Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misambano: Hivi ndivyo alivyougua hadi kifo Ally Star

MISAMBANO Pict

Muktasari:

  • Ally Star alifariki dunia Januari 3, 2026 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na leo mwili wake unasafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao Kichangani wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro.

Msanii wa muziki wa taarabu na Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT), Abdul Misambano amezungumzia kifo cha mwimbaji na mtunzi wa taarabu, Ally Star.

Akizungumza na Mwanaspoti, Misambano amesema Ally Star alikuwa msanii aliyependa furaha na aliyeleta mwanga ndani ya bendi, hali iliyomfanya aheshimiwe na kupendwa na wengi.

Amesema pamoja na utani na ucheshi wake, Ally Star alikuwa mtu wa nidhamu na aliyeheshimu kazi na jukwaa la sanaa.

Msanii huyo amesema dalili za kuumwa kwa Ally Star zilianza kujitokeza kabla za kampeni uchaguzi mkuu mwaka jana, ambapo alianza kulalamika kuhusu hali yake ya afya. Hata hivyo, baada ya kampeni kumalizika, afya yake ilizorota zaidi kiasi cha kuhitaji matibabu kutoka kwa wataalamu wa afya.

"Ally Star ameanza kuumwa miezi minne iliyopita kabla hata ya kampeni za uchaguzi, hivyo katika kampeni hatukuwa naye. Tumemaliza kampeni mkurugenzi wa TOT Khadija Kopa alinipigia simu twende tukamuone," amesema Misambano na kuongeza:

"Tulipofika nyumbani kwake hatukumkuta na hali nzuri ndipo Khadija Kopa akasema tumpeleke katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu. Muhimbili amekaa wiki tatu na nusu ndio amefariki jana."

Akizungumzia tatizo lililokuwa likimsumbua Ally Star, mwanamuziki huyo amesema alipatwa na kiharusi (stroke)' na alikutwa na ukungu kwenye kifua.

Misambano amesema alimfahamu Ally Star tangu 1993 alipojiunga na Bendi ya TOT na tangu wakati huo alionyesha mapenzi makubwa katika muziki wa taarabu akijituma kwa dhati kuitumikia sanaa hiyo.

Amesema kifo cha msanii huyo ni pigo kubwa kwa TOT pamoja na tasnia ya muziki wa taarabu akisisitiza kuwa kazi alizoziacha zitaishi kupitia nyimbo alizoimba na kutunga pamoja na maadili na mshikamano aliowaachia wasanii wenzake.

Ally Star alifariki dunia Januari 3, 2026 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na leo mwili wake unasafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao Kichangani wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro.