Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DAZ Baba: Napitia changamoto nyingi, namkumbuka Mangwair

DAZ Pict

Muktasari:

  • Daz Bana alifanya makubwa sana kiasi cha kuwateka mashabiki wengi, ila kwa sasa yuko kimya kidogo kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Mwanaspoti limemtafuta na kupiga naye stori.

KWA wapenda muziki mzuri wenye ujumbe bila shaka watakuwa na kumbukumbu nzuri za ‘nyimbo za taifa’ kama Barua, Maji ya shingo, umbo namba 8, Nipe Tano Kama hiyo haitoshi, watakumbuka pia wimbo wa majonzi wa Kamanda ambao waliufanya kama Kundi la Daz Nundaz, humo ndani, sauti ya kichwa kinachokwenda kwa jina la Daz Baba kilikonga nyoyo vilivyo. 

Daz Bana alifanya makubwa sana kiasi cha kuwateka mashabiki wengi, ila kwa sasa yuko kimya kidogo kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Mwanaspoti limemtafuta na kupiga naye stori kama ifuatavyo:

DA 05

SABABU YA UKIMYA

"Hapana mimi nipo napambana maana gemu ya muziki ni kama maisha mengine, ni mzunguko, unaweza ukawa juu au ukashuka. Napambana kupanda juu upya japo sio kazi rahisi kwa sasa hasa kuwapata mashabiki wale wa zamani, sasa hivi wengi wameshawatengenezewa muziki wao.

"Kiufupi sijaachana na muziki na siwezi kwa sababu muziki ndiyo maisha yangu, ila ni changamoto tu zilinipitia ndiyo maana nikawa kimya ila napambana bado kama nilivyosema."

DA 01

ISHU YA UNGA

"Nilitegemea hili swali, kiufupi nilishazungumza sana kuhusu dawa za kulevya, yaani imekuwa kama ni wimbo wa taifa kwangu, kikubwa ni changamoto za kimaisha tu zimefanya kuwa kimya."


kuhusu watu kudai afya yake inasababishwa na dawa hizo, anasema; "Acha watu waseme, sasa mimi lini niliwahi kuwa mnene? Ndiyo maana kuhusu ishu za dawa iwe bangi ama nini ni vitu ambavyo siwezi kuzungumzia kabisa, nayasikia sana ya kuambiwa nimekuwa na afya mgogoro sababu ya utumiaji wa bangi nyingi, mwenye afya mgogoro angeweza kutembea sehemu mbalimbali au kujitafutia pesa? Tatizo watu hawabadiliki wanapenda kuishi na historia ya mambo ya zamani."

DA 02

MICHONGO YA SASA

"Kwanza niwaambie mashabiki zangu wasinikatie tamaa, mimi nipo na sasa narudi kama zamani, maana kuna ngoma nimerekodi ndiyo zinamaliziwamaliziwa ili niziachie, sijakaa kimya kizembe kwenye sanaa."

Nje ya muziki je?

"Dah! Kwa sasa sina biashara, ingawa nina michongo yangu ya hapa na pale katika harakati za maisha ikiwemo kujikita kwenye ishu za utalii sana."

DA 03

DAZ NUNDAZ NA YEYE NI HIVI

Kuhusu kushirikiana na Daz Nundaz katika nyimbo hizo na hali ya kundi hilo, anasema; "Hapana niko peke yangu kwa kuwa wenzangu hawapo. Tuligawanyika kwa sababu mkishakuwa timu kila mtu anakuwa na maamuzi yake, basi ikawa kila mtu anataka masilahi ikabidi tugawanyike kila mmoja ila hatuna ugomvi wowote, amani muda wote tukikutana."


ALICHOKIMISI

"Kwenye gemu ninamiss kuruka na mashabiki wangu na ninaamini kwa namna nilivyojipanga sasa hivi nitarudi na kuendelea kama ilivyokuwa awali ni suala la muda tu."

DA 04

AMKUMBUKA ALBERT MANGWEA

"Aisee hakuna mwanamuziki kama Mangwair, huyu jamaa alikuwa ni mtu wa furaha tu, alikuwa hana mambo ya mabifubifu na muda wote alikuwa mtu wa kuimbaimba yaani alikuwa anapenda sana muziki, hadi leo angekuwepo angeendelea kupambana."