Eeh! Jux kufanya sherehe nyingine
Muktasari:
- Jux alisema, mtoto wake Rakeem ni baraka kubwa na kama baba mpya, ana kila sababu ya kusherehekea kwa kiwango kikubwa.
MSANII maarufu wa Bongo Fleva, Juma Mkambala maarufu kama Jux, amesema mashabiki wake waendelee kumfuatilia kwa karibu kwani anaandaa sherehe nyingi zaidi baada ya ujio wa mtoto wake hapa Bongo.
Jux alisema, mtoto wake Rakeem ni baraka kubwa na kama baba mpya, ana kila sababu ya kusherehekea kwa kiwango kikubwa.
“Huyu ni mtoto wangu wa kwanza, lazima nifanye sherehe nyingi zinazomhusu, kwanza nitaanza na sherehe ya kumkaribisha Tanzania na sherehe zangu huwa zina faida hata kwa nchi yetu kwa sababu ninaleta wageni wengi kutoka nje ya nchi,” alisema Jux.
Msanii huyo amekumbusha namna harusi yake iliyofanyika JP ilivyoingiza zaidi ya wageni 200 waliotembelea Tanzania, akisisitiza kuwa tukio la sasa litakuwa kubwa zaidi.
Wiki hii September 24,2025 Jux amemkaribisha mtoto wake Prince Rakeem kwenye ardhi ya nyumbani Tanzania akitokea Canada na alizaliwa huko mwezi mmoja uliopita.
Ujio huo umeambatana na mke wake pamoja na ndugu wengine wa mke wake jambo ambalo limeonekana kuwa la furaha kubwa kwa Jux akielekea kuanza maisha mapya kabisa baada ya ndoa sasa akiwa na mtoto pamoja na mke wake. Jux alifunga ndoa na Priscilla Februari 07, 2025.