Mavazi yampa umarufu D Voice

MAVAZI ya msanii mpya wa lebo ya Wasafi (WCB), D Voice yamekuwa maarufu zaidi mtandaoni kwa mashabiki wanayazungumzia kwa sana.

Msanii huyo aliyetambulishwa na supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Novemba mwaka kabla ya hapo alikuwa anasikika zaidi akiimba nyimbo za singeli ukiwamo ule wa Madanga ya Mke Wangu aliyoimba na Meja.

D Voice alitambulishwa akiwa amefanya albamu ya nyimbo 12 baadhi akiimba na wasanii wa lebo hiyo, akiwemo bosi wake, Diamond aliyeimba naye wimbo wa Kama Wengine ambao ni wa singeli.

Vilevile kamshirikisha Mboso katika biti linaloitwa Mpeni Taarifa, Zuchu ni BamBam, Lavalava ni Turudiane na zote zinafanya vyema kwenye mitandao ya kijamii.

Ingawa unaofanyiwa chalenji zaidi na kinadada mtandaoni ni ule alioimba na Zuchu wa BamBam.
D Voice amekuwa akionekana kwenye mavazi tofauti kwenye mitandao ya kijamii kama utambulisho wake ili kujulikana zaidi kwa mashabiki wake.