mwanamuziki wa Singeli, Msaga Sumu, Khalid Ali au Dj Msolopa, amethibitisha msanii huyo kupata ajali huku chanzo chake akidai ni bodaboda.

Akizungumza na Mwananchi, meneja huyo amesema katika ajali hiyo Msaga Sumu ameumia eneo la usoni.

“Taarifa ni za kweli kabisa na kwenye ajali nilikuwepo lakini Mungu amejaalia nimeumia tu kwenye mkono na maeneo ya kwenye mbavu kidogo, sasa yeye (Msaga Sumu) ameumia sana usoni na yupo MOI.

“Wakati tunarudi bodaboda alikatiza mbele yetu kwahiyo dereva katika kumkwepa ndio kuna kitu akaparamia tukapinduka mara tatu. Kwa sasa hali yake sio mbaya yupo vizuri madaktari wanashughulika naye, tunasubiri majibu ya moja kwa moja kutoka kwa daktari,” amesema Dj Msolopa na kuongeza.

“Kwa sasa sitoweza kusema chochote ila yupo sawa kabisa yaani anaongea tofauti na hali ilivyokuwa siku ya kwanza ambayo ni jana wakati tunamtoa Tunduru kumleta Dar es Salaam.”

Taarifa za awali kuhusiana na ajali hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Ngollo Malenya mapema leo ambapo alieleza kuwa msanii huyo alipata ajali jana Ijumaa Mei 16,2025 wakati akirejea Dar es salaam akiwa anatokea Namtumbo kutumbuiza kwenye mkesha wa mwenge.

“Msaga sumu alikuja Wilaya ya Namtumbo Mei 15,2025 kwa ajili ya kutumbuiza usiku wa mwenge wa uhuru ambao ulifika Namtumbo na baadaye Mei 16,2025 asubuhi baada ya kumaliza shughuli yake alianza safari kuelekea Dar es Salaam kupitia Barabara ya Tunduru.

“Walipofika Kijiji cha Azimio, Kata ya Mtina wilayani Tunduru ndipo ajali ilipotokea na Msaga Sumu aliumia na kukimbizwa haraka Hospitali ya Wilaya ya Tunduru na kupata matibabu ya awali ambapo kwenye paji la uso alichanika, akashonwa hapohapo Tunduru Hospitali.

Aliongezea kwa kueleza: “Pia ana maumivu kwenye mbavu hivyo akasafirishwa na gari la wagonjwa kuelekea Dar es Salaam kwa matibabu zaidi, na mpaka sasa hivi ameshafika Hospitali ya MOI kwa ajili ya uchunguzi wa ziada, nimepata taarifa anaendelea vizuri na pia matibabu ya awali yamemsaidia,” amesema Mkuu wa Wilaya Namtumbo, Ngollo Malenya kwenye mahojiano na AyoTv.